Changalucha
JF-Expert Member
- Oct 19, 2011
- 508
- 593
Sidhani kama kujua dini yangu kutafanya uninyooshe maana sijapinda. Lakini msisitizo wangu uko palepale "afya ya akili:". Nilipoona ile 'clip' ya 'Makerubi' wa Mfalme Zumaridi Binti Bundala walivyokuwa wakiruka sarakasi siku alipokuwa anakamatwa nikakumbuka maneno ya BWANA MUNGU ya kuwa "Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa". Hapohapo nikakumbuka tukio la Kanungu, Rukungiri kule Uganda mnamo tarehe 18 Machi mwaka 2000, Nikawakumbuka Joseph kibwetere, Credonia Mwerinde, Angelina Mugisha na viongozi Wenzao wa The Movement for the Restoration of the Ten Commandments of God. Nikawakumbuka waliyoyafanya akina Charles Manson na Jim Jones miaka ya nyuma kule Amerika. Nikawaza habari za imani za Davidian (Davidian faith) na Ukapoliptiki (Apocapyptic belief and Apocalyptic ism).Wewe ni dini gani tuanzie hapo ili nikunyooshe vizur
Juzi tena nilipoona na kusikiliza 'clip' ya mahojiano ya Zumaridi katika mtandao wa Millad Ayo kuhusu jua liwakalo usiku, tughorofa turefu twa dhahabu, magari ya mbinguni nikahitimisha tu kuwa kuna kitu hakiko sawa katika jamii hii na nikawaza sana Serikali za Afrika zilijifunza nini tukio la Kanungu la tarehe 18, Machi mwaka 2000?