Elections 2015 Kinana aanza ziara ktk Majimbo 64. Magufuli aunda kikosi kazi... Mkapa, Kikwete nao wajipanga!

Elections 2015 Kinana aanza ziara ktk Majimbo 64. Magufuli aunda kikosi kazi... Mkapa, Kikwete nao wajipanga!

Joined
Aug 8, 2013
Posts
10
Reaction score
33
Tunapenda kuwataarifu wanachama wetu na umma wa Watanzania kuhusu masuala yafuatayo:

Mwenendo wa Kampeni za CCM

Mgombea Urais wa CCM, Dkt. John Pombe Magufuli, na Mgombea Mwenza, Ndugu Samia Hassan Suluhu, wameendelea kufanya kampeni katika maeneo mbalimbali nchini..

Hadi jana, tarehe 10.10.2015, Dkt. Magufuli alikuwa amekwishatembelea Mikoa 22 na Majimbo 203. Amekwishafanya mikutano mikubwa rasmi 240 na mikutano 865 ya kusimamishwa na wananchi njiani, hasa wananchi wa vijijini. Dkt. Magufuli amekuwa akitumia usafiri wa barabarani, ambapo hadi sasa ametembea kilomita 31,467 kwa barabara kuu, barabara za mikoa, barabara za wilaya, barabara za mlisho (feeder roads), na barabara za mijini na vijijini.

Watu wengi wamekuwa wanajitokeza kwenye mikutano yetu. Lakini la muhimu zaidi ni hamasa na matumaini wanayopata baada ya kumuona jukwaani na kumsikiliza Dkt. Magufuli. Wananchi wanapoondoka kwenye mikutano yetu ya kampeni wanakuwa wamepata fursa ya kumsikia mgombea wetu kwa kitambo kinachotosheleza, wamemuelewa, wameelewa sera za CCM na wameshawishika kukipigia kura Chama Cha Mapinduzi.

Tunaingia katika ngwe ya mwisho ya kampeni zetu. Tangu kampeni zianze hadi sasa, ushindi wa CCM unajidhihirisha. Hata hivyo, katika kujihakikishia ushindi na kuongeza kiwango cha ushindi, katika ngwe hii ya mwisho, tumeanza kampeni nzito.

Katibu Mkuu wa CCM, Ndugu Abdulrahman Kinana, ameanza ziara ya kampeni katika majimbo 64. Vilevile, viongozi wengine wa CCM, akiwemo Rais na Mwenyekiti wa CCM Mstaafu Mzee Benjamin William Mkapa, nao wataanza safari za kuzunguka nchi nzima kumuongezea kura Dkt. Magufuli na wagombea wetu wa Ubunge na Udiwani.

Tutatumia helikopta nne kwa ajili ya shughuli hii. Dkt. Magufuli na Ndugu Suluhu wataendelea kutumia usafiri wa gari hadi mwisho wa kampeni, isipokuwa pale tu itakapokuwa hakuna budi.

Maandalizi ya Kuleta Mabadiliko ya Haraka na ya Kweli

Pia, tunapenda kutoa taarifa kwamba, mgombea wetu, Dkt. John Pombe Magufuli, ameunda jopo la wanataaluma na wataalamu huru magwiji wazalendo wa uchumi, biashara, utawala na sheria, kutoka kwenye taasisi za elimu ya juu, asasi zisizo za kiraia, na sekta binafsi, kwa ajili ya maandalizi ya kufanya mabadiliko makubwa Serikalini kuanzia siku ya kwanza atakayokuwa madarakani.

Dkt. Magufuli amelipa jopo hili majukumu yafuatayo:

1. Kuchunguza na kupendekeza maeneo ambayo Serikali itabana matumizi, ikiwemo manunuzi ya umma, posho za vikao na matumizi ya magari, ili atoe maamuzi kuanzia siku ya kwanza atakapoapishwa;

2. Kuchunguza na kupendekeza maeneo ambayo Serikali itaongeza mapato mara moja bila hatua za kibajeti kuanzia siku ya kwanza atakapoapishwa;

3. Kuchunguza na kupendekeza maboresho makubwa katika mfumo wa utendaji na utumishi na ufanisi katika Serikali;

4. Kupitia kodi na ushuru wenye usumbufu kwa wafanyabiashara wa ngazi zote, wakulima, wafugaji na wavuvi iwapo unaweza kurekebishwa bila kuathiri bajeti ya Serikali inayotekelezwa sasa.

5. Kupitia sheria zote za nchi na kuorodhesha Sheria ambazo zinapaswa kubadilishwa haraka ili kuharakisha mabadiliko ya kweli na ya haraka ambayo ameyaahidi kwa Watanzania;

6. Kupitia na kuorodhesha masuala yote na kero zote zinazosubiri maamuzi ya Serikali ili atoe maamuzi kuanzia siku ya kwanza atakapoapishwa.

7. Kupendekeza miundo na idadi ya Wizara na kutengeneza rasimu za mikataba ya kazi kwa Mawaziri, Makatibu Wakuu na watendaji wengine wakuu atakaowateua mara baada ya kuapishwa.

8. Kupendekeza njia za haraka za kumaliza kero za watumishi wa umma, hasa walimu, askari, madaktari na wauguzi, ili aanze nao kazi wakiwa na ari na morali ya kusukuma mabadiliko ya kweli.

9. Kutengeneza rasimu ya mpango-kazi wa utekelezaji wa Ilani ya CCM na ahadi alizozitoa kwenye kampeni, hasa upatikanaji wa ajira kwa haraka na umeme wa uhakika;

10. Kupendekeza muundo wa kitaasisi na utaratibu muafaka wa kutekeleza ahadi ya kutoa shilingi milioni 50 kwa kila kijiji na mtaa nchini.

Dkt. Magufuli ameazimia kuanza kazi mara moja kwa bidii kubwa na maarifa mapya.


Imetolewa na:-

January Makamba
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa
Mjumbe wa Kamati ya Kampeni

 
Hiyo Ya 5 Kama Kuna Cha Kubadilisha,mchunguze Pia Sheria Ya Mtandao Watu Wawe Huru,ifutwe Au Irekebishwe Maana Imewafanya Watu Weng Kuwa Waoga Hata Kama Walikuwa Na Uwezo Wa Kukosoa Wamejawa Na Uoga.
 
Hiyo Ya 5 Kama Kuna Cha Kubadilisha,mchunguze Pia Sheria Ya Mtandao Watu Wawe Huru,ifutwe Au Irekebishwe Maana Imewafanya Watu Weng Kuwa Waoga Hata Kama Walikuwa Na Uwezo Wa Kukosoa Wamejawa Na Uoga.

Mkuu hebu fikiria wale wanaozushia watu vifo
 
Yameogelewa mchana huu- Lumumba!

Habari kutoka Lumumba zinasema Maraisi Wastaafu wameamua kupanda Majukwaani Kumsaidia Magufuli. Tunawasihi sana Wasitumie lugha za MATUSI VITISHO Na UONGO Kwani wao kama Viongozi hawastahili kufanya hivyo.
 
Yaani mnachunguza wakati mlisema matatizo ya watanzania mnayajuwa...!!!
Anyway baneni matumizi na ongezeni juhudi kwenye haya
1. Fungeni wote wa mishahara hewa
2. Halmashauri zenye hati chafu watieni ndani wote
3. Kamata wakwepa kodi wote
4. Futa misamaha ya kodi
 
Back
Top Bottom