Elections 2015 Kinana aanza ziara ktk Majimbo 64. Magufuli aunda kikosi kazi... Mkapa, Kikwete nao wajipanga!

Elections 2015 Kinana aanza ziara ktk Majimbo 64. Magufuli aunda kikosi kazi... Mkapa, Kikwete nao wajipanga!

namchagua magufuli sichagui ccm hapa kazi tu

Ushalogwa kuwa magafuli si ccm, amka, acha uvivu wa kifikiri.

Magufuli yupo ccm, ccm ileile ya matapeli, mafisadi, wala Rushwa, wezi, majangili, wauza sembe.
 
Magufuli ndio Rais wa awamu inayokuja

Sasa rais ambae amekuja na ilani kabla hajamaliza kuinadi ameitupa pembeni halafu anaandaa tena timu za kufanya uchunguzi na kutoa mapendekezo! Inakuja kwenye akili hiyo? Nadhani njia ya Lowassa ni nyeupe kabisa. CCM wametawala miaka yote na kuwapuuza wananchi leo ndio wanakumbuka kufanya uchunguzi?
 
Ambacho hawajui sasa ni kwamba uchaguzi ni kama umeisha.Wapiga kura almost wote wanajua nani watampigia kura tarehe
25/October.So far hakuna undecided voter thus far!Yaani as we speak..HATA UPIGE PUSH-UP UCHI JUKWAANI..YOU WILL NEVER SWING THE ELECTORATES DECISION MAANA WATU WALISHAAMUA KITAMBOO!
 
Kazi yako mwisho tar 25 Oct, tar 26 Oct utakuwa unahangaika kutafta kazi nyingine
Sina wasi na kazi. Mimi nakula pensheni hapa! Wewe ndiyo utasaga meno alfajiri ya 26/10/2015 na Yuda wenu atakuwa anatafuta mbinu ya kurudisha vipande baada ya kuuza chama.
 
Nikisikia neno ccm nakumbuka bunge la katiba chuki inazidi hasa nikimuona yule mama mwenza..hebu jaribu kukumbuka alivyokuwa naibu mwenyekiti maneno yake
 
Mambo yote anayo yazungumzia wakati huu yalitakiwa yafanyiwe kazi miaka 10 iliyopita. Hakuna mtanzania atakaye kwenda kurudi nyuma katika safari ya kukiondoa chama hiki dhalimu. Dakika zilizo baki hata CCM wakaamua kwenda kuinunua nchi ya Uingereza yote na kuimiliki hakuna mwana mabadiliko yoyote atakaye kwenda kubadirisha uamuzi wa kuki nyima kura Chama Cha Mapinduzi.
Kabisa mkuu. Au angalao kwenye ilani yao ya sasa ilitakiwa wawe wameshafanya huo uchunguzi na waje na suluhisho... tutafanya 1...2....3...
Sio tena kuanza kutafiti... Hii inaonyesha kuwa CCM wanasema kwa mdomo lakini matendo ni sifuri
 
Wagombea wao hawawezi kutumia chopa,maandalizi ya kuzombea watu yatakuwa finyu,Makofuli amepewa ushauri na daktari asijaribu kupandapanda chopa.
By the way Lowassa anashinda uchaguzi asubuhi asubuhi.

Kupanda chopa ni kazi ngumu kuliko kupiga pushup majukwaani.
 
Yaani mnachunguza wakati mlisema matatizo ya watanzania mnayajuwa...!!!
Anyway baneni matumizi na ongezeni juhudi kwenye haya
1. Fungeni wote wa mishahara hewa
2. Halmashauri zenye hati chafu watieni ndani wote
3. Kamata wakwepa kodi wote
4. Futa misamaha ya kodi

Yap,, huu ndio upinzani wa kweli,, unakosoa na kutoa solution,, ushauri wako wameuona bila shaka wataufanyia kazi!!
 
Haaaha yani mnategemea mkapa atabadili akili za watu au kinana aisee mkapa huyu huyu aliewaita malofa
 
Sina wasi na kazi. Mimi nakula pensheni hapa! Wewe ndiyo utasaga meno alfajiri ya 26/10/2015 na Yuda wenu atakuwa anatafuta mbinu ya kurudisha vipande baada ya kuuza chama.

Hiyo pension unaitoa wapi, wakati mtashindwa mapema asbh
 
Maji ya shingo au ndo maji yamezidi unga...??? Mwaka huu mtakoma kujua EL
 
Labda kwa jicho moja tuone hivyo,Labda kwa jicho lingine tuone kama matokeo yalishaamuliwa kabla ya kampeni kuanza.Watoto wa mjini wanasema "CCM walikuwa wanatuejoy, walishapanga matokeo kabla ya mechi".

Soma hapa

Mgombea urais wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dk John Pombe Magufuli.

Mgombea urais wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dk John Pombe Magufuli ameunda jopo maalumu la wanataaluma na wataalamu kutoka kada mbali mbali ikiwa ni maandalizi ya uundaji wa serikali yake endapo atashinda urais.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa CCM, January Makamba alisema kuwa jopo hilo la wanataaluma na wataalamu wa uchumi, biashara, utawala na sheria, kutoka kwenye taasisi za elimu ya juu, asasi zisizo za kiraia, na sekta binafsi, wamepewa majukumu maalumu ya kufanya mabadiliko makubwa serikalini kuanzia siku ya kwanza ambayo Magufuli atakuwa madarakani.

Makamba ameyataja baadhi ya majukumu hayo kuwa ni


Dkt. Magufuli amelipa jopo hili majukumu yafuatayo:

1. Kuchunguza na kupendekeza maeneo ambayo Serikali itabana matumizi, ikiwemo manunuzi ya umma, posho za vikao na matumizi ya magari, ili atoe maamuzi kuanzia siku ya kwanza atakapoapishwa;

2. Kuchunguza na kupendekeza maeneo ambayo Serikali itaongeza mapato mara moja bila hatua za kibajeti kuanzia siku ya kwanza atakapoapishwa;

3. Kuchunguza na kupendekeza maboresho makubwa katika mfumo wa utendaji na utumishi na ufanisi katika Serikali;

4. Kupitia kodi na ushuru wenye usumbufu kwa wafanyabiashara wa ngazi zote, wakulima, wafugaji na wavuvi iwapo unaweza kurekebishwa bila kuathiri bajeti ya Serikali inayotekelezwa sasa.

5. Kupitia sheria zote za nchi na kuorodhesha Sheria ambazo zinapaswa kubadilishwa haraka ili kuharakisha mabadiliko ya kweli na ya haraka ambayo ameyaahidi kwa Watanzania;

6. Kupitia na kuorodhesha masuala yote na kero zote zinazosubiri maamuzi ya Serikali ili atoe maamuzi kuanzia siku ya kwanza atakapoapishwa.

7. Kupendekeza miundo na idadi ya Wizara na kutengeneza rasimu za mikataba ya kazi kwa Mawaziri, Makatibu Wakuu na watendaji wengine wakuu atakaowateua mara baada ya kuapishwa.

8. Kupendekeza njia za haraka za kumaliza kero za watumishi wa umma, hasa walimu, askari, madaktari na wauguzi, ili aanze nao kazi wakiwa na ari na morali ya kusukuma mabadiliko ya kweli.

9. Kutengeneza rasimu ya mpango-kazi wa utekelezaji wa Ilani ya CCM na ahadi alizozitoa kwenye kampeni, hasa upatikanaji wa ajira kwa haraka na umeme wa uhakika;

10. Kupendekeza muundo wa kitaasisi na utaratibu muafaka wa kutekeleza ahadi ya kutoa shilingi milioni 50 kwa kila kijiji na mtaa nchini.

Dkt. Magufuli ameazimia kuanza kazi mara moja kwa bidii kubwa na maarifa mapya.
 
Back
Top Bottom