Tetesi: Kinana agoma kufika mbele ya Kamati ya Maadili ya CCM

Tetesi: Kinana agoma kufika mbele ya Kamati ya Maadili ya CCM

Status
Not open for further replies.
Lile azimio lililotolewa na Halmashauri Kuu ya Taifa kuhusu kuhojiwa kwa Makatibu Wastaafu, CCM ingelitafakari kwa maakini kwa vile lilitolewa kwa mihemuko. Azimio lilitolewa ili wengine waonekane wamezungumza kwenye kika.
 
K
Lile azimio lililotolewa na Halmashauri Kuu ya Taifa kuhusu kuhojiwa kwa Makatibu Wastaafu, CCM ingelitafakari kwa maakini kwa vile lilitolewa kwa mihemuko. Azimio lilitolewa ili wengine waonekane wamezungumza kwenye kika.
Kwa namna ya chama cha CCM kinavyoendeshwa hivi sasa, lile azimio limetolewa na Mwenyekiti wao na wajumbe wa NEC "walilazimishwa" kuliunga mkono hata kama wengi wao hawakuliafiki
 
Sijawahi kuona mwanajeshi anaekubali kuburuzwa na asiye mwanajeshi aliyemzidi cheo.

Nionavyo, namna pekee ya kuwahoji hao wazee ni kuwaomba miadi (appointment) na kuwafata majumbani kwao, kwa heshima zote wanazostahiki kwa umri wao na nyadhifa zao walizostaafu, na kufanya nao mahojiano ya kistaarabu.

Huwezi kuwaweka kitimoto hao wakakubali. Hawana cha kupoteza.
Hili nalo neno

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sijawahi kuona mwanajeshi anaekubali kuburuzwa na asiye mwanajeshi aliyemzidi cheo.

Nionavyo, namna pekee ya kuwahoji hao wazee ni kuwaomba miadi (appointment) na kuwafata majumbani kwao, kwa heshima zote wanazostahiki kwa umri wao na nyadhifa zao walizostaafu, na kufanya nao mahojiano ya kistaarabu.

Huwezi kuwaweka kitimoto hao wakakubali. Hawana cha kupoteza.
Maneno sahihi sana haya.

Faiza mbona kuna wakati huwa unaandika vioja vya ajabu? Huwa anaamua tu kujitoa ufahamu?
 
MAKATIBU wakuu wastaafu wawili wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana na Yusuf Makamba, wamejivua uanachama wa chama hicho.

Habari zilizoifikia SAUTI KUBWA zinasema Kinana na Makamba walijiondoa rasmi CCM kwa maandishi. Barua zao, kila mmoja na ya kwake, zilifikishwa ofisini kwa Katibu Mkuu wa CCM tarehe 7 Februari 2020.

Chanzo kinachoaminika kutoka CCM Makao Makuu kimeiambia SAUTI KUBWA: “Barua zao zimefika kwa nyakati tofauti, zimepokelewa. Lakini inaonekana kama walikuwa wameziandika muda mrefu baada ya kushauriana, maana zinafanana na zimewasilishwa siku moja. Taarifa hizi zilipofikishwa kwa Mzee (Rais John Magufuli) zilimvuruga kwa kweli.”

Kwa mujibu wa chanzo hicho, ambacho hakitatajwa hapa, Rais Magufuli, baada ya kupokea ujumbe wa Kinana na Makamba kujivua uanachama, aliwaomba wazee wawili waandamizi – Rais Mstaafu Benjamin Mkapa na Spika Mstaafu Pius Msekwa – wamsaidie kuzungumza na akina Kinana ili kuwashawishi wabadili msimamo wao.

Hata hivyo, Kinana na Makamba wamegoma kusikiliza ushawishi wa mtu yeyote. Katika barua zao za kujiondoa CCM, kwa mujibu wa chanzo chetu, Kinana na Makamba waliambatanisha pia kadi zao za uanachama.

“Tayari wameturudishia kadi zetu, maana yake wao si wanachama wetu tena,” kimesema chanzo hicho.

Kinana na Makamba ni miongoni mwa makatibu wakuu wanaoheshimika katika CCM, wenye ushawishi, na ambao wametumikia nchi katika nyadhifa mbalimbali kuanzia jeshini hadi serikalini na kwenye chama.

Siku ambayo walikabidhi barua na kadi zao na kutangaza rasmi kujiondoa CCM, ndiyo siku walipotarajiwa kuhojiwa na Kamati ya Maadili ya CCM iliyoagizwa na Rais Magufuli katika kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM (NEC), ili wajieleze kuhusu waraka walioanidika kwa Baraza la Wazee la chama hicho wakilalamikia kubezwa na kudhalilishwa na mhuni mmoja anayetumia jina la rais kudhihaki na kushambulia wakosoaji wa rais na serikali.

Mbali na Kinana na Makamba, mwingine aliyeitwa kuhojiwa na kamati hiyo ni Bernard Membe, waziri wa zamani wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, ambaye aliunga mkono waraka wa wazee hao, na pia alidukuliwa akizungumza katika simu mambo ambayo hayakumfurahisha Rais Magufuli.

Yeye alikutana na kamati hiyo Mjini Dodoma Ijumaa tarehe 7, Februari 2020; na baada ya mahojiano alionekana mwenye kujiamini na mwenye furaha. Mmoja wa wajumbe walioshiriki mahojiano hayo amezungumza na SAUTI KUBWA kwa sharti la kutotajwa, akisema: “Tulijuta kumuita Membe. Kuna maswali amehoji na masuala amezungumza nasi hadi tukahisi yeye ndiye anayetuhoji. Ukweli ni kwamba chama chetu kinahitaji mabadiliko makubwa ya kimsingi, maana kuna shida mahali. Bwana mkubwa anatupelekesha, na watu jasiri wa kumwambia ukweli hawapo, tunaishia kuagizwa tu, hata kutenda mambo yaliyo kinyume cha misingi ya CCM. Membe ametukumbusha yote haya. Kwa kweli, sijui kinachoofuata.”

Hata hivyo, SAUTI KUBWA iliambiwa wiki iliyopita kuwa agizo la kamati kuwahoji wakongwe hao lilikuwa kama igizo tu, kwani Rais Magufuli na watu wake walishaamua kuwa Membe na Kinana wavuliwe uanachama, na Mzee Makamba apewe onyo kali.

Kwa Kinana na Makamba kujivua uanachama na kugoma kuhojiwa, wamewaza hatua mbili mbele ya Magufuli. Chama hakiwezi kuwahoji kwa kuwa wao hawafungwi tena na nidhamu wala maadili ya CCM kwa kuwa si wanachama CCM.

Ingawa barua zao zilipelekewa kimya kimya, na uongozi wa juu wa CCM umekuwa unahangaika kuzuia taarifa hizi kuvuja, zilivuja mapema mno; na kitendo chao cha kutofika mbele ya kamati kuhojiwa kimezua maswali na mjadala mpana ndani nanje ya CCM.

Baadhi ya wadau wa siasa za Tanzania wanasema inawezekana kitendo hiki kikawaingiza wote wawili, au mmoja wao, kwenye matata makubwa, kwani uongozi wa CCM ni wa visasi, unaweza kutaka kuwakomoa na kuwadhalilisha.

Profesa mmoja wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam amesema: “Tusishangae sasa kusikia siku moja Kinana au Makamba wametiwa mbaroni na wanashitakiwa kwa utakatishaji fedha, maana hii ndiyo fimbo mpya ambayo inatumika kuumiza wanaotofautiana na watawala. Lakini iwapo watashitakiwa umma utajua kuwa sababu hasa si uhalifu wao bali ni hii barua yao na uamuzi wao.”

Kiongozo mmoja mwandamizi wa CCM ameiambia SAUTI KUBWA: “Kiukweli, Mzee Kinana na Mzee Makamba hawana cha kupoteza. Nadhani sisi ndio tuna cha kupoteza, maana ukisoma waraka unaowasababishia haya yote utagundua kuwa wao ni watetezi wa misingi ya chama chetu. Wanachotetea ndicho wanaCCM wote tunapaswa kutetea, lakini sasa tofauti iliyopo kati yetu na wao ni kwamba wao wameonyesha ujasiri ambao sisi hatuna. Wengi wetu tumebaki kutii maagizo ya bwana mkubwa, huku chama kinaporomoka!”

SAUTI KUBWA inatambua kuwa kuna mtifuano mkubwa ndani ya CCM ambao haujawahi kutokea tangu uwepo wa chama hicho, ingawa wanafanikiwa kuufunika kwa kutishana – kwa kutumia vuombo vya dola.
Naona akina Kinana "wamemkata" Magufuli kwa mtindo uleule wa kustukiza kama ambavyo yeye alivyowakata Nape na Mwigulu kwenye baraza la mawaziri. Maguduli kasema "Suuuh..!" na wao wamesema "Swaaah..!" Au wakae pamoja na "kuanza upyaaaa!"
 
Komredi Kinana kaona utoto kwenda, hata wakimpa adhabu ya kumfuta uanachama bado ni alama tosha ya CCM hata asipokuwa na kadi! Sio watu Kama Bashite,Kitila, Waitara, Bashiru, Pole pole ambao hata hadhi ya ushabiki wa chama hawana hata wakiwa na kadi!

Kwa Membe it's ok kwenda bado ana future ndani ya Chama. Nahisi soon Komredi Mangula ataomba kujiuzulu kupisha siasa za 'kihuni' ndani ya Chama.
Mkuu ongeza idadi ya wajumbe hapo..tafadhar!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yaani wazee Makamba,Kinana,wakubali kuhojiwa na wahuni wachumia tumbo, Bashiru, polepole na wahuni wenzao wasiokijua hata chama , thubutu,Jiwe lichama lako hilo.
 
Hatareee


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Kwanza mpaka sasa bado hakuna uthibitisho kuwa hili ni kweli, lakini ikitokea likawa kweli, Kinana na Makamba wakajitoa CCM kwasababu ya kile kinyangarika, then huu utakuwa ni uthibitisho kuwa wamegundua kile kinyangarika kinatumwa tuu, hivyo ili kulinda heshima zao, wakaamua kujiepusha na CCM na kumwachia vinyangarika na anayewatuma

Kitendo cha watu waliokipigania chama kwa machozi, jasho na damu katika maisha yao yote, halafu, wakaja kuchafuliwa na kudhalilishwa na kinyangarika fulani ambacho kinatumwa, karma ya Kinana na Makamba ni kubwa, hivyo kama hii ni kweli, then just sit and watch jinsi karma itakavyo kishughulikia hicho kinyangarika na anayekituma!.
P
Pascal mbona unajitoa akili , hapa karma haina nafasi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lakini kumbuka Mwenyekiti wa chama chao ndiye amebariki haya.

Zingatia pia mwenyekiti wa chama ndiye Amir jeshi mkuu. Sidhani kama hapo kuna anayemzidi cheo kwa namna yeyote ile.

Lakini uungwana,hekima na busara ni jambo jema kadiri ulivyopendekeza.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama nimeelewa sawasawa, ni kwamba:

Mwenyekiti amewafokea Polepole, Bashiru na wajumbe wa kamati, lakini zaidi amefokewa Polepole kwa kuhidlsiwa kuwa ndiye aliyevujisha siri.

Kinana na Makamba wameandika barua za kujiondoa kwenye chama kwa maana ya kustaafu siasa. Kamati baada ya kupilokea barua zao ikawaomba kuwa wasiliseme jambo hilo kwa umma, nao wakawaambia kuwa, na wao (wajumbe wa kamati) wasiseme juu ya jambo hilo.

Cha kushangaza baada ya muda mfupi, jambo tayari limetoka na watu wanajua. Mwenyekiti amechukia, na kuwafokea sana Polepole na Bashiru, kiasi cha bwana Bashiru kuondoka ofisini na kwenda kupumzika.

Hivi ndivyo nilivyoelewa.


Duh haaaa najaribu kufikiri namna Polepole alivyokuwa mdogo kama piriton na mnyonge kama mshitakiwa aliyehukumiwa kifungo cha miaka 10 jela na adhabu ya kuchapwa viboko vingi.
 
Mtu akichukuliwa hatua bila kusikilizwa atasema sikupewa nafasi ya kusikilizwa.
Kaitwa asikilizwe anaona anaonewa kuitwa kusikilizwa Kama mtu anamalalamiko Lazima aitwe asikilizwe. Ili aeleze malalamiko yake.
Anataka aitwe Musiba kwenye chama ndio nayeye aitwe? Naona kama hoja hainamashiko kabisa ya kuitwa Musiba huenda Musiba anakesi mahakamani na chama hakiingilii hilo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu walikuwa wanamwita ili wamsikilize au wanamhoji kwa tuhuza wanazotoa,mbona hueleweki

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mangula wakina JK walivyomuweka kando alirudi kwao akawa mkulima wa Nyanya unadhani anahamu kurudi huko?

Sasa hivi upepo wa V8 24/7 huku mashati yake ya 'bahama' yakimeremeta,tumikia kafiri upate mradi wako.
Komredi Kinana kaona utoto kwenda, hata wakimpa adhabu ya kumfuta uanachama bado ni alama tosha ya CCM hata asipokuwa na kadi! Sio watu Kama Bashite,Kitila, Waitara, Bashiru, Pole pole ambao hata hadhi ya ushabiki wa chama hawana hata wakiwa na kadi!

Kwa Membe it's ok kwenda bado ana future ndani ya Chama. Nahisi soon Komredi Mangula ataomba kujiuzulu kupisha siasa za 'kihuni' ndani ya Chama.

dodge
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom