Kinana akerwa na Utitiri wa Traffic barabarani. Atoa maagizo mazito kwa Afande IGP Camilius Wambura

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Joined
Aug 24, 2011
Posts
53,868
Reaction score
121,001

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinanana amemshauri Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP), Camilius Wambura kufanya tathimini ili kuona uwezekano wa kupunguza idadi ya Askari wa usalama barabarani ambao wanalalamikiwa na Wananchi kusababisha kero.

Kinana ametoa ushauri huo jana akiwa katika mwendelezo wa ziara yake katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini ambapo Wananchi wa maeneo mbalimbali ya Mikoa ya Songwe na Mbeya wamelalamikia idadi kubwa ya Askari wa barabarani ambao wamekuwa wakiwasimamisha mara kwa mara, kutaka fedha ambazo hata hivyo hawatoi stakabadhi yoyote.

Malalamiko hayo ya Wananchi yaliendelea kuibuka hata katika kikao cha ndani cha Wanachama wa CCM Mkoa wa Songwe ambapo mmoja ya wanachama hao, dereva wa magari ya kubeba abiria, ametoa malalamiko mbele ya Kinana akidai wamechoka kusimamishwa mara kwa mara na Trafiki na kila wanaposimama wanatoa sh. 2,000 kwa kila kituo.

Akijibu malalamiko hayo Kinana amesema “Nampongeza Rais kwa kumtea IGP mpya, nina hakika ni IGP mwadilifu, mchapakazi na hodari lakini namuomba na kumshauri atazame wingi wa Trafiki mijini, kila baada ya muda mfupi unasimamishwa na Trafiku, wenye magari hawaendeshi kwa raha, hivyo nimsihi IGP afanye tathimini kuhusu uwepo wa Trafiki wengi kwenye miji yetu, wamekuwa wengi sana kila ukitembea kidogo unasimamishwa, kilomita moja unakuta Trafiki”
 
Kinana mnafiki sana anawezaje kukaa na Rais wakapanga kuuza Loliondo ashindwe kuongea naye jambo la trafiki?

Aache upumbavu na kiki za kisiasa azungumzie mfumko wa bei na nyongeza ya mishahara kwa watumishi anazidiwa na Vijana wadogo kina Pambalu na Mwaipaya wanadili na maisha ya watu.

Bei ya vifurushi, mafuta petroli Kagera 3, 800/ analeta storry za Abunwas wasio na akili wanashangilia.
 
CCM mara inasema Trafiki wapewe elfu tano ya kubrashia viatu mara wapunguzwe

Ila ngoja tuone maana Matrafiki wamekuwa kero ila sio wote kuna wengine wanajua wanafanya nini kama Trafiki wa Mkoa wa Tabora wakikupiga mkono ujue unakosa na wanaweza kukuonya na kukuambia usirudie.
 
Kama daktari mmoja wagonjwa 80, mwalimu mmoja wanafunzi 40, trafiki mmoja magari mangapi? tuanzie hapo kwanza.....
Yes tunaweza pata hesabu hapo ila kuna njia kuanzia pale kisongo Arusha mpaka Moshi ni balaa kila baada mita kadhaa hawa hapa binafsi napenda option ya usiku japo wanasaidia kupunguza mwendo kasi
 
KINANA AMSHAURI IGP KUFANYA
TATHMINI WINGI WA TRAFIKI BARABARANI
IMG-20220728-WA0191.jpg

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinanana amemshauri Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP), Camilius Wambura kufanya tathimini ili kuona uwezekano wa kupunguza idadi ya askari wa usalama barabarani ambao wanalalamikiwa na wananchi kusababisha kero.

Kinana ametoa ushauri huo jana akiwa katika mwendelezo wa ziara yake katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini ambapo wananchi wa maeneo mbalimbali ya mikoa ya Songwe na Mbeya wamelalamikia idadi kubwa ya askari wa barabarani ambao wamekuwa wakiwasimamisha mara kwa mara, kutaka fedha ambazo hata hivyo hawatoi stakabadhi yoyote.

Malalamiko hayo ya wananchi yaliendelea kuibuka hata katika kikao cha ndani cha wanachama wa CCM Mkoa wa Songwe ambapo mmoja ya wanachama hao, dereva wa magari ya kubeba abiria maarufu kama Costa, kutoa malalamiko mbele ya Kinana akidai wamechoka kusimamishwa mara kwa mara na trafiki na kila wanaposimama wanatoa sh. 2,000 kwa kila kituo.

Akijibu malalamiko hayo Kinana alisema kwanza anampongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kumteua IGP Wambura. “Nampongeza Rais kwa kumtea IGP mpya, nina hakika ni IGP mwadilifu, mchakazi na hodari.

“Lakini namuomba na kumshauri atazame wingi wa trafiki mijini, kila baada ya muda mfupi unasimamishwa na trafiki, wenye magari hawaendeshi kwa raha, hivyo nimsihi IGP afanye tathimini kuhusu uwepo wa trafiki wengi kwenye miji yetu, wamekuwa wengi sana kila ukitembea kidogo unasimamishwa, kilomita moja unakuta trafiki.

“Namuomba IGP afanye tathimini watu wapumue, watu biashara zao zinaharibika kwa sababu ya kuambiwa paki pembeni, tunaheshimu umuhimu wa usalama nchini, lakini tunakerwa na kuambiwa paki gari pembeni. Namuomba IGP, naheshimu na natambua uwezo wake mkubwa, lakini afanye tathimini je, kuna umuhimu wa kuwa na idadi kubwa ya trafiki barabarani?´alihoji Kinana.

Pamoja na hayo Kinana alisema katika ziara yake amepokea malalamiko mengi ya wananchi wakilalamikia idadi ya trafiki na katika kushughulikia malalamiko hayo, ametoa ushauri huo kwa IGP Wambura kuangalia uwezekano wa kufanya tathimini kuhusu uwepo wa idadi ya trafiki barabarani.

Akizungumzia ushauri huo wa Kinana, IGP Wambura alisema ni mzuri sana na ameupokea.

IGP Wambura alisema ushauri huo una afya kwa maendeleo na kwamba anakwenda kuufanyia kazi ndani ya taasisi yake.

== ==
 
Hawa jamaa wakiwa hawana shida ya kuwatumia Polisi, husema kila neno kuonesha kwamba Polisi ni tatizo kubwa sana kwa wananchi. Wakiwahitaji Polisi, huwaambia wananchi wasicheze na vyombo vya dola.

Wanajua sana sanaa ya kucheza na akili za watanzania.
 
KINANA AMSHAURI IGP KUFANYA
TATHMINI WINGI WA TRAFIKI BARABARANI
View attachment 2307358

Back
Top Bottom