Kinana akerwa na Utitiri wa Traffic barabarani. Atoa maagizo mazito kwa Afande IGP Camilius Wambura

Kinana akerwa na Utitiri wa Traffic barabarani. Atoa maagizo mazito kwa Afande IGP Camilius Wambura

Lakini ni kweli traffic wanaudhi sana, wanavizia Magari utadhnia tuko vitani. Usiombe ukakutana na wale tochi,kuna wale wanao vizia ukikaribia kibaha wako wengi kweli, mmoja najificha na Camera anapiga magari picha halafu anawatumia wenzake mbele pale karibu na maili moja wanadaka magari pale, jamaa wale wanapata pesa nyingi sana.

Maeneo ya kona bar napo wamejazana hasa siku ya jumamosi wanavia pale kwenye taa, Sinza moli baada ya mataa napo wamejazana pale wanavia na kukusanya pesa na sehemu nyingine ni mataa ya salendor pale jamaa wamejaa kikosi kazi kipo pale na taa za pale nadhani kuna ambazo haziko vizuri basi jamaa wanadaka sana pale. Sehemu yeyote ambayo imekaa kimtego mtego jamaa utawakuta wapo wanavizia.
 
Hao ndio chanzo kikuu na cha uhakika cha mapato kwa jeshi la Polisi
 
Wacheze na it tu..waweke camera ambazo zitakuwa zinapiga picha na kutuma taarfa kwa dereva na polisi.

#MaendeleoHayanaChama
Tutaongeza unemployment mitaani; familia nyingi zitaumia.
 
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinanana amemshauri Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP)...
Kulewa madaraka ya kisiasa; anatoa maagizo kwa IGP kama nani. Yeye siyo kiongozi wa kiserikali, na IGP siyo kiongozi wa CCM.
 
IGP azingatie ushauri
Chama ndicho kinasimamia Serikali

Kupuuza aweza jikuta katumbuliwa halafu Mama sehemu ingine akahutubia kuwa mtu anapewa ushauri na watu wazima au maelekezo wanapuuza!!
 
Mbeya To Vwawa ni 72kilometre, kuna vituo 13 vya trafiki
 
Naunga mkono hoja. Mama amefungua nchi mizigo ya nchi jirani inapita bandari yetu na mizigo inatakiwa iwahi kwa wenye nayo. Bandari inachelewa kutoa mizigo na kuipangua kwenda bandari kavu ICDs ili kupata nafasi ya ku off load mizigo mipya.

Moja ya sababu ya kijinga na ya kusikitisha ni utitiri wa Trafiki barabarani Tanzania nzima. Upo umuhimu wa kufunga digital speed torch na camera kuliko kujaza matrafiki njiani. Wageni wanatushangaa sana wanapoona kigenge cha trafiki hata 9 sehemu moja halafu ikitokea ajali mbele wakafanye assessment huwaoni wao wanasubiri kupiga mabao magari.

Hii ni karne ya 21 watu hawapendi kupotezewa muda bila sababu za msingi serikali inatakiwa ilielewe hili mapema na kulifanuia kazi. Imefika wakati myu akinunua gypsum board kkkoo labda anapeleka kerege basi atayarishe rushwa kama 6 za kusimamishwa njiani . Lazima tujali muda ili uchumi ujengeke.

Mizani pia nayo si lazima iwe mingi sana. Watnedaji wetu lazima wa think globally sio local. Nadhani police ina mahitaji amkubwa sana ya watendaji wangepunguzwa kama hapa mjini wakaimarishe doria mitaani huko panya road wanatesa watu.

Nchi za wenzetu unabeba mzigo godown mpaka site hakuna anayekubugudhi na watu wanafanya kazi usiku kucha hapa usiku utaona landcruiser imekukimbiza. This is very barbaric.
 
Jamani Mama anatafutwa na kutafutiwa angle kwa nguvu. Ila naamini Mama keshawajua mpango wa akina Kinana. Traffic wamesaidia sana kupunguza ajali leo hii eti watoke. Lengo ni kumchafua Mama
 
Vip, Meno ya tembo mzigo hautembei hakuna pa kupitisha au na yeye na v8 lake anasimamishwa?
Hayo Maneno ya kichokochoko yalioazishwa na Mchungaji Msigigwa Bungeni ,alipofikishwa Mahakamani na Kinana aliomba radhi.
 
Hivi kwa kawaida pointi moja ni trafiki wangapi?

Nilipita barabara moja nikakuta pointi moja ina trafiki watano, wengine wamekaa juu ya pikipiki
 
Ni kweli pia maana washkaji ni wengi sana barabarani mchana.
Usiku wakiwepo wengi ni vizuri zaidi kwa ajili ya ulinzi
 
Tuanze na Arusha
Ukitoka Morombo utawakuta Crdb, baada ya mita zusizo zidi mita 500 uta wakuta Field force, utawakuta Safina, utawakuta dispensari, utawakuta Mbauda kabla ya mataa, ukivuka mataa tuu wapo wengine, uta kutana nao Ngarenaro, baada mita 150 kabla ya mataa wapo, ukifika Kilombero hao, ukifika summit mita 100 toka kilombero hao.
Elewa hadi hapo huja tembea kilomita sita.. Hiyo ni Arusha
 
Wimbo wa meno ya tembo ulishachuja tafuteni mwingine,

Ila naona mzee kinana kaachia udemu kana fallyipupa
 
Kulewa madaraka ya kisiasa; anatoa maagizo kwa IGP kama nani. Yeye siyo kiongozi wa kiserikali, na IGP siyo kiongozi wa CCM.
Kama kweli IGP naye "ameupokea" huo "Ushauri" na atautekeleza, tatizo litakuwa kwa IGP na wala si kwa Kinana. Tusubiri tuone.
 
Traffic checks nchi za waastarabu ni random and far between . Kero la trafiki Tanzania ni mateso makubwa kwa wa miliki wa magari. Truth of matter traffic checks are extortion stops . Inasikitisha,inahuzunisha,inafedhehesha Serikali kufumbia macho uhununi wa trafiki. Hili "pandemic" limalizwe once and for all.
 
IGP alipo apishwa agizo la kwanza alilo pewa na Mh. Rais ni kubadili jeshi la polisi.

Sasa wiki ime kata bado hakuna badiliko alilo fanya. Huyu ni mtu alikuwa polisi hapa hapa Tanzania haja toka Kenya.

Lakini ukiuliza muda wote ana fanya nini ata kujibu ana jifamilia rise.

Kupata kiongozi wa maana kuongoza jeshi la polisi lazima atoke nje ya polisi maana tabia za polisi zina fanana.
 
Back
Top Bottom