Kinana akerwa na Utitiri wa Traffic barabarani. Atoa maagizo mazito kwa Afande IGP Camilius Wambura

Kinana akerwa na Utitiri wa Traffic barabarani. Atoa maagizo mazito kwa Afande IGP Camilius Wambura

20220728_221610.jpg

Picha: Abdulrahman Kinana

“Hii ni nchi pekee ambayo trafiki wamejazana humo kila mahali, kilometa 1 trafiki, kituo cha basi trafiki.

Namuomba Mkuu wa Jeshi la Polisi wafanye tathmini watu wapumue, wafanye shughuli zao.”

Hayo yamesemwa na Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Abdulrahman Kinana
 
kuanzia pale kisongo Arusha mpaka Moshi ni balaa
Mimi hiyo Barabara nimeapa sitopita mchana tena hadi naingizwa Kaburini.

Iko siku mbele ya Makuyuni nakutana nao wanasema Spare tyre yangu ni kipara wakati sio wanasema nitoe rushwa ya msimbazi au waniandikie fine ya elfu thelathini nilipandwa na ghadhabu sana.

Nikaendelea na safari yangu kufika kwa Saadala wakanipiga mkono ati Overspeeding ati kwenye 50kph nimeingia na 51 Msimbazi mwingine ukanitoka

Nikaenda mpaka Haidaru nikajipumzisha na kuwalaani huku Konyagi ikiteremka vizuri na Binti wa Kipare.
 
Ndo aina ya viongozi tunaowategemea waendeleze Africa, anyways anacheza na emotions ila logic ni bure kabisa
 
Nenda Arusha ufurahi. Kamji kadogo kila mtr kadhaa wapo. Unasimama hapa baada ya m500 mwelekeo ule ule mwingine anakusimamisha.
 
Traffic ni kero kuu barabarani, Mzee Kinana, Mungu akubariki sana kwa kulisemea vizuri sana hili, Traffic wanasaka hela utafikiri saccos, ni hatari sana, Mh. Rais wetu Samia alilisema hili nakumbuka ni mwaka jana, kuwa traffic ni kero sana, ila sasa Makamu Mwenyekiti wake kalisema tena, naamini, wananchi watapumua sasa. Traffic ni kero kuu hapa Tanzania.
 
Hapana. Barabara zetu bila matrafiki zitateketeza watu. Kama unaona unacheleweshwa safari na matrafiki, anza safari mapema. Usalama vs kero kipi bora? Bora usalama.
 
Mhe, Kinana asante sana, nawe afande IGP Wambura sikia kilio hiki cha Watanzania.

Matrafiki karibia wote hawako barabarani kiusalama wa laia na mali zao.

Bali ni usalama wa matumbo yao wenyewe!

Yaani mtu inafikia huna kosa lolote, lakini unaambiwa kwamba unatuachaje-achaje hapa! Kwao gari bovu siyo chukizo tena ila rasilimali yao kubwa.

Hali imezidi kuwa mbaya mpaka ma-RTO na Ma-DTO wameona kuwa ofisini hakulipi, nao wameingia mzigoni.
Hatukatai mtu kufanya maendeleo yake binafsi. Lakini siyo kushindana kununua magari na kujenga nyumba kwa pesa za kuwapora laia.

Waheshimiwa, nakubaliana kwamba wapunguzwe barabarani, lakini na watakaosalia wafuatiliwe, mbona huwa wanachukuwa pesa waziwazi mno? Kwani Takukuru ya nchi hii huwa kazi yao nini hasa. Mbona ni rahisi kuwakamata waovu hawa?

Hivi takukuru hata kutegesha camera kwenye vijiwe vyao nako kumewashinda?

Au ndiyo nanyi fungu linawafikia? Sasa kama ninyi hamfanyi hivyo nani huwa anawadhibiti watu hawa?

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinanana amemshauri Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP)...
 
Kuanzia singida hadi mwanza kuna trafiki wa tochi wengi sana barabarani ni kero kubwa sana wapunguzwe maana dar to mwanza safari ni ndefu wanapotezea abiria muda sana wakisimamisha bus mtakaa saa nzima wanadai rushwa kubwa kwa nguvu!!


Sasa niliona wakipiga mkono bus jamaa anakanyaga mafuta tukiwapita wanarushiwa buku ten ten hata mabasi hayasimami maana ni kero mno ukisimama tu mjadala masaa mawili na nusu saa maana wanakutajia pesa ndefu eti umekiuka spidi limit! Yaani ni rahisi mno kuwashika kwa rushwa!


Halafu it doesn't make sense bus linapita mbele linasimamishwa na kuoneshwa picha eti ulipopita igunga au kabuku ulikuwa na speed 280 wakati si kweli huu ni wizi na ufisadi na uonevu kwa raia mama Samia atusaidie serikali iondoe huu wizi wa mchana , wengi wanaonewa sana zinawekwa spidi za uongo ili ulipe faini au rushwa. Serikali hii ina vyanzo vingi vya kuibia raia maana huu utaratibu wa picha sijui za whatsapp my foot ni wa trafiki walioajiriwa na serikali na wizi wao wanafanya mchana kweupe!

Nikamate hapo hapo sio kunionesha picha ya whatsapp dakika 40 eti nilipita huko nyuma spidi 120 kwenye kona nshaaaa!!

Ulaya wizi huu wa serikali kwa raia kupitia tozo kubwa na tochi ya trafiki hakuna! Wao hukamua kodi tu kupitia mishahara na mauzo, anaepata mshahara mkubwa au mauzo makubwa ana kodi kubwa!Masikini wanalipa kodi kidogo sana na mwenye mshahara wa milioni moja kushuka chini halipi paye!

Serikali za nchi maskini zinaonea sana raia na kuwadidimiza kwenye lindi la umaskini kupitia mambo mengi!Wakiandamana kudai haki zao badala ya kupewa ulinzi wanapigwa mabomu na marungu kuonesha how primitive the african governments still are!
 
Polisi wakitaka hela waweke tochi digital tu, afu wakae ofisini. Watadaka gari nyingi mno kuliko kuviziana
 
Back
Top Bottom