Kinana akerwa na Utitiri wa Traffic barabarani. Atoa maagizo mazito kwa Afande IGP Camilius Wambura

Wata mjibu. Kama waliweza kumjibu Mh. Rais, sitoshangaa hata Kinana akajibiwa kwamba wao wana intelijensia. Asiwaingilia.
 
Sisiem kwa ngenga hawajambo maneno na matendo mbingu na ardhi.
 
Hili aliongea kinana yuko sahihi sana, ni aibu kwa nchi ya Tanzania kila mita 10 unakuta traffic tena wana uliza maswali yale yale ya kijinga, eti fire extinguisher, driving license, insurance, wanaangalia tairi, wengine wako na list ya makosa 48 wana tazama, wengine wana jificha porini na tochi, huu nu upuuzi sana.

Utadhani nchi yetu iko vitani, kila mita 10 traffic police, ni kero kubawa sana , wengine hadi wanaomba maji ya kunywa kinyume na maadili kazi zao, ilitakiwa kutoka Arusha hadi Dar walai usimame mara moja au hakuna, kuwe na one stop traffic checking ,na after checking watoe certificate/kibali kuwa tume kagua mazaga zaga yote baada ya hapo safari inaanza hadi ufikapo kusiwe na utitiri huu wa kijinga.
 
Mwenye mamlaka na yeye anaomba badala ya kutoa maagizo
 
Kama daktari mmoja wagonjwa 80, mwalimu mmoja wanafunzi 40, trafiki mmoja magari mangapi? tuanzie hapo kwanza.....
Magari yanaweza kuwa mengi pia,jiulize ni magari mangapi yenye makosa ya barabarani yanayofika vituoni?Je,wingi wa Traffic Police kumesaidia kwisha kwa ajali za barabarani zinazotokana na ubovu wa vyombo,miundo mbinu ya usafirishaji?Je,vyombo vingapi visivyofaa kuwa barabarani na bado vinatembea?Madereva wangapi wenye sifa stahiki wapo barabarani?
Je,hakuna technology inayoweza kufanya kazi wafanyazo askari hawa wanaopamba barabara zetu kwa suti zao nyeupe?
Ah,acha niishie hapo kwa sasa maana jamaa wapo pale kukusanya na bei elekezi zinafahamika,ila TAKUKURU na Watanganyika wametulia tuli.
 
Sio magari tu, Bodaboda pia.
Vituo vidogo vimejaza pikiki balaa
 
Tatizo la dot.com tunalaamu tu bila ya Kuja na mbadala, sasa wewe una comment hapa hii sio suluhu!,sasa tell us how to remedy this
Suluhu zilishatolewa, na wanazijua. Waliambiwa wa'digitize' mifumo yote inayohusu usalama barabarani na matukio yote yawe recorded na kuwa reported in real time! Badala yake wamedigitize tozo peke yake. Digitization inatakiwa iende kwenye maeneo yote.

Na tungeweza kufanikiwa hili kama tungekuwa na nishati ya uhakika kwa kukamilika Bwawa la umeme la Mwalimu Nyerere huko Rufiji! Lakini, wale wanao lipinga Bwawa hilo wanatushauri tutumie nishati ya haja kubwa zetu (rejea hotuba ya Balozi wa Uholanzi nchini Wieb De Boer aliponukuliwa na ITV- tazama kuanzia dakika 7 sekunde 42) kuwa na nishati!

Sina hakika kama tuna elewana hapa!
 
Tatizo kubwa hao Traffic wamewekwa kuwa chanzo cha mapato serikalini na kwao wenyewe.
Hawa wamewekwa kuwa chanzo cha mapato kwa wanaowapangia vitengo.

Mitaani tunalazimishwa ulinzi shirikishi wakati watu tunaowalipa kutulinda kwa kodi zetu wamegeuka majambazi wakutupora, tena kwa kutumia rasilimali zinazogharamiwa na kodi zetu.

Kuna hawa askari polisi wanaotumia pikipiki. Wao ni kufukuzana na watu mchana mitaani kupora mali za watu. Tukio la uhalifu litokeapo usiku hakuna askari wa kusaidia.

Jeshi la polisi linahitaji major overhaul.
 
Anakereka mzigo wake unapekuliwa sana unapopita
 
Biashara zake za meno ya tembo zinacheleweshwa na Trafiki kufika sokoni
 
Waje na mbadla wake. Tuwe na camera , watu wakutane na bill zao mwisho wa mwezi.
 
Kinana anabanwa kusafirisha dili zake ?
Akae kwa kutulia, nchi inahitaji ulinzi hii.
 
Barabara nzuri za lami lakini usafiri hauna tija. Traffic wanatumia gari binafsi Bagamoyo - Msata kumulika magari toka kichakan. Je chaoi na cha serikali kipi kikubwa. Tume ya Kipolisi ilifanyie kazi. Tanrods wanaweka 50km limit kila pahala. Kivuli?. Haina raha tena kwenda mikoani kwa gari binafsi. Bora nitumie mabasi.

 
Trafic wanadai hela toka kwa madereva kwa nguvu hasa Dar.
 
Kinana anasahau kuwa traffic ni chanzo kipya na cha kuaminika cha mapato ya serikali?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…