Kinana asome alama za Nyakati, wana CCM hawamwelewi

Kinana asome alama za Nyakati, wana CCM hawamwelewi

Hao njaa tu wakikosa buku tano lazima wafure....yani ukiitwa kwenye mikutano yao kengele ya kwanza kichwani leo nabadilisha Mboga

Chadema ndo imebaki na wafuasi wa KWELI yaani chama imo ndani ya moyo mpaka kwenye Damu....

Na nauli zimekayibong sasa ule wimbo wa fronti kwa fronti mtamujeee ....unaenda kula Mwaka mpyaa kwenu na maumivu bado maloope inawasubiri ...
Ccm hamna kitu chadema ndio kabsaaa. Kwa ufupi nchi hii haina vyana
 
Utasikia Mtu Anatemeshwa Bungo Mdomoni, Mambo Yameanza Pole Pole
 
Kinana ni mwana CCM kiongozi wa genge chafu ndani ya CCM.
Kinana ni mwizi na mbadhirifu kama wengine tuiowafahamu mfano wa Makamba Jr.
Vema Kinana akajitambua na kufunga Domo lake kabla hayajamkuta ya kumkuta.

Hii sio awamu ya ujinga!
Nani sio mwizi na msafi huko ccm? Dhalimu mwenyewe alikuwa anajifanya msaf, lakini uchafu aliofanya kwenye plea bargaining hausemeki.
 
Tatizo ni usukuma ndio unao waletea shida, utaratibu ulio tumika na magufuli na ulianza kutumika na makonda sio uongozi bora bali ni udhalilishaji wa watumishi viongozi.

Huwezi kumuita mkuu wa mkoa "njoo hapa kimbia" hiyo sio heshima kwa sababu yeye ni kiongozi ana watu wanasubiri maelekezo yake huwezi kumuita kama mtoto wako ni udhalilisha ule ila wajinga wajinga ndio walikuwa wanapenda kutokana na kukosa kwao elimu na kupenda kwao majungu
Sasa huyo mkuu wa mkoa ni nani? Waafrica na upumbavu ni pete na kidole!
Ukuu wa mkoa ni ujinga gani? wanasaidia nini uwepo wao? Jinga kabisa!
 
KINANA:VIONGOZI SERIKALINI FUATENI NYAYO ZA RAIS SAMIA KUESHIMU SHERIA, KANUNI MNAPOCHUKUA HATUA DHIDI YA WATENDAJI

Na Mwandishi Wetu

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Abdulrahman Kinana ametaka viongozi na watenaji serikalini kuzingatia kanuni, sheria, utaratibu na Katiba wanapowakosoa watendaji.

Amesema ni vyema wakajifunza kwa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan ambaye pamoja na kuwa na uwezo na mamaka lakini hajawahi kusimama hadharani na kuvunja haki ya utu wa mtu hususan watendaji katika ngazi mbalimbali.

Kinana aliyasema hayo jana Ushirombo, Wilaya ya Bukombe mkoani Geita alipokuwa akizungumza na wanachama wa CCM, viongozi na wananchi alipofungua jengo la ofisi za CCM la wlaya hiyo.

“Nataka kufafanua hili ambalo nimezungumza katika Mkutano Mkuu hapa Bukombe, ni kwamba viongozi wasimamie watendaji serikalini, wasimamie sheria, kanuni na utaratibu lakini si vizuri kuwasema hadharani na kuwafedhehesha watendaji wa serikali.

“Mfano mzuri wa kuigwa ni wa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwani hatujawahi kuona akisimama hadharani akmfedhehesha mtendaji serikalini, kwa sababu yeye ni muumini wa utawala bora, unaozingatia katiba, sheria, kanuni na taratibu,” alisema.

Kinana alsisitiza watendaji wote wa serikali wanasimamiwa na kanuni, sheria, katiba na utendaji serikalini.

View attachment 2841961View attachment 2841962
mie nadhani muandishi ndio haelewi na sio wanaCCM
 
Jitu kama Sabaya au Makonda, shule hayajasoma yalikuea yanashinda makorongoni, ndio anamvaa injinia na kumpiga mkwara
 
Hivi kijana huyu sahihi amesahau alipokuwa anawaita mawaziri ni mizigo hadharani acha unafiki rudi kwenu Kismayo
 
Huo ndio ukweli!

Kwenye utendaji kuna kitu kinaitwa Proffessionalism.

Kisiasa unaweza ukadhani mtendaji ana makosa...lakini kumbe siyo!

Na Watendaji huchapwa na Kalamu na siyo kwenye podium!

Uko mtindo wa Mwanasiasa ili kuonekana anatenda vema ni Lazima amuumbue mtendaji...of course kwenye macho ya wapiga kura ni credit lakini kuanzia tu hapo morale ya Mtumishi ktk utendaji inakufa papo hapo!

Unakuwa na waigizaji tu kwenye maeneo ya kazi badala ya Watendaji..!

Makamu alikuwa very right!

By the way huyu mzee akiongea kitu usipoelewa basi tena!
Umeandika ujinga tupu.
 
Msemaji anamambo ya kipuuzi sana ndio maana kila kitu kikawekewa utaratibu na kanuni ukutaka kufuata mihemko ya hawa raia ambao wengi wao ni wapenda majungu na chuki dhidi ya watumishi wa umma utaonea sana watumishi ambao hawana cha kukufanya ukiwa kwenye jukwaa.

Sio ustaarabu naheshima ya kiuongozi kupigia kelele watendaji kwenye majukwaa ya kisiasa, huo sio utaratibu, hata mke wako nyumban kuna mambo huwezi muuliza mbele ya watoto hata kama kakosea mbele yao
Upuuzi na ujinga mtupu.
 
Kinana ni kiongozi wa makundi ya kihuni ndani ya CCM, watu wamemchoka ndiyo maana hawamuelewi.
 
Back
Top Bottom