Kinana: CCM imevunja rekodi ukusanyaji wa maoni juu ya Rasimu ya Katiba Mpya

nngu007

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2010
Posts
15,860
Reaction score
5,801

[video=youtube_share;G6_PyJm4IIE]http://youtu.be/G6_PyJm4IIE[/video]​
 
Maoni yake yalikusanywa kwenye mechi kati ya Simba na Kiomboi shooting...
 
CCM iache Siasa za Kishamba.Maoni yanatakiwa yawe wazi kwa Kila Mtu.Sijaona tangazo lolote linalowaalika watu kwenda kutoa Maoni kwenye Mabaraza au Vikao vya CCM,Sasa hiyo Rekodi imevunjiwa wapi?Ni vigezo gani viliwekwa ili tuamini kwamba kweli Rekodi imevunjwa?.
 
haya majitu ni matapeli aisee,hayo maoni yamekusanywa wapi? mbona sikuwahi kuona mkutano wa ccm wa kukusanya maoni hayo?
 
CCM iache Siasa za Kishamba.Maoni yanatakiwa yawe wazi kwa Kila Mtu.Sijaona tangazo lolote linalowaalika watu kwenda kutoa Maoni kwenye Mabaraza au Vikao vya CCM,Sasa hiyo Rekodi imevunjiwa wapi?Ni vigezo gani viliwekwa ili tuamini kwamba kweli Rekodi imevunjwa?.
Mkuu angalia usemi wako kwa sababu katika usemi huu wewe ndiyo unaonekana 'mshamba'.

Maoni ya wananchi wote yalikusanywa na Tume ya Jaji Warioba kupitia Mabaraza ya Katiba ambayo yaliundwa, kusimamiwa na kuendeshwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba mojawapo ya mabaraza hayo ni mabaraza ya kata, wilaya n.k. ambayo yalilalamikiwa na CHADEMA kuwa yamejaa wanaCCM pekee badala ya wananchi wote.

Mabaraza ya CCM ni mabaraza ya taasisi ambayo yanaundwa na taasisi yenyewe. Haya ni sehemu ya pili ya aina ya mabaraza kama yalivyoainishwa katika Sheria ya Mabadiliko ya Katiba Sura ya 83. Haya ni pamoja na Asasi na makundi ya watu wenye mwelekeo na malengo yanayofanana hii ina maana kwamba hata walevi au wafungwa wanaweza wakaanzisha baraza lao la katiba kama tume ya Jaji Warioba itaona umuhimu wa kuwepo.

CCM kama Taasisi iliyoundwa na wanachama na pia kuwepo kwake kisheria kunategemea wanachama ndiyo maana imekusanya maoni ya wanachama wake kama Taasisi.

Hii ndiyo inapelekea kuwepo kwa hoja ya Jaji Warioba aliposema kuwa hawatachukua maoni ya "jukwaani wala ya kwenye helikopta" kwa cover la Taasisi pamoja na kwamba kauli yake hiyo ni debatable.
 
mkuu bado hoja inabaki ileile, ni lini na wapi ccm walikusanya maoni kama taasisi? Unazungukazunguka lakini ni bra bra tu...
 
Ccm kwa ujanja ujanja ndo wenyewe, wanachama wa ccm wanashangaa lini wameitwa kutoa maoni yanayohusu katiba kama taasisi ndani ya chama chao? Huu ubabaishaji wa maccm siku moja utaligarimu taifa letu!
 
Mkuu angalia usemi wako kwa sababu katika usemi huu wewe ndiyo unaonekana 'mshamba'.

Maoni ya wananchi wote yalikusanywa na Tume ya Jaji Warioba kupitia Mabaraza ya Katiba ambayo yaliundwa, kusimamiwa na kuendeshwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba mojawapo ya mabaraza hayo ni mabaraza ya kata, wilaya n.k. ambayo yalilalamikiwa na CHADEMA kuwa yamejaa wanaCCM pekee badala ya wananchi wote.

Mabaraza ya CCM ni mabaraza ya taasisi ambayo yanaundwa na taasisi yenyewe. Haya ni sehemu ya pili ya aina ya mabaraza kama yalivyoainishwa katika Sheria ya Mabadiliko ya Katiba Sura ya 83. Haya ni pamoja na Asasi na makundi ya watu wenye mwelekeo na malengo yanayofanana hii ina maana kwamba hata walevi au wafungwa wanaweza wakaanzisha baraza lao la katiba kama tume ya Jaji Warioba itaona umuhimu wa kuwepo.

CCM kama Taasisi iliyoundwa na wanachama na pia kuwepo kwake kisheria kunategemea wanachama ndiyo maana imekusanya maoni ya wanachama wake kama Taasisi.

Hii ndiyo inapelekea kuwepo kwa hoja ya Jaji Warioba aliposema kuwa hawatachukua maoni ya "jukwaani wala ya kwenye helikopta" kwa cover la Taasisi pamoja na kwamba kauli yake hiyo ni debatable.

Nawe acha kupotosha watu humu......,mabaraza yaliyoundwa hayana uhusiano na vyama vya siasa japo wajumbe walipitishwa na wajumbe ambao ni wenyeviti wa mitaa/vijiji ambao wengi wao walitokana na ccm. Hii tu haimaanishi kuwa ccm wamekusanya maoni kupitia wajumbe hawa..... ccm kama taasisi yenye mawazo na maoni yanayofanana ilitakiwa ionyeshe jinsi ilivyokusanya maoni ya watu milioni mbili nukta tatu kama inavyojinadi hivi sasa. Kusema wamekusanya maoni ya watu wengi na kuvunja rekodi bila statistic ni ubatili mtupu...
 
CCM iache Siasa za Kishamba.Maoni yanatakiwa yawe wazi kwa Kila Mtu.Sijaona tangazo lolote linalowaalika watu kwenda kutoa Maoni kwenye Mabaraza au Vikao vya CCM,Sasa hiyo Rekodi imevunjiwa wapi?Ni vigezo gani viliwekwa ili tuamini kwamba kweli Rekodi imevunjwa?.

Mkuu nadhani mambo ya ndani ya CCM katibu mkuu wake ndiye anaweza kueleza vizuri zaidi kuliko mtu mwingine. Lakini ikumbukwe kuwa mabaraza ya katiba ya wanaccm ni sehemu tu ya mchakato mzima wa maoni kuhusu katiba. Ni vizuri tukikumbuka kuwa CCM ina wanachama, kwa hiyo akiangalia idadi ya wanachama wake na turn out, inawezekana kabisa kuwa Kinana yuko sahihi.
 
Nawe acha kupotosha watu humu......,mabaraza yaliyoundwa hayana uhusiano na vyama vya siasa japo wajumbe walipitishwa na wajumbe ambao ni wenyeviti wa mitaa/vijiji ambao wengi wao walitokana na ccm. Hii tu haimaanishi kuwa ccm wamekusanya maoni kupitia wajumbe hawa.....
Badala ya kusema mimi ninapotosha, ingekuwa vizuri ukaelewa kilichoko kwenye bandiko langu.

Wapi nimesema maoni ya CCM yamekusanywa kutoka kwenye Mabaraza ya Katiba ambayo yaliundwa, kusimamiwa na kuendeshwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba. Legally, Mabaraza yanayosimamiwa na kuendeshwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba niya wananchi wote yanayotokana na wajumbe waliochaguliwa na wananchi wote kupitia mitaa, kata, wilaya n.k
ccm kama taasisi yenye mawazo na maoni yanayofanana ilitakiwa ionyeshe jinsi ilivyokusanya maoni ya watu milioni mbili nukta tatu kama inavyojinadi hivi sasa. Kusema wamekusanya maoni ya watu wengi na kuvunja rekodi bila statistic ni ubatili mtupu...
Sasa wewe unataka CCM ionyeshe jinsi ilivyokusanya maoni ya wanachama wake wapi?. Hapa JF?.

Kwanza ukiangalia hata hiyo video haionyeshi hotuba nzima ya Katibu Mkuu wa CCM kwa maana kuwa hatufahamu baada ya kutoa hayo maelezo aliendelea kusema nini zaidi, lakini kikubwa zaidi anayetakiwa kujua njia ambazo CCM walitumia kupata mapendekezo yao ni Tume ya Jaji Warioba kupitia vidhibiti ambavyo Tume ya Jaji Warioba inazitaka taasisi mbali mbali kukamilisha.
 
Badala ya kusema mimi ninapotosha, ingekuwa vizuri ukaelewa kilichoko kwenye bandiko langu.

Wapi nimesema maoni ya CCM yamekusanywa kutoka kwenye Mabaraza ya Katiba ambayo yaliundwa, kusimamiwa na kuendeshwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba. Legally, Mabaraza yanayosimamiwa na kuendeshwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba niya wananchi wote yanayotokana na wajumbe waliochaguliwa na wananchi wote kupitia mitaa, kata, wilaya n.k

Sasa wewe unataka CCM ionyeshe jinsi ilivyokusanya maoni ya wanachama wake wapi?. Hapa JF?.

Kwanza ukiangalia hata hiyo video haionyeshi hotuba nzima ya Katibu Mkuu wa CCM kwa maana kuwa hatufahamu baada ya kutoa hayo maelezo aliendelea kusema nini zaidi, lakini kikubwa zaidi anayetakiwa kujua njia ambazo CCM walitumia kupata mapendekezo yao ni Tume ya Jaji Warioba kupitia vidhibiti ambavyo Tume ya Jaji Warioba inazitaka taasisi mbali mbali kukamilisha.

mkuu acha kutetea undefendable acts.
huwezi kukusanya maoni ya wanachama 2.6m bila watu kujua kama unavyoona wengi wanashangaa ambao ni wafuatiliaji wazuri wa siasa kama mimi na wewe kwahiyo CCM has cooked the books na sababu ni moja tu ya kufanya haya wanajaribu kuwa preemptive chadema ili waonekane wana support kubwa.ukisikia watu wanasema cdm inaendesha ccm huo ndio ushahidi make the numbers scream higher than necessary to shut down your opponent.
 
Misahafu ilitufundisha kuwa Bwongo ni......ambayo kwa kweli ni ccm
 
Ukizoea kuchakachua mambo huwezi kuacha kirahisi tabia hiyo.
Ni lini na wapi CCM tuliwafuata wanachama wetu nchi nzima ili kuchukua maoni yao?

Ninachokumbuka CCM tulikuwa na vikao vya ndani kwa mikoa michache(Darasa la kukaririsha 'mistari' ya kwenda kusema kwenye tume ya Warioba) ambapo wajumbe walikuwa ni makada wetu ambao watakwenda kwenye mabaraza ya kata kwenda kupeleka maoni tuliyowakaririsha kwanza.
Lengo la vikao hivyo lilikuwa ni kuwafunda(kuwakaririsha) makada wetu waandamizi.
Wakufunzi walikuwa viongozi wa juu wa CCM.
 
Badala ya kusema mimi ninapotosha, ingekuwa vizuri ukaelewa kilichoko kwenye bandiko langu.

Wapi nimesema maoni ya CCM yamekusanywa kutoka kwenye Mabaraza ya Katiba ambayo yaliundwa, kusimamiwa na kuendeshwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba. Legally, Mabaraza yanayosimamiwa na kuendeshwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba niya wananchi wote yanayotokana na wajumbe waliochaguliwa na wananchi wote kupitia mitaa, kata, wilaya n.k

Sasa wewe unataka CCM ionyeshe jinsi ilivyokusanya maoni ya wanachama wake wapi?. Hapa JF?.

Kwanza ukiangalia hata hiyo video haionyeshi hotuba nzima ya Katibu Mkuu wa CCM kwa maana kuwa hatufahamu baada ya kutoa hayo maelezo aliendelea kusema nini zaidi, lakini kikubwa zaidi anayetakiwa kujua njia ambazo CCM walitumia kupata mapendekezo yao ni Tume ya Jaji Warioba kupitia vidhibiti ambavyo Tume ya Jaji Warioba inazitaka taasisi mbali mbali kukamilisha.
mkuu bado unazunguka, je wapi na lini ccm ilikusanya haya maoni ya watu milioni mbili na ushei? Je maoni ya watu ni siri? Mbona tume ya warioba ilichukua maoni kwa wananchi mchana kweupe? Kuna nini huu usiri wa ccm katika mambo ya umma? . In short mkuu ukweli ccm wamepika data, wanachama wao wengi mikoani wanalalamika kwa ccm kutowapa nafasi kutoa maoni kama inavyofanya Chadema!
 
mkuu bado hoja inabaki ileile, ni lini na wapi ccm walikusanya maoni kama taasisi? Unazungukazunguka lakini ni bra bra tu...
CCM wao walichagua njia ya kukusanya maoni siyo kwenye mikutano ya nje bali mikutano ya ndani kwa maana hiyo kwa kiasi kikubwa ni wanachama wa CCM pekee waliohudhuria hiyo mikutano ndiyo wanaofahamu vizuri process yao ya ukusanyaji wa maoni.

Kuna thread ililetwa hapa JF ya tamko la Nape kuhusu utaratibu wao katika ukusanyaji wa maoni kupitia wanachama wao kama taasisi.
 
nahisi kinana atakuwa amekusanya maoni ya wanaccm akiwa ndotoni
 
CCM wao walichagua njia ya kukusanya maoni siyo kwenye mikutano ya nje bali mikutano ya ndani kwa maana hiyo kwa kiasi kikubwa ni wanachama wa CCM pekee waliohudhuria hiyo mikutano ndiyo wanaofahamu vizuri process yao ya ukusanyaji wa maoni.

Kuna thread ililetwa hapa JF ya tamko la Nape kuhusu utaratibu wao katika ukusanyaji wa maoni kupitia wanachama wao kama taasisi.

mjomba umeshaambiwa vikao hivyo vya ndani unavyodai viliwahusu wana ccm wachache sana na vilikuwa siyo vya kutoa maoni kama unayodai bali vya kuwakaririsha mistari ya kwenda kusema mbele ya tume na wengine wakashindwa hata kusema wakafikia kusoma mbele ya wajumbe wa tume na wengine kuishia kutimuliwa. ccm haijawahi kuita wanachama watoe maoni yao
 
mkuu bado unazunguka, je wapi na lini ccm ilikusanya haya maoni ya watu milioni mbili na ushei? Je maoni ya watu ni siri? Mbona tume ya warioba ilichukua maoni kwa wananchi mchana kweupe? Kuna nini huu usiri wa ccm katika mambo ya umma? . In short mkuu ukweli ccm wamepika data, wanachama wao wengi mikoani wanalalamika kwa ccm kutowapa nafasi kutoa maoni kama inavyofanya Chadema!
Mkuu. Jaribu basi hata kutumia LOGIC kidogo.

Kumbuka CCM huwa inadai mbele ya umma kuwa ina wanachama milioni 5+, kwa maana hiyo hawawezi wakaja na data za kupika zenye idadi ya wanachama milioni 2,618,753 pekee ambazo ukiziangalia zinatoa picha mbaya kwa uhai wa chama kinachojinasibu kama kina wanawanachama milioni 5+.

Anyway, tukubali kutokubaliana kwa sababu wanaofahamu ukweli halisia ni CCM na wanachama wake.
 
Back
Top Bottom