Kinana: CCM imevunja rekodi ukusanyaji wa maoni juu ya Rasimu ya Katiba Mpya

Kinana: CCM imevunja rekodi ukusanyaji wa maoni juu ya Rasimu ya Katiba Mpya

Ndivyo ambavyo CCM hupiga bao kirahisi bila wapinzani kujua, Kwani kabla hata chopa kuanza kuruka CCM Ilikuwa na vikao vyake vya mabaraza ya kata na nililishuhudia kule visiwani, Mabaraza ya Kata ya CCM yameanza kabla ya mabaraza ya Tume ndiyo maana wengi walioyasikia walidhani ni yaliyoundwa na Tume

Unashindwa hata kuongopa?
Yani mabaraza ya CCM ya Kujadili Rasimu ya Katiba yamechukuliwa kabla hata Tume haijachukua Maoni ya Kuandika Rasimu yenyewe?
Au MACCM walikuwa nayo hii Rasimu kabla hata ya Mchakato wa Tume kuanza.

Au nikuulize swali unajua Tofauti ya Maoni ya Kutunga Rasimu ya Katiba Na Maoni ya Kujadili Rasimu ya Katiba ?
 
Akili za pembe za ndovu bana!! Anaropoka tu!
 
mkuu, yaani hapo ndipo ccm inadhihirisha kuwa ni chama makini na kongwe. pia kina mfumo na viongozi thabiti toka mabalozi wa nyumba kumi hadi mwenyekiti Taifa. ccm wanajua sheria inasemaje na ndo maana walijipanga mapema

Umeingia Mkenge na wote mnaonekana ni watupu.

MACCM yatakusanya vipi Maoni ya Rasimu wakati hata Tume Yenyewe haija Tunga Rasimu yenyewe?

Tuache uongo.
 
Kuna watu kazi yao ni kupinga tu.

Hata hawajui vikao vya CCM ni vipi lakini wanapinga. Wanadhani CCM inafanya show off politics za kuruka angani na kuvaa migwanda.

Kama hamjui, CCM ina watu kila kijiji, mtaa kila sehemu nchini. CCM haihitaji kumpa posho Katibu Mkuu wake azunguke nchi nzima ili kujua wanachama wake wana maoni gani. Vikao vya CCM vya matawi vinatosha. CCM has that infrastructure, vyama vya magumashi havina infrastructure ndio maana watu kumi wanahangaika kuzunguka nchi nzima.
 
Unashindwa hata kuongopa?
Yani mabaraza ya CCM ya Kujadili Rasimu ya Katiba yamechukuliwa kabla hata Tume haijachukua Maoni ya Kuandika Rasimu yenyewe?
Au MACCM walikuwa nayo hii Rasimu kabla hata ya Mchakato wa Tume kuanza.

Au nikuulize swali unajua Tofauti ya Maoni ya Kutunga Rasimu ya Katiba Na Maoni ya Kujadili Rasimu ya Katiba ?

Kama hujaelewa vema kuuliza, mabaraza ya katiba yameanza kufanya kazi baada ya rasimu kutolewa na tume, na ndio muongozo wa tume, wengi wenu mnashinda kwenye mitandao hamfuatilii mambo kwenye field yanawapita. Kama ulikuwa unasikia maoni mengi ya Wazanzibari kupinga serikali tatu wanataka utaratibu wa serikali mbili uendelee yalikuwa na maoni ndani ya mabaraza ya katiba ccm.
 
hizo kejeli zenu zinadhihirisha namna gani mlivyo watupu kwenye jambo hili. by the way, kama nyie si members wa ccm, iweje mjue kuwa haijakusanya maoni ya taasisi?

Kumbe mjadala wa katiba ni siri kubwa kiasi kwamba ni kwa faida ya ccm tu? kwamba hatatetesi wengine wasizipate wala kusikia?
 
Mkuu nadhani mambo ya ndani ya CCM katibu mkuu wake ndiye anaweza kueleza vizuri zaidi kuliko mtu mwingine. Lakini ikumbukwe kuwa mabaraza ya katiba ya wanaccm ni sehemu tu ya mchakato mzima wa maoni kuhusu katiba. Ni vizuri tukikumbuka kuwa CCM ina wanachama, kwa hiyo akiangalia idadi ya wanachama wake na turn out, inawezekana kabisa kuwa Kinana yuko sahihi.

Vilaza wako wengi sana,mabaraza ya katiba ya ccm ni yapi? Au haya yaliyoundwa na watu kulipwa posho na serikali ndio ya ccm?

Na haiingii akilini watu wazima wanapiga makofi baada ya kuambiwa utumbo kwamba ccm ndiyo imeshinda kukusanya maoni kwa kukusanya kwa watu milioni mbili,kwa akili za kawaida tu watanzania wako mil 45 unasema umevunja rekodi kwa kupata maoni mil 2 ni akili ambazo hata kuku anakuzidi hawa 43mil wametoa maoni wapi? Halafu watu wazima na akili zao wanapiga makofi,

Hivi kulikuwa na kushindana kukusanya maoni? Au kwa kuwa wameona na Chadema wanakusanya ndio imekuwa taabu? Ccm kwa yale mabaraza ndio maana watu walilalamika kwamba ccm inaingilia mchakato kwa kutaka kuchagua viongozi wao ili wakaandike mambo ambayo ccm wanataka ili waendelee kubaki madarakani hata ka a hawatakiwi mbona wanajiaibisha kwa kufanya mambo ya ajabu?
 
[video=youtube_share;G6_PyJm4IIE]http://youtu.be/G6_PyJm4IIE[/video]​

Viongozi wa hovyo, huendesha chama hovyo hovyo na hivyo kuwa na taarifa za hovyo. iwe ni serikalini au kwenye Chama chao, imekuwa ni utaratibu wa kawaida kwa huyo M/Kiti wa hicho Chama kudangavywa? Maana kwa kiongozi makini, ange hoji CCM kama taasisi ni wapi wame fanya hiyo mokutano ya Mabaraza ya Katiba zaidi ya makao makuu ya CCM kuwapelekea nakala/ machapisho ya kukariri hao wanao waita wanachama!!?

Leo hii wanakuja na taarifa zisizo na uhalisia wa kile wanacho danganyana kwenye hilo ghala lao la kutolea taarifa za uongo hapo Dodoma. Kwa jinsi hali ilivyo kuwa ngumu Kisiasa kwa CCM, wanaogopa hata kuitisha mkutano kama sio kusimama kwenye majukwaa ya wazi kuongea na hao wanao waita wanachama wao 5 Mil.

Pamoja na hayo, hivi mnataka kuniaminisha kwamba kwenye Katiba ya JMT, kitu kinachoitwa "WANANCHI" ina maana hawajulikani kwamba ni Taasisi?
 
Kuna watu kazi yao ni kupinga tu.

Hata hawajui vikao vya CCM ni vipi lakini wanapinga. Wanadhani CCM inafanya show off politics za kuruka angani na kuvaa migwanda.

Kama hamjui, CCM ina watu kila kijiji, mtaa kila sehemu nchini. CCM haihitaji kumpa posho Katibu Mkuu wake azunguke nchi nzima ili kujua wanachama wake wana maoni gani. Vikao vya CCM vya matawi vinatosha. CCM has that infrastructure, vyama vya magumashi havina infrastructure ndio maana watu kumi wanahangaika kuzunguka nchi nzima.

Acha kututania mkuu.

Huko mitaani na vijijini wanaishi wanaccm pekeyao? Si wote tunaishi changanyikeni na kushare information.....
 
Acha kututania mkuu.

Huko mitaani na vijijini wanaishi wanaccm pekeyao? Si wote tunaishi changanyikeni na kushare information.....

Umeshawahi kuhudhuria kikao cha CCM?

Umeshawahi kujua kuwa CCM wanafanya kikao cha tawi?
 
Kuna watu kazi yao ni kupinga tu.

Hata hawajui vikao vya CCM ni vipi lakini wanapinga. Wanadhani CCM inafanya show off politics za kuruka angani na kuvaa migwanda.

Kama hamjui, CCM ina watu kila kijiji, mtaa kila sehemu nchini. CCM haihitaji kumpa posho Katibu Mkuu wake azunguke nchi nzima ili kujua wanachama wake wana maoni gani. Vikao vya CCM vya matawi vinatosha. CCM has that infrastructure, vyama vya magumashi havina infrastructure ndio maana watu kumi wanahangaika kuzunguka nchi nzima.

Acha Porojo we kilaza,mkutano wa ccm nani anahudhuria kwa hiyari yake mwenyewe? Msipowaaoomba watu kwa magari,kutangaza posho kwanza na kuweka wasanii wenu wauza unga wale ndio mpate watu

Hivyo vikao mnaviitisha usiku au muda gani ambao watu hawaoni? Kuweni na aibu kudanganyana kwa kujifariji halafu mnapiga makofi,yaani hakuna tofauti na majuha yooote poleni sana
 
Umeshawahi kuhudhuria kikao cha CCM?

Umeshawahi kujua kuwa CCM wanafanya kikao cha tawi?

Hapa mtaani kwangu balozi wa ccm hajawahi kunitaarifu uwepo wa kikao hicho, isitoshe balozi wa ccm wa mtaa wa pili

nilikuwa naye jana kama saa nne usiku anashangaa tu hajuwi habari za kinana na takwimu zake. Nadhani ni Mtaani kwenu

tu ndo mlifanya mabalaza ya katiba ya kiccm, sisi kwetu hatujayaona wala kuyasikia.
 
Sasa Nape Nnauye huwa analilia nini hasa??

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Umeshawahi kuhudhuria kikao cha CCM?

Umeshawahi kujua kuwa CCM wanafanya kikao cha tawi?

Pamoja na kushindwa kuyaona wala kualifiwa uwepo wa mabalaza ya ccm yahusuyo katiba, lakini Ijumaa jioni

Chadema chini ya Mbowe na Lisu walifika katika hapa mjini kufanya mjadala
, hakika watu wengi wahudhulia na

walifarijika sana kuwepo cdm na kufanikisha mjadala kwa uwazi na uhakika kwa faida ya watanzania wote na vizazi

vya hapo baadaye.
 
Hapa mtaani kwangu balozi wa ccm hajawahi kunitaarifu uwepo wa kikao hicho, isitoshe balozi wa ccm wa mtaa wa pili

nilikuwa naye jana kama saa nne usiku anashangaa tu hajuwi habari za kinana na takwimu zake. Nadhani ni Mtaani kwenu

tu ndo mlifanya mabalaza ya katiba ya kiccm, sisi kwetu hatujayaona wala kuyasikia.
Labda waseme waliitana wachache hapo Lumumba.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Hapa mtaani kwangu balozi wa ccm hajawahi kunitaarifu uwepo wa kikao hicho, isitoshe balozi wa ccm wa mtaa wa pili

nilikuwa naye jana kama saa nne usiku anashangaa tu hajuwi habari za kinana na takwimu zake. Nadhani ni Mtaani kwenu

tu ndo mlifanya mabalaza ya katiba ya kiccm, sisi kwetu hatujayaona wala kuyasikia.

Kumbe tatizo lako ni unidirectional thinking.

Kila tawi linafanya vikao ambavyo vimeandikwa kinagaubaga kwenye katiba. Vikao hivyo vinajadili masuala mbalimbali.

Katika kipindi hiki cha kuandika katiba, vikao hivyo vinejadili pia maoni juu ya katiba.

Kama mjumbe wako hajui kuwa kuna vikao vya tawi, basi mmechagua mjumbe BOMU. Vikao vipo na minutes zipo, kama uko curious enough nenda kwa Katibu wa tawi wa CCM atakupa ratiba ya vikao vilivyokaliwa na vijavyo.
 
Acha Porojo we kilaza,mkutano wa ccm nani anahudhuria kwa hiyari yake mwenyewe? Msipowaaoomba watu kwa magari,kutangaza posho kwanza na kuweka wasanii wenu wauza unga wale ndio mpate watu

Hivyo vikao mnaviitisha usiku au muda gani ambao watu hawaoni? Kuweni na aibu kudanganyana kwa kujifariji halafu mnapiga makofi,yaani hakuna tofauti na majuha yooote poleni sana

Ulivyosikia kuna mtu kasema ashiriki siasa mpaka ahakikishiwe mshahara mnono na chama chake ukadhani tabia hiyo anayo kila mtu!
 
Back
Top Bottom