Kinana: CCM imevunja rekodi ukusanyaji wa maoni juu ya Rasimu ya Katiba Mpya

Kinana: CCM imevunja rekodi ukusanyaji wa maoni juu ya Rasimu ya Katiba Mpya

Kumbe tatizo lako ni unidirectional thinking.

Kila tawi linafanya vikao ambavyo vimeandikwa kinagaubaga kwenye katiba. Vikao hivyo vinajadili masuala mbalimbali.

Katika kipindi hiki cha kuandika katiba, vikao hivyo vinejadili pia maoni juu ya katiba.

Kama mjumbe wako hajui kuwa kuna vikao vya tawi, basi mmechagua mjumbe BOMU. Vikao vipo na minutes zipo, kama uko curious enough nenda kwa Katibu wa tawi wa CCM atakupa ratiba ya vikao vilivyokaliwa na vijavyo.



quote_icon.png
By ZeMarcopolo
Kuna watu kazi yao ni kupinga tu.

Hata hawajui vikao vya CCM ni vipi lakini wanapinga. Wanadhani CCM inafanya show off politics za kuruka angani na kuvaa migwanda.

Kama hamjui, CCM ina watu kila kijiji, mtaa kila sehemu nchini. CCM haihitaji kumpa posho Katibu Mkuu wake azunguke nchi nzima ili kujua wanachama wake wana maoni gani. Vikao vya CCM vya matawi vinatosha. CCM has that infrastructure, vyama vya magumashi havina infrastructure ndio maana watu kumi wanahangaika kuzunguka nchi nzima.


Mkuu ZeMarcopolo

Hapo kwenye red inamaana mjumbe wa mtaani kwangu hajuwi, na yule wa mtaa wapili hajui, Ni mtandaogani unaojivunia hapa jukwaani uliompana wa ccm usiwague hao wajumbe?

Mimi sio mwanachama wa ccm, lakini marakwamara hupitia kwa majirani zangu wajumbe wa ccm kufaham

kinachoendelea hususani masuala ya katiba, maana nikwamanufaa yetu sote sio ccm tu. Lakini wanashangaa kinana

kapata wapi takwimu hizo maana katika mitaa yao hawajawahi fanya mabalaza/vikao hivyo.
 
kuna haja ya chadema kuelimishwa ili wajue maana ya taasisi. maana wengi wao hata wanachoongea hakijulikani

We nae acha ubishi, wananchi wengi ambao pia ni wanachama wa vyama vya siasa hawakai kwenye majengo ya taasisi yenu useme eti utaongea nao wengine wasijue. Wanachama wa vyama vya siasa ni sehemu ya wananchi na njia iliyotumiwa na CHADEMA ni njia pekee ya kumfikia kila mwanachama tena kwa gharama ndogo ya muda na mali. Tatizo CCM mmechanganyikiwa, hamjui mnakoenda wala mnachokifanya kina impact gani kwa jamii. Hivi hamna hata wasomi wawasaidieni kufanya maamuzi!?
 
Mkuu ZeMarcopolo

Hapo kwenye red inamaana mjumbe wa mtaani kwangu hajuwi, na yule wa mtaa wapili hajui, Ni mtandaogani unaojivunia hapa jukwaani uliompana wa ccm usiwague hao wajumbe?

Mimi sio mwanachama wa ccm, lakini marakwamara hupitia kwa majirani zangu wajumbe wa ccm kufaham

kinachoendelea hususani masuala ya katiba, maana nikwamanufaa yetu sote sio ccm tu. Lakini wanashangaa kinana

kapata wapi takwimu hizo maana katika mitaa yao hawajawahi fanya mabalaza/vikao hivyo.

Mafanikio hayajakuwa asilimia 100. Hao wajumbe wasioudhuria vikao ndio wamesababisha mafanikio yasiwe asilimia 100, hata hivyo majority wameshiriki na mchakato umefanikiwa.
 
nashindwa kuelewa hawa jamaa wanataka katiba ya ccm au ya Tanzania
 
Nahisi CCM na CHADEMA wana tofautiana sana katika tafsiri ya neno wanachama, CCM inawatafsiri wanachama kuwa ni wale viongozi wa chama chao, ndio maana hata kwenye mchakato wa katiba wamewahusisha viongozi peke yao, CHADEMA inawatafsiri wanachama kuwa ni wale mwenye kadi na mapenzi mema na chama ambao ni wengi sana (mamilioni ya watanzania) hivyo njia bora ya kuwashirikisha kwenye mchakato wa katiba ni kuwafuata huko huko waliko na kufanya nao mazungumzo. Nani ana swali!?
 
CCM wao walichagua
njia ya kukusanya maoni siyo kwenye mikutano ya nje bali mikutano ya
ndani kwa maana hiyo kwa kiasi kikubwa ni wanachama wa CCM pekee
waliohudhuria hiyo mikutano ndiyo wanaofahamu vizuri process yao ya
ukusanyaji wa maoni.

Kuna thread ililetwa hapa JF ya tamko la Nape kuhusu utaratibu wao
katika ukusanyaji wa maoni kupitia wanachama wao kama taasisi.

naona sasa umechoka kufikiria au nyie ndo wale wazee ambao nape anaombea wapotee duniani!! umejarb sana kutetea namba ya hao waliotoa maoni ccm lakn swali linakuja inawezekana kweli watu milioni 2.3 watoe maoni wewe ucpate taarifa kua kuna hlo swala halaf wanachama hai wa ccm hawafiki hata hyo idadi muulize nape
 
Hiyo rekodi aliyoivunja iliwekwa lini na nani?? wanachama wa ccm milioni mbili unusu na zaidi wamekaa vikaoni ndani ya mwezi mmoja.....
 
Ndio Namshangaa huyu gamba mkuu adolay


Mkuu mama toto

Nimemuuliza [MENTION]ZeMarcopolo [/MENTION] kwamba nikweli meli ya katibu mkuu CCM bwana Kinana inasafirisha

nyara za serikali hususani pembe za ndovu? Nashangaa amekaakimya, sijuwi anawezeje kumwamini mtu anayefirisi taifa

letu kuhusu katiba? siajabu tukapata katiba ya maafiadi endapo hata akina Kinana wanapewa majukwaa kutoa takwimu za uwongo.
 
Mkuu kumbuka kuna aina mbili ya mabaraza ya katiba ambapo aina moja ni Mabaraza ya Katiba ambayo yaliundwa, yakasimamiwa na kuendeshwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba na aina ya pili ni Mabaraza ya Katiba ya Asasi, Taasisi na Makundi ya Watu wenye Malengo yanayofanana.

Maelezo yako naona kama unachanganya kati ya wajumbe wa mabaraza yaliyosimamiwa na Tume ya mabadiliko ya katiba ambapo wajumbe wengi wanasemekana walikuwa ni viongozi na wanachama wa CCM ambapo inadaiwa walifanyishwa vikao na kukaririshwa vipengere ambavyo walitakiwa wakavitoe kwenye vikao vya mabaraza hayo kama wajumbe.

CCM pia ni taasisi ambayo inaangukia kwenye aina ya pili ya mabaraza ya katiba ambayo muundo na uratibu na uendeshaji wake unatokana na jinsi inavyoona unafaa katika kuichambua rasimu ya Katiba. Wajumbe wake wanaweza wakawa pia ni kati ya wale waliokuwa pia kwenye kundi la kwanza lakini maoni yao katika kundi hii yanachukuliwa niya kitaasisi kama zilivyo Asasi na Vikundi vingine.

Unachosema nadhani ni sahihi, ila kuna kitu kimoja ambacho nadhani watu wengi hapa wanakitilia mashaka (mimi pia); ni idadi ya waliotoa maoni (2.6 millions). Hii ni idadi kubwa sana ya watu waliotoa maoni kwa kipindi cha mwezi mmoja na kama wiki moja hivi (walianza July 15) !. Kumbuka katika mikutano yote ya Tume ya Katiba kwa muda wote walioutumia kukusanya maoni walishiriki wananchi 1,365,337 na waliotoa maoni walikuwa 333,537 tu.

Huoni ni kitu cha ajabu kwa CCM kukusanya wanachama wake zaidi ya milioni mbili na nusu kwa kipindi cha roughly one month, bila wananchi wengine ku-note kinachoendelea!, Besides nimewapigia simu wanachama wawili wa CCM (active members), nao wanashangaa, wanasema labda wanachama wengine ila wao hawakuwa na habari na hilo !
 
jana nimeona kwenye taarifa ya habari chanel ten bwana kinana akawa anasema kwa mbwembe sana eti ccm ndo wameweka recod ya kukusanya maoni mengi sana za ya wanachama wake milioni mbili wametoa maoni yao kuhusu katiba mpya zaidi ya vyema vingine ni
Nikacheka sana na kujisemea kumbe wao walichukua maoni kwa wana ccm pekee ambao wenye kadi lakini kwa wale washabiki wao ambao awana kadi awakutoa maoni yao kuhusu muundo wa katiba mpya
Nikawaza pia na kusema chadema ina idadi kubwa sana hata zaidi ya ccm ya wanachama wao na je iweje kinana aseme wao ndo wamekusanya maoni mengi sana zaidi ya vyama vingine? Walimaanisha nini nape ingia hapa jukwaani tueleze hizo takwimu mmezitoa wp na kujua kwamba nyie ndo mmekusanya maoni mengi zaidi ya vyama vingine.
 
CCM hawajakusanya maoni yoyote zaidi ya kuwalisha maneno wanachama wao.
 
Kwa mujibu wa namba aliyotaja Jangili (Kinana) kila kikao cha kujadili katiba kilikuwa na at least watu 130. Katika ngazi za chini wanakodai maccmnwalifika watu 130 kuhudhulia kikao kimoja ni wengi sana hasa ukizingatia kuwa wanachama wa ccm waliobaki wengi ni wazee. Pia uzoefu wangu unaonyesha kuwa siku hizi watu hawahudhurii vikao vya ccm kaka hakuna posho. Huu ni uongo wa mchana toka kwa jangili na ni disgrace kwa chama chenu.

By the way baba yangu ni kiongozi wa CCM ngazi ya Kata, nimemdadisi kujua anaelewa chochote kuhusu hiyo mikutano ameshangaa, hakuna kikao chochote cha ccm chenye wanachama zaidi ya 50 kwa wakati mmoja kimefanyika katani kwake tangu uchaguzi wa 2010 uishe.
 
Kinana naomba kukuuliza hii katiba ni ya masisiem ama ya watanzania?Tukisema yale mabaraza mliyochakachukua ni kwa maslahi yenu na kwa ushahidi huu mtabisha?
Ama kweli masisiem ni ukoo wa panya......
 
Watakuja na wimbo tunamtaji wa wapiga kura milioni 2.6 nyi subiri
 
Mkuu angalia usemi wako kwa sababu katika usemi huu wewe ndiyo unaonekana 'mshamba'.

Maoni ya wananchi wote yalikusanywa na Tume ya Jaji Warioba kupitia Mabaraza ya Katiba ambayo yaliundwa, kusimamiwa na kuendeshwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba mojawapo ya mabaraza hayo ni mabaraza ya kata, wilaya n.k. ambayo yalilalamikiwa na CHADEMA kuwa yamejaa wanaCCM pekee badala ya wananchi wote.

Mabaraza ya CCM ni mabaraza ya taasisi ambayo yanaundwa na taasisi yenyewe. Haya ni sehemu ya pili ya aina ya mabaraza kama yalivyoainishwa katika Sheria ya Mabadiliko ya Katiba Sura ya 83. Haya ni pamoja na Asasi na makundi ya watu wenye mwelekeo na malengo yanayofanana hii ina maana kwamba hata walevi au wafungwa wanaweza wakaanzisha baraza lao la katiba kama tume ya Jaji Warioba itaona umuhimu wa kuwepo.

CCM kama Taasisi iliyoundwa na wanachama na pia kuwepo kwake kisheria kunategemea wanachama ndiyo maana imekusanya maoni ya wanachama wake kama Taasisi.

Hii ndiyo inapelekea kuwepo kwa hoja ya Jaji Warioba aliposema kuwa hawatachukua maoni ya "jukwaani wala ya kwenye helikopta" kwa cover la Taasisi pamoja na kwamba kauli yake hiyo ni debatable.

Kwa maana hyo unataka kutuambia ccm ndiyo ina idadi kuwa ya wanachama
? Zaidi ya chadema na baadhi ya vyama vingine?
Na ndo maana wamejitangaza kuwa wameweka record?
 
Kinana naomba kukuuliza hii katiba ni ya masisiem ama ya watanzania?Tukisema yale mabaraza mliyochakachukua ni kwa maslahi yenu na kwa ushahidi huu mtabisha?
Ama kweli masisiem ni ukoo wa panya......

wewe ndio hauko tz, umemaliza la saba kweli, kila taasisi iliunda mabaraza yake tofauti kabisa na yale ya tume, mfano kuna baraza la waandishi wa habari km taasisi, wanamziki na wacheza filamu etc
 
Back
Top Bottom