Precise Pangolin
JF-Expert Member
- Jan 4, 2012
- 13,010
- 6,678
Mkuu acha na huyo Mlevimkuu bado hoja inabaki ileile, ni lini na wapi ccm walikusanya maoni kama taasisi? Unazungukazunguka lakini ni bra bra tu...
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mkuu acha na huyo Mlevimkuu bado hoja inabaki ileile, ni lini na wapi ccm walikusanya maoni kama taasisi? Unazungukazunguka lakini ni bra bra tu...
Mkuu angalia usemi
wako kwa sababu katika usemi huu wewe ndiyo unaonekana 'mshamba'.
Maoni ya wananchi wote yalikusanywa na Tume ya Jaji Warioba kupitia
Mabaraza ya Katiba ambayo yaliundwa, kusimamiwa na kuendeshwa na Tume ya
Mabadiliko ya Katiba mojawapo ya mabaraza hayo ni mabaraza ya kata,
wilaya n.k. ambayo yalilalamikiwa na CHADEMA kuwa yamejaa wanaCCM pekee
badala ya wananchi wote.
Mabaraza ya CCM ni mabaraza ya taasisi ambayo yanaundwa na taasisi
yenyewe. Haya ni sehemu ya pili ya aina ya mabaraza kama yalivyoainishwa
katika Sheria ya Mabadiliko ya Katiba Sura ya 83. Haya ni pamoja na
Asasi na makundi ya watu wenye mwelekeo na malengo yanayofanana hii ina
maana kwamba hata walevi au wafungwa wanaweza wakaanzisha baraza lao la
katiba kama tume ya Jaji Warioba itaona umuhimu wa kuwepo.
CCM kama Taasisi iliyoundwa na wanachama na pia kuwepo kwake kisheria
kunategemea wanachama ndiyo maana imekusanya maoni ya wanachama wake
kama Taasisi.
Hii ndiyo inapelekea kuwepo kwa hoja ya Jaji Warioba aliposema kuwa
hawatachukua maoni ya "jukwaani wala ya kwenye helikopta" kwa cover la
Taasisi pamoja na kwamba kauli yake hiyo ni debatable.
nahisi kinana atakuwa amekusanya maoni ya wanaccm akiwa ndotoni
Chama
kilichokusanya maoni ya wanachama wao kwa uwazi ni chadema tu na
sivinginevyo, vingine ni kuforge data kwa kwenda mbele!
Badala ya kusema mimi
ninapotosha, ingekuwa vizuri ukaelewa kilichoko kwenye bandiko langu.
Wapi nimesema maoni ya CCM yamekusanywa kutoka kwenye Mabaraza ya Katiba
ambayo yaliundwa, kusimamiwa na kuendeshwa na Tume ya Mabadiliko ya
Katiba. Legally, Mabaraza yanayosimamiwa na kuendeshwa na Tume ya
Mabadiliko ya Katiba niya wananchi wote yanayotokana na wajumbe
waliochaguliwa na wananchi wote kupitia mitaa, kata, wilaya n.k
Sasa wewe unataka CCM ionyeshe jinsi ilivyokusanya maoni ya wanachama
wake wapi?. Hapa JF?.
Kwanza ukiangalia hata hiyo video haionyeshi hotuba nzima ya Katibu Mkuu
wa CCM kwa maana kuwa hatufahamu baada ya kutoa hayo maelezo aliendelea
kusema nini zaidi, lakini kikubwa zaidi anayetakiwa kujua njia ambazo
CCM walitumia kupata mapendekezo yao ni Tume ya Jaji Warioba kupitia
vidhibiti ambavyo Tume ya Jaji Warioba inazitaka taasisi mbali mbali
kukamilisha.
Chama kilichokusanya maoni ya wanachama wao kwa uwazi ni chadema tu na sivinginevyo, vingine ni kuforge data kwa kwenda mbele!
Labda hayo maoni kinana
alikuwa anakusanya serengeti na Ngorongoro wakati akiwa anavuna tembo
kama kawaida yake
Ndivyo ambavyo CCM
hupiga bao kirahisi bila wapinzani kujua, Kwani kabla hata chopa kuanza
kuruka CCM Ilikuwa na vikao vyake vya mabaraza ya kata na nililishuhudia
kule visiwani, Mabaraza ya Kata ya CCM yameanza kabla ya mabaraza ya
Tume ndiyo maana wengi walioyasikia walidhani ni yaliyoundwa na
Tume
Duuuuuh kweli CCM ina
wenyewe na wenyewe ndo waliotoa maoni!!..Zidumu fikra za
mwenyekiti..Hiki chama ni michosho miyeyusho isiyo na mwisho!! Kimekaa
kiuwizi uwizi tuuu na kitapelitapeli..Inafikia hatua mpaka wanaanza
kujiibia wenyewe..Hayo maoni walikusanya wapi? lini? kwa kutumia nini??
na waliwatumia watu gani?? Upuuzi huu unaofanywa na wahuni wachache
ndani ya CCM kuvuruga kila jambo haukubaliki tena!!
CCM wao walichagua njia ya kukusanya maoni siyo kwenye mikutano ya nje bali mikutano ya ndani kwa maana hiyo kwa kiasi kikubwa ni wanachama wa CCM pekee waliohudhuria hiyo mikutano ndiyo wanaofahamu vizuri process yao ya ukusanyaji wa maoni.
Kuna thread ililetwa hapa JF ya tamko la Nape kuhusu utaratibu wao katika ukusanyaji wa maoni kupitia wanachama wao kama taasisi.
Mkuu, wee endelea tu na porojo zako. Wenzako wako serious katika hili. Ccm ni chama ambacho kina watu makini sana na kinafanya kwa mujibu wa sheria. Thanx Jaji Warioba kwa kuwapasha ukweli CHADEMA. walithani kwa kuruka na chopa ndo kukusanya maoni kumbe walikuwa wanajipotezea muda bureHayo maoni ya Kinana atakuwa aliyatoa kwa TEMBO maana hakuna sehemu nyingine yalipopatikana ambayo iko wazi!!
Kweli CCM ina watu makini kama mwenyekiti wao kwa kuhongwa suti na vyandarua na kutoa dhahabu na tanzanite yetu. Pia kina watu kama kinana ambao wako makini katika ukamati wa tembo bila tembo kupiga kelele, watu makini kama Nchemba kwa kupiga bomu mabomu na bila kukamatwa, wako wengi naomba niishie hapo.Mkuu, wee endelea tu na porojo zako. Wenzako wako serious katika hili. Ccm ni chama ambacho kina watu makini sana na kinafanya kwa mujibu wa sheria. Thanx Jaji Warioba kwa kuwapasha ukweli CHADEMA. walithani kwa kuruka na chopa ndo kukusanya maoni kumbe walikuwa wanajipotezea muda bure
CCM imevunja rekodi yake yenyewe iliyoweka mwaka 1977 wakati wa mchakato wa uundwaji wa kariba ya sasa.OK, lets assume you and CCM are right. Kwa utaratibu walioutumia CCM, naomba ufafanuzi wa statement: CCM YAVUNJA REKODI UKUSANYAJI WA MAONI
Kama hiyo ndio njia waliyoitumia (kujifungia vyumbani), wamevunja rekodi ya nani? Iliyokuwa imewekwa na nani? Kulinganisha na ya nani? Kwa data zipi? Hebu waache longo longo za kujitafutia cheap populariy.
Mkuu kumbuka kuna aina mbili ya mabaraza ya katiba ambapo aina moja ni Mabaraza ya Katiba ambayo yaliundwa, yakasimamiwa na kuendeshwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba na aina ya pili ni Mabaraza ya Katiba ya Asasi, Taasisi na Makundi ya Watu wenye Malengo yanayofanana.mjomba umeshaambiwa vikao hivyo vya ndani unavyodai viliwahusu wana ccm wachache sana na vilikuwa siyo vya kutoa maoni kama unayodai bali vya kuwakaririsha mistari ya kwenda kusema mbele ya tume na wengine wakashindwa hata kusema wakafikia kusoma mbele ya wajumbe wa tume na wengine kuishia kutimuliwa. ccm haijawahi kuita wanachama watoe maoni yao
Mkuu, hiyo mioasho yenu haitawaondolea CHADEMA aibu na ujinga mliouonesha wakati wa mchakato wa kupata maoni ya Taasisi juu ya rasimu ya katiba mpya. Hakika CHADEMA mmejiaibisha sana na inaonesha ni namna gani chama kimekosa watu muhimu wa kuwashauri viongozi waoKweli CCM ina watu makini kama mwenyekiti wao kwa kuhongwa suti na vyandarua na kutoa dhahabu na tanzanite yetu. Pia kina watu kama kinana ambao wako makini katika ukamati wa tembo bila tembo kupiga kelele, watu makini kama Nchemba kwa kupiga bomu mabomu na bila kukamatwa, wako wengi naomba niishie hapo.
OK, lets assume you and CCM are right. Kwa utaratibu walioutumia CCM, naomba ufafanuzi wa statement: CCM YAVUNJA REKODI UKUSANYAJI WA MAONI
Kama hiyo ndio njia waliyoitumia (kujifungia vyumbani), wamevunja rekodi ya nani? Iliyokuwa imewekwa na nani? Kulinganisha na ya nani? Kwa data zipi? Hebu waache longo longo za kujitafutia cheap populariy.
Jaji Warioba alisema Idadi ya wananchi wanaohudhuria na kutoa maoni katika mikutano nayo imeongezeka. Kwa mfano, idadi ya wananchi waliohudhuria mikutano ya awamu ya kwanza walikuwa 189,526. Awamu ya pili ni 325,915 wakati wananchi waliohudhuria mikutano ya awamu ya tatu ni 392,385. Aidha, wananchi waliotoa maoni kwa kuzungumza katika mikutano ya awamu ya kwanza walikuwa 17,127. Awamu ya pili walikuwa 12,334 wakati wananchi 21,512 walizungumza katika awamu ya tatu;
Tume ya Mabadiliko ya Katiba