Kinana: CCM imevunja rekodi ukusanyaji wa maoni juu ya Rasimu ya Katiba Mpya


ukweli mchungu kwa chadema. hakika chadema hawapendi kujua ukweli labda kwa vile viongozi wao na wafuasi wao wengi wao ni vihiyo
 
Labda hayo maoni kinana alikuwa anakusanya serengeti na Ngorongoro wakati akiwa anavuna tembo kama kawaida yake
 
Chama
kilichokusanya maoni ya wanachama wao kwa uwazi ni chadema tu na
sivinginevyo, vingine ni kuforge data kwa kwenda mbele!

kuna haja ya chadema kuelimishwa ili wajue maana ya taasisi. maana wengi wao hata wanachoongea hakijulikani
 

mkuu, hawa chadema nafikiri wamepungukiwa kwa kiasi kikubwa sana uelewa juu ya ukusanyaji wa maoni ya taasisi. pia hawajui kama kinachhojadiliwa sasa ni rasimu ya katiba na si maoni ya wananchi juu ya katiba mpya. chadema walichokifanya si kukusanya maoni ya wanachama wao bali walikuwa wanawaambia wananchi nini msimamo wao juu ya rasimu hiyo.
 
Chama kilichokusanya maoni ya wanachama wao kwa uwazi ni chadema tu na sivinginevyo, vingine ni kuforge data kwa kwenda mbele!

Ndivyo ambavyo CCM hupiga bao kirahisi bila wapinzani kujua, Kwani kabla hata chopa kuanza kuruka CCM Ilikuwa na vikao vyake vya mabaraza ya kata na nililishuhudia kule visiwani, Mabaraza ya Kata ya CCM yameanza kabla ya mabaraza ya Tume ndiyo maana wengi walioyasikia walidhani ni yaliyoundwa na Tume
 
Labda hayo maoni kinana
alikuwa anakusanya serengeti na Ngorongoro wakati akiwa anavuna tembo
kama kawaida yake

hizo kejeli zenu zinadhihirisha namna gani mlivyo watupu kwenye jambo hili. by the way, kama nyie si members wa ccm, iweje mjue kuwa haijakusanya maoni ya taasisi?
 
Duuuuuh kweli CCM ina wenyewe na wenyewe ndo waliotoa maoni!!..Zidumu fikra za mwenyekiti..Hiki chama ni michosho miyeyusho isiyo na mwisho!! Kimekaa kiuwizi uwizi tuuu na kitapelitapeli..Inafikia hatua mpaka wanaanza kujiibia wenyewe..Hayo maoni walikusanya wapi? lini? kwa kutumia nini?? na waliwatumia watu gani?? Upuuzi huu unaofanywa na wahuni wachache ndani ya CCM kuvuruga kila jambo haukubaliki tena!!
 

mkuu, yaani hapo ndipo ccm inadhihirisha kuwa ni chama makini na kongwe. pia kina mfumo na viongozi thabiti toka mabalozi wa nyumba kumi hadi mwenyekiti Taifa. ccm wanajua sheria inasemaje na ndo maana walijipanga mapema
 
Hayo maoni ya Kinana atakuwa aliyatoa kwa TEMBO maana hakuna sehemu nyingine yalipopatikana ambayo iko wazi!!
 

wewe kwa vile umeajiriwa kutoa maoni ya chadema humu jf ndo unajidanganya kuwa ccm ni ya wachache. kumbuka mchakato wa chadema umeanzia kwa mabalozi na sasa ni ccm Taifa. hapo mmepigwa bao la kisigino. nyie sijui mtakaa lini vikao vya taifa maana viongozi wenu wanafurahia tu kuruka kwa chopa na kujichotea mamilioni ya fedha
 


OK, lets assume you and CCM are right. Kwa utaratibu walioutumia CCM, naomba ufafanuzi wa statement: CCM YAVUNJA REKODI UKUSANYAJI WA MAONI

Kama hiyo ndio njia waliyoitumia (kujifungia vyumbani), wamevunja rekodi ya nani? Iliyokuwa imewekwa na nani? Kulinganisha na ya nani? Kwa data zipi? Hebu waache longo longo za kujitafutia cheap populariy.
 
Hayo maoni ya Kinana atakuwa aliyatoa kwa TEMBO maana hakuna sehemu nyingine yalipopatikana ambayo iko wazi!!
Mkuu, wee endelea tu na porojo zako. Wenzako wako serious katika hili. Ccm ni chama ambacho kina watu makini sana na kinafanya kwa mujibu wa sheria. Thanx Jaji Warioba kwa kuwapasha ukweli CHADEMA. walithani kwa kuruka na chopa ndo kukusanya maoni kumbe walikuwa wanajipotezea muda bure
 
Nimeamini Chadema chama kubwa na ndio chama pekee cha upinzani maana kila anaepinga magamba hapa JF anaonekana ni chadema. LONG LIVE CHAMA DUME CHADEMA
 
Kweli CCM ina watu makini kama mwenyekiti wao kwa kuhongwa suti na vyandarua na kutoa dhahabu na tanzanite yetu. Pia kina watu kama kinana ambao wako makini katika ukamati wa tembo bila tembo kupiga kelele, watu makini kama Nchemba kwa kupiga bomu mabomu na bila kukamatwa, wako wengi naomba niishie hapo.
 
CCM imevunja rekodi yake yenyewe iliyoweka mwaka 1977 wakati wa mchakato wa uundwaji wa kariba ya sasa.
 
Mkuu kumbuka kuna aina mbili ya mabaraza ya katiba ambapo aina moja ni Mabaraza ya Katiba ambayo yaliundwa, yakasimamiwa na kuendeshwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba na aina ya pili ni Mabaraza ya Katiba ya Asasi, Taasisi na Makundi ya Watu wenye Malengo yanayofanana.

Maelezo yako naona kama unachanganya kati ya wajumbe wa mabaraza yaliyosimamiwa na Tume ya mabadiliko ya katiba ambapo wajumbe wengi wanasemekana walikuwa ni viongozi na wanachama wa CCM ambapo inadaiwa walifanyishwa vikao na kukaririshwa vipengere ambavyo walitakiwa wakavitoe kwenye vikao vya mabaraza hayo kama wajumbe.

CCM pia ni taasisi ambayo inaangukia kwenye aina ya pili ya mabaraza ya katiba ambayo muundo na uratibu na uendeshaji wake unatokana na jinsi inavyoona unafaa katika kuichambua rasimu ya Katiba. Wajumbe wake wanaweza wakawa pia ni kati ya wale waliokuwa pia kwenye kundi la kwanza lakini maoni yao katika kundi hii yanachukuliwa niya kitaasisi kama zilivyo Asasi na Vikundi vingine.
 
Mkuu, hiyo mioasho yenu haitawaondolea CHADEMA aibu na ujinga mliouonesha wakati wa mchakato wa kupata maoni ya Taasisi juu ya rasimu ya katiba mpya. Hakika CHADEMA mmejiaibisha sana na inaonesha ni namna gani chama kimekosa watu muhimu wa kuwashauri viongozi wao
 

Mkuu Kwa maneno ya Viongozi wa CCM, rekodi walioivunja ni hii hapa,

Wakati wao CCM wanadai wamefanya jumla ya Mabaraza 18,879, huku washiriki wakiwa 2,618,753 ambayo hayo yamefanyika kuanzia 15/07/2013 up to 24/08/2013 when compare to above figure.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…