Kinana: CCM ni kubwa kuliko Serikali

Kinana: CCM ni kubwa kuliko Serikali

Ibara ya 34 (1) (2) (3) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iko wazi:

34 (1) Kutakuwa na serikali ya Jamhuri ya Muungano ambayo itakuwa na mamlaka juu ya mambo yote ya Muungano katika Jamhuri ya Muungano na pia juu ya mambo mengine yote yahusuyo Tanzania Bara.

"mambo yote"

...

Nchi inaongozwa na katiba wala sio chama. Na katiba imeweka wazi kuwa Serikali ndio yenye mamlaka katika mambo yote, Kinana anazingua.

Yesu ni Mwokozi
mambo yote YA MUUNGANO katika Jamhuri ya Muungano na pia juu ya mambo mengine yote YAHUSUYO TANZANIA BARA.
 
Serikali ndio inayoshika hatamu, sio chama jameni
Alikuwa anapokea wanachama wapya katika mikutano ya serikali,
Anafanyia vikao vya chama ofisi namba moja,
Walinzi wake wanavaa sare za chama,
Alimteua kanali wa jeshi kuwa kada wa chama,
Alimteua kada wa chama kuwa mkuu wa watumishi!,
Alitumia vyombo vya dola kuwa trepu wanachama wenzake waliokuwa wanamsema!

Mambo ni mengi, hayo ni baadhi tu tuliyoyaona kwa nje.

Unaona haya ni sawa
 
achana na yule mzee alikuwa wa hovyoo

Alithubutu kuwaambia wananchi wake kuwa hawakupata maendeleo kwa sababu walichagua chama kingine ...

JESUS IS LORD
 
"Kasema CCM sio chombo cha serikali, CCM haitokani na Serikali, ila Serikali zote mbili (Tanzania na Zanzibar) zinatokana na CCM, CCM haipokei maagizo kutoka Serikalini, ila Serikali inapokea maagizo kutoka CCM, hii ni kupitia ilani na sera zilizotungwa na viongozi mbali mbali wa Serikali!"

Huu ni ujumbe mzito samaa kwa team sukuma Gang

Hapa naona kuna watu wanaenda kunyooshwa
Of course huo ndio ukweli ambao kuna wachache hawaupendi
 
Naona kwamaneno haya ya chama hakiagizwi na serikali itatusaidia kuwanyosha;-
(1) KATELEFONI FIX-uwongouwongo wake Kinana tunaomba mwambie kwenye ilani yenu hamna ukurasa wa kusema uwongo.
(2)MWIGULU NCHEMBA-kufanya ubabaishaji kwenye masuala ya uchumi na fedha .
(3) SELEMANI JAFO-kutuletea kamati FEKI ya mto mara na Profesa Wake MANYELE sijui kwenye ilani yenu mmesahau majukumu ya NEMC.
(4)DOROTH GWAJIMA:- sijui kama anampango wowote kuitafsiri ilani yenu kutatua matatizo yanayowakabili machinga nchini.
(5)JOYCE NDALICHAKO;-naona ni mtu ambaye kama wizara ya elimu ilimshinda sidhani kama anaubavu wa kuweka ilani yenu kwa vitendo kwenye wizara ya sasa
 
Kinana katajwatajwa sana na lile vuvuzela pendwa la le dikteta kupanga njama ya kumpeleka mavumbini
 
Chama ndicho kinaunda serikali.. kwa hiyo ni sahihi: kwa sasa CCM ndiyo maboss na wana haki ya kuisimamia serikali kuhakikisha wanatekeleza ilani yake.

Serikali ni pana kuliko chama chochote cha siasa. Kinana anarudia maneno ya Moi haya ambayo baadae yalimuumbua
 
Inawezekana Kinana pia anamaanisha mwenyekiti amewekwa mfukoni na "wajanja wa mjini" ila yeye kwa nje anamaanisha chama ndio kina nguvu kuizidi serikali.

On the other side, alichokisema kinaweza kuwa sawa, au kinyume chake pia ikawa sawa, kwasababu pande zote mbili zinaongozwa na mtu mmoja, na hakuna wa kumpinga toka upande wowote, wote humshangilia hata akiwagombeza.
Mwenyekiti wa chama ndio Boss katika chama !! Na upande wa serikali mkuu wa serikali na mkuu wa nchi ni Rais !! !!?
 
Hii ni kweli, katiba mpya inahitajika kuondoa nguvu ya kauli hii hatuwezi kuwa na serikali inayopokea maagizo kutoka kwenye chama ambayo ni rahisi sana kuua upinzani ibaki madarakani
 
"Kasema CCM sio chombo cha serikali, CCM haitokani na Serikali, ila Serikali zote mbili (Tanzania na Zanzibar) zinatokana na CCM, CCM haipokei maagizo kutoka Serikalini, ila Serikali inapokea maagizo kutoka CCM, hii ni kupitia ilani na sera zilizotungwa na viongozi mbali mbali wa Serikali!"

Huu ni ujumbe mzito samaa kwa team sukuma Gang

Hapa naona kuna watu wanaenda kunyooshwa
Sasa hv Kuna watu watakimbia nchi,wananchi lazima wasage meno kwa gharama kubwa za maisha.
 
Yuko sahihi kwasababu serikali inatumia policy's za sisiemu......
 
"Kasema CCM sio chombo cha serikali, CCM haitokani na Serikali, ila Serikali zote mbili (Tanzania na Zanzibar) zinatokana na CCM, CCM haipokei maagizo kutoka Serikalini, ila Serikali inapokea maagizo kutoka CCM, hii ni kupitia ilani na sera zilizotungwa na viongozi mbali mbali wa Serikali!"

Huu ni ujumbe mzito samaa kwa team sukuma Gang

Hapa naona kuna watu wanaenda kunyooshwa
TUNAPOSEMA CCM ni POLISI, TUME TISS tupo sahihi kumbe vyote hivyo vinapokea Maagizo ya CCM
ndio maana kila kiwapatacho WAPINZANI ni Maagizo ya CCM kwa SERIKALI
KAMATA Mbowe mpe KESI ya Ugaidi ni Agizo la CCM kwa Serikali
 
Ili chama kishike dola, kishinde chaguzi zake
Lazima kiwe kwenye mfumo huu wa ccm
Yaani chama alafu $

Ova
Ni. Kweli kwamba kwa mfumo wetu ili ushike dola inakupasa kuwa na chama.

Na kwenye uchaguzi huwa sera zinanadiwa za vyama mbali mbali.

Lakini sasa ukishashika dola kinachoangaliwa ni interest za Wananchi na sio za Chama.

Hivyo kusema kwamba Chama Kipo juu ya serikali huko ni kujipa mamlaka makubwa sana yanayokwenda kinyume cha katiba.

Serikali haipaswi kusikiliza maagizo ya chama, kwani yenyewe ndio taasisi yenye mamlaka ya juu kikatiba.

Bali chama kinapaswa Kuishauri serikali.
 
Back
Top Bottom