Kinana, Mbowe, Vuai, Mnyika, Chenge na Heche wajifungia kwa vikao vya saa 4 Courtyard

Kinana, Mbowe, Vuai, Mnyika, Chenge na Heche wajifungia kwa vikao vya saa 4 Courtyard

KAMA NI HIVYO NI SAWA ILA VIKAO HIVYO HIVYO WAKIKAA NA ZITO MNAANZA MATUSI, MFANO ANGEKUWA NI ZITTO UNGEONA MITUSI HAPA AU UNGESIKIA CCM B HUYOO,CJUI MSALITI NK, MKOMAE MUACHE UTOTO

Chama Cha upinzani Ni kimoja vingine Ni matawi ya ccm.
 
Hapana mkuu Mimi nafurahi wakikaa pamoja viongozi wetu ili kujenga mshikamano na upendo miongoni mwetu ili tuishi kwa amani na kuaminiana, Sote tunajenga Taifa moja hivyo lazima kila mtu ajione Anayo nafasi katika ujenzi wa Taifa letu na ajisikie fahari kuwa sehemu ya Tanzania

Uwe unaongea hivi kila siku utafika mbali.
 
Kinana atakuwa anawafundisha siasa...waachane na harakati za mahakamani..wajue siasa..
Wajue Ku compromise madogo ili wapate makubwa...
Siasa sio kushinda Kesi mahakamani

Lisu kawapotosha kupenda mahamani na uana harakati.
 
KAMA NI HIVYO NI SAWA ILA VIKAO HIVYO HIVYO WAKIKAA NA ZITO MNAANZA MATUSI, MFANO ANGEKUWA NI ZITTO UNGEONA MITUSI HAPA AU UNGESIKIA CCM B HUYOO,CJUI MSALITI NK, MKOMAE MUACHE UTOTO
Zitto anakosolewa siyo kwa kukaa na CCM, bali hukaa wakifanya nini?

Mbowe alikaribishwa na Magufuli kwenye mkutano Mwanza, alichokisema kinafanana na alichokisema Zitto alipokaribishwa na Magufuli akiwa Kigoma?

Umeona mwaka huu alichokisema Zitto alipokaribishwa na Rais Samia Suluhu Pale Kigoma??
 
Nini kinaendelea? Hili ni swali linalogonga vichwa vya Watanzania wengi wenye shauku ya kujua majadiliano baina ya viongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), yatahitimishwa lini.

Jana vigogo wa vyama hivyo wasiozidi 15 walijifungia kwa saa nne katika Hoteli ya Courtyard jijini hapa, kuendeleza majadiliano yaliyoanza miezi sita nyuma.

Majadiliano ya kwanza yalifanyika Ikulu ya Chamwino, Dodoma, Mei 20 mwaka huu kwa Rais Samia Suluhu Hassan akiambatana na viongozi waandamizi wa CCM na Serikali, ambao walikutana na ujumbe wa viongozi wa CHADEMA, ulioongozwa na Mwenyekiti wao, Freeman Mbowe.

======================

Tangu wakati huo, inaelezwa timu za viongozi wa vyama hivyo vyenye wanachama na wafuasi wengi nchini, zimekuwa zikikutana kwa siri kubwa katika majadiliano ambayo yamekuwa na lengo la kuboresha mazingira ya kisiasa nchini.

Usiri wa vikao hivyo umekuwa ukitawala pande zote na taarifa zao zimekuwa zikifunikwa na zile za kikosi kazi kilichokuwa na jukumu la kupitia maoni ya wadau wa demokrasia ambacho ripoti yake ikiwa na masuala mbalimbali, imekabidhiwa hivi karibuni kwa Rais Samia.

Jana, vigogo wa CCM wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti-Bara, Abdulrahman Kinana na upande wa Chadema, ukiongozwa na Mbowe waliongoza wajumbe wao kujifungia katika kikao hicho cha siri.

Kikao hicho, kilianza saa sita adhuhuri mchana na kukamilika 10:06 jioni katika hoteli hiyo.

Awali, kabla ya kuanza kwa kikao hicho, viongozi wa CCM walikuwa wa kwanza kuwasili wakiongozwa na aliyewahi kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Andrew Chenge aliyewasili saa 5:14 asubuhi.

Saa 5:17 alifika Naibu Katibu Mkuu wa zamani wa CCM-Zanzibar, Vuai Ali Vuai akiwa na baadhi ya viongozi wengine waandamizi wa chama hicho.

Gazeti hili lililokuwa limeweka kambi katika hoteli hiyo, lilimshuhudia Mbowe akiwasili saa 5:46 asubuhi akipishana dakika 11 na Kinana aliyefika saa 5:55 na wote walipoingia walikwenda moja kwa moja kwenye ukumbi wa Welington ambako kikao hicho kilifanyika.

Baada ya vigogo hao kuingia, saa 5:59 na saa 6:02 mchana, waliingia Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika na John Heche mtawalia. Heche ni mjumbe wa kamati kuu ya chama hicho.

Saa 6:07 mchana, wanasheria wa Chadema, Jeremiah Mtobesya na Jonathan Mdeme nao waliingia katika kikao hicho.

“Huu ni mwendelezo wa vikao vyetu, ni nini kimejadiliwa, subirini muda ukifika mtaambiwa,” alieleza mmoja wa wajumbe wa kikao hicho, ambaye hakutaka kuzungumza kwa undani.

Hata hivyo, taarifa ambazo gazeti hili linazo ni kwamba, majadiliano hayo yamefikia hatua nzuri na yatakapokamilika yatawekwa hadharani.

“Watu walijua baada ya kikosi kazi haya majadiliano hayapo, la hasha! Yanaendelea kama kawaida na sasa yapo hatua nzuri.”

“Mwisho Watanzania wataelezwa nini kinaendelea na bila shaka tutafanya mkutano na waandishi kwa pamoja,” alieleza kiongozi mmoja wa CCM ambaye si miongoni mwa wajumbe wa kamati hiyo.

“Mama kama alivyoahidi, anaendesha nchi kwa 4R, akiamini hiyo ndiyo njia ya kuwaleta wananchi pamoja. Nchi ni yetu sote na kila mmoja ana wajibu wa kuijenga.”

4R hizo ni (Reconcilation - maridhiano, Resiliency - ustahamilivu, Reforms -mabadiliko na Rebuilding - kujenga upya) ambazo alizielezea katika makala yake maalum aliyoandika kuadhimisha miaka 30 tangu kurejea kwa mfumo wa vyama vingi vya siasa nchini.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Shaka Hamud Shaka alipoulizwa na gazeti hili alisema hana uhakika kama kuna kikao hicho kwani, yeye si mjumbe wa vikao hivyo.

“ Lakini ninachojua kama wamekutana ni mwendelezo wa majadiliano na kama kimefanyika muda ukifika tutawajulisha.”

Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika alipoulizwa kuhusu kikao hicho hakuwa tayari kufafanua chochote zaidi ya kusema: “Aliyekwambia kuwa kuna kikao kimefanyika, atakuwa na uwezo wa kukueleza zaidi. Asante.”

Baada ya kumalizika kwa kikao hicho, waliokuwa wa kwanza kutoka ndani ya ukumbi ni Mbowe na ujumbe wake ikiwa ni saa 10 jioni kisha wakafuatia Kinana na wenzake. Wakati wote wa kikao hicho ukiendelea, hali ya ulinzi ilikuwa wa kawaida na shughuli nyingine zilikuwa zikiendelea kama kawaida, huku magari ya viongozi hao yakijazana eneo la mapokezi.

MWANANCHI
Wahuni waliyoshika ccm wanatafuta namna ya kuua wimbi na mwenendo wa kimapinduzi kwenye fikra za watanzania uliyorejeshwa na magufuli.
Hebu fikiri ccm wanafanya mazungumzo gani ya siri na chama cha kiliberali na cha wapinga maendeleo kama chadema. Isitoshe ccm iliigaragaza chadema kabisa kwenye uchaguzi hivyo kuonesha wananchi wanaunga mkono mwendo wa kushoto wa kimapinduzi, mwendo wa asili wa chama cha mapinduzi chama cha azimio la arudha.
Kama ni maswala ya katiba chadema ni mawakala wa kuua muungano na hawataki kipengele chenye kusema tanzania ni nchi ya kijamaa kwa maana ni nchi inayojenga usawa.
 
allen killewela>siasa zipo za aina tatu duniani, kuna siasa za mlengo wa kati,# kuna siasa za mlengo wa kushoto kupinga kila kitu,na kuna siasa za mlengo wa kulia kuunga mkono kila kitu!Zitto anafanya siasa za mlengo wa kati,hawezi kusimama jukwaani kuzungumza mnavyotaka nyinyi chadema!
 
Umeshaondoka Ulaya??!
Mkutano mkubwa kuongelea siasa eti maelewano wakati nchi ina hali ngumu

Hawajadili kutuvusha bali wanawaza matumbo yao tu
Hapo wanaahidiwa hela tu hakuna jipya
Unafanya siri kwani vita hii
 
Mataga umekoroga, wewe mwenyewe huewezi elewa hiki ulichoandika.
Mambo ya chini chini kwenye issue isiyotaka usiri kama uhuru wa siasa itakuja kuzaa kashfa! Usikute kuna maslahi ya watu yanajadiliwa kabla ya makubaliano kwenda public!
 
Kama kwenye karavati kikao yupo heche Sina wasiwasi na hicho kikao
 
Kinana atakuwa anawafundisha siasa...waachane na harakati za mahakamani..wajue siasa..
Wajue Ku compromise madogo ili wapate makubwa...
Siasa sio kushinda Kesi mahakamani
Kama ni mwalimu mzuri wa SIASA, mbona hakumfundisha JPM, badala yake akapelekwa KIZIMBANI na KUHUKUMIWA?
 
Makamu Mwenyekiti ndio humuwakilisha Rais kwenye vikao vingi maana muda mwingi yupo busy .
Utetezi dhaifu sana huu. Rais anayejitambua hawezi kuwa too busy kiasi akashindwa kutenga muda wa kukaa na wenyeviti wa vyama vya upinzani na kujadili maswala muhimu ya mustakabali wa taifa hili.
 
allen killewela>siasa zipo za aina tatu duniani, kuna siasa za mlengo wa kati,# kuna siasa za mlengo wa kushoto kupinga kila kitu,na kuna siasa za mlengo wa kulia kuunga mkono kila kitu!Zitto anafanya siasa za mlengo wa kati,hawezi kusimama jukwaani kuzungumza mnavyotaka nyinyi chadema!
Hivi lile jengo mlilosema mmejenga, mlianza ujenzi lini?
 
Kinana atakuwa anawafundisha siasa...waachane na harakati za mahakamani..wajue siasa..
Wajue Ku compromise madogo ili wapate makubwa...
Siasa sio kushinda Kesi mahakamani
Kinana ana siasa gani za kufundisha watu nchi hii?

Wewe una uhakika gani kwamba wana compromise madogo na kupata makubwa na isiwe kinyume chake, wakubali ku compromise makubwa wapate madogo?

Kushinda kesi mahakamani kumeingiaje kwenye hayo majadiliano?

Watu mnajiandikia tu kama vile mmeshikwa makalio.
 
allen killewela>siasa zipo za aina tatu duniani, kuna siasa za mlengo wa kati,# kuna siasa za mlengo wa kushoto kupinga kila kitu,na kuna siasa za mlengo wa kulia kuunga mkono kila kitu!Zitto anafanya siasa za mlengo wa kati,hawezi kusimama jukwaani kuzungumza mnavyotaka nyinyi chadema!
Kuhusu aina za siasa inaonesha hujui kitu kuhusu jambo hilo. Kushoto ni Ujamaa, kulia ni Ubepari na kati ni nusu kwa nusu.
 
Kinana atakuwa anawafundisha siasa...waachane na harakati za mahakamani..wajue siasa..
Wajue Ku compromise madogo ili wapate makubwa...
Siasa sio kushinda Kesi mahakamani
Mkuu kesi ilifunguliwa na waliovuliwa uanachama how Tena wao ndio wameenda mahakamani?

Kuhusu compromise mbona zaidi ya mwaka Sasa hawafanyi rallies huko sio compromising na utawala uliopo?

Chadema wanajua sana compromise walifanya hivyo tokea enzi za Jk walipata Nini? Wakamnyeyekea JPM na kuomba maridhiano Mwanza walipata Nini?

Nadhani Cha muhimu wanachotaka Samia na Mbowe ni HAKI na USAWA kwenye uwanja wa siasa that's all sio kunyenyekeana mbona Ruto hakunyenyekea na amekua Rais? Odinga aliyecompromise amepata Nini?

HAKI HAKI HAKI is the politics we want sio compromising na kutegemea huruma za mtu
 
Back
Top Bottom