Naamini viongozi wangu wa CCM lazima wamewafunda na kuwafundisha masuala ya kiuongozi ya kuwa na vifua na kuwa Wasiri wakati vikao vinaendelea, Bila Shaka lazima semina ilitangulia ya kuwapa viongozi wa chadema ili wajuwe umuhimu wa wao kushiriki katika vikao hivyo na Nini kinapaswa kufanyika wakati mazungumzo yanaendelea ndio maana unaona viongozi wa chadema wamegoma kusema kilichozungumzwa maana wameshalishwa madini toka CCM ya namna ya kuwa na subiri ya midomo yao,
Hicho ndicho huwa naandikaga humu kuwa kiongozi unapaswa kuwa na kifua ,Mtulivu,Busara,Subira na hekima, kujuwa wakati gani uongee na wakati gani ukae kimya, siyo kupelekeshwa tu na mihemuko ya vijana wao wanaowaka Kama Moto wa petroli, Naamini Nguli wa Siasa ndugu Kinana amefanya kazi kubwa ya kuwaelimisha viongozi wa Chadema ndio sababu ya kuona wamebadilika kitabia na kuwa Wasiri
Nawapongeza katika hili na waendelee hivi hivi mpaka mwisho wa mazungumzo yao, wawe wenye Subira,hekima,busara,utulivu na kujuwa umuhimu wa usiri wakati mazungumzo yanaendelea, siyo kukimbia tu kuripoti mambo ambayo hayapaswi kuripotiwa au kutolewa hadharani wakati bado hawajafika mwisho wa mazungumzo, lazima wajuwe hata mwisho wa mazungumzo Ni Nani atapaswa kuzungumza kwa kila upande hasa chadema maana kwa CCM hakuna shida maana ndio chama kiongozi kinachojuwa utaratibu unaopaswa kuwepo na kufuatwa
Kiukweli Mimi Lucas Mwashambwa Najivunia Sana kuwa mwanachama wa CCM, kwa kuwa hiki Ni chama kilichokomaa kisiasa, chenye hadhina ya viongozi katika kila idara ,CCM Ni chuo Cha uongozi na mahali pekee ambapo wanachama wote tuna nafasi sawa ,hakuna ubaguzi Wala unyanyasaji ndani ya CCM,
Kazi iendeleee