Kinana, Mbowe, Vuai, Mnyika, Chenge na Heche wajifungia kwa vikao vya saa 4 Courtyard

Kinana, Mbowe, Vuai, Mnyika, Chenge na Heche wajifungia kwa vikao vya saa 4 Courtyard

Wanajadiliana jinsi ya kugawana buyu la asali...

Wanasiasa ni wabinafsi sana... Kinachojadiliwa sio kwa niaba ya wananchi bali jinsi gani watashea kutafuna mali za Taifa..

Ukiniambia au Ukinionyesha Mbowe au Kinana kama wana uchungu wananchi, na wanajadiliana kwa manufaa ya wananchi...Nitambea kwa miguu Dar to kigoma
Kikao nicha siri wewe hayo yakugawana buyu la asali umeyatoa wapi au nyie ndo wale msiopenda mambo mema nchi hii.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
W
Kuna siku CCM, CDM na ACT wataamka watajikuta wapo out of touch na wananchi.

Hawa vijana chini ya 30 watakuja kubadilisha siasa za hii nchi.

Watoto gani hao?. Hawa ambao wanatembea uchi na kuigiza ushoga?. Tanzania ijayo itakuwa mbaya kuliko Sasa hivi, maana itajaa watoto machawa wengi na walamba lips wengi. Hakuna jipya.
 
Kwa ivo kama kuna hali ngumu ndiyo shughuli za kutafuta maelewano hazitakiwi ziwepo?

Hivi CHADEMA kwani wanaongoza nchi hadi wajadili kutuvusha? Bunge na serikali si ndiyo zinawajibu wa kutuvusha, sasa CHADEMA inaingiaje?

Umejuaje kama wanaahidiwa hela?

Kwani kikao na mkutano wa hadhara ni sawa??
Mkuu wapinzani ni wananchi pia na wana haki ya kuieleza Chama tawala kama hawafanyi inavyotakiwa

Kuna mengi ya kuongea hadharani zaidi ya Vikao vya siri
 
Mkutano mkubwa kuongelea siasa eti maelewano wakati nchi ina hali ngumu

Hawajadili kutuvusha bali wanawaza matumbo yao tu
Hapo wanaahidiwa hela tu hakuna jipya
Unafanya siri kwani vita hii

Tuache kujificha kwenye matatizo. Bunge lipo, maafisa watendaji kata wapo, madiwani wapo, wenyeviti wa vijiji wapo, nk Kama unashida ya maendeleo kawaone hao. Yani vyama viwili kukutana imekuwa nongwa.
 
Kuna siku CCM, CDM na ACT wataamka watajikuta wapo out of touch na wananchi.

Hawa vijana chini ya 30 watakuja kubadilisha siasa za hii nchi.

Problem hivyo vyama vina wa suck in hao vijana na kuwageuza againts vijana wenzao. But hii haimaanishi haiwezekani, i can still smell changes
 
Yanaanza lini hayo maonob, niyasubiri Kwa kigoda kabisa
Omba, usisubiri Hadi yatokee maana ukisubiri yatokee utakuwa umechelewa.

Omba binafsi,ombea familia Yako, Taifa na Dunia nzima Ili madhara yasiwe makubwa sana.

Timeframe ni 20 Oct Hadi 20 march next yr.

October Hadi December mapambano yanaendelea ktk spiritual realm bt uhalisia utaanza onekana miezi mitatu kuanzia January.

Mashariki ya Kati ndo Dira ya yatokeayo Ulimwenguni.
 
Wewe huoni chadema walau wamebadilika kidogo kitabia na kuwa na Tabia za kiutu uzima za kuwa na Subira na utulivu

Kinana wa kumsema vibaya Magufuli kwenye simu Hana uwezo huo. Yeye afundishe usengenyaji kwenye simu na ujangili wa pembe za ndovu.
 
Bila kupewa semina na ndugu Kinana mpaka muda huu wangekuwa wameshaanza kusema kila mtu na lake Kama kawaida yao ya kutaka kuwa wakwanza,maana ndani ya Chadema kila mtu Ni kambale

Semina gani?. Kumbe hujui tofauti ya semina na kikao?.
 
Semina gani?. Kumbe hujui tofauti ya semina na kikao?.
Semina lazima ilitangulia kabla ya kikao kwa ajili ya kuwafunda viongozi wa chadema kuhusu na kuzingatia Sheria na maadili ya kikao, siyo kuanza kuongea ongea tu Kama walivyozoea kufanya, ndio maana unaona leo walau wamejirekebisha baada ya kupewa madini toka kwa nguli wa sayansi ya siasa ndugu Kinana
 
Katiba mpya ni muhimu sababu matatizo tunayoyapitia kama Nchi, maji, mafuta, mfumuko wa Bei nk nk ni ya KIMFUMO hivyo ikiandikwa na kupatikana, itatibu hayo yote.
Kuna mahala tunaogopa kuwa nayo
Labda visiwa wanataka mengi who knows
Haiwezekani wakajivuta hivi tangu JKN
Alisema kwa katiba hii anaweza kuwa Dictator lakini hakubadili why?
 
Mambo ya chini chini kwenye issue isiyotaka usiri kama uhuru wa siasa itakuja kuzaa kashfa! Usikute kuna maslahi ya watu yanajadiliwa kabla ya makubaliano kwenda public!

Mbona mambo ya siasa yalishawekwa wazi na kikosi kazi Cha rais. Haya mazungumzo ni Kati ya CHADEMA na CCM, wao watatoa kila kitu mwishoni.
 
Please, hivyo ni vikao vya CHADEMA na CCM wanajadiliana mambo ya kufanya siasa kwa Uhuru na sio mafarakano Kama ilivyokuwa Happ nyuma. Kuhusu maendeleo ya wananchi Kuna Rais, Mawaziri, bunge, Halmashauri na wenyeviti wa vijiji na vitongoji. Walaumu hao Kama hujapata maendeleo
Kufanya siasa kwa Uhuru ndio muhimu kuliko kero za wananchi kuhusiana na tozo na mfumuko wa bei, kero za maji na umeme?

Kataa au kubali wanasiasa wa Afrika ni wa Binafsi, wanashughulikia matumbo yao tu.
 
Mkuu wapinzani ni wananchi pia na wana haki ya kuieleza Chama tawala kama hawafanyi inavyotakiwa

Kuna mengi ya kuongea hadharani zaidi ya Vikao vya siri
Wangeongeaje hadharani wakati ata vikao vya ndani tu walikua wanafurushwa na polisi.Ksma kuna mambo unayaona hayaendi sawa ni swala la kila mtu kusimama na kusema sio wengine kujibanza nyuma ya migongo ya watu alafu wao ndo wanakua wa kwanza kutoa lawama kwa wale waliojitokeza kusema na wakakutana na mazila.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
CHADEMA kimekuwa ni chama NDOIGE. Ukikipenda ndiyo umekipenda na ukikichukia ndiyo umekipenda pia!!
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Kufanya siasa kwa Uhuru ndio muhimu kuliko kero za wananchi kuhusiana na tozo na mfumuko wa bei, kero za maji na umeme?
Wananchi wanao Wenyeviti wa vijiji/mitaa, madiwani, wabunge na Rais. Unataka watu wasiotajwa kikatiba kushughulika na matatizo ya watanzania wafanye kazi isiyowahusu?
 
Back
Top Bottom