Kinana, Mbowe, Vuai, Mnyika, Chenge na Heche wajifungia kwa vikao vya saa 4 Courtyard

Kinana, Mbowe, Vuai, Mnyika, Chenge na Heche wajifungia kwa vikao vya saa 4 Courtyard

Kinana atakuwa anawafundisha siasa...waachane na harakati za mahakamani..wajue siasa..
Wajue Ku compromise madogo ili wapate makubwa...
Siasa sio kushinda Kesi mahakamani
Kwamba kinana ni proffesional wa siasa Tanzania, basi kama nchi bado tuna safari ndefu sana ikiwa huyu pembe za ndovu ndio mwalimu wa siasa, atlist ungesema anafundisha ufisadi na ukwapuaji kidogo ningekuelewa
 
Mkutano mkubwa kuongelea siasa eti maelewano wakati nchi ina hali ngumu

Hawajadili kutuvusha bali wanawaza matumbo yao tu
Hapo wanaahidiwa hela tu hakuna jipya
Unafanya siri kwani vita hii
 
Mkutano mkubwa kuongelea siasa eti maelewano wakati nchi ina hali ngumu
Kwa ivo kama kuna hali ngumu ndiyo shughuli za kutafuta maelewano hazitakiwi ziwepo?
Hawajadili kutuvusha bali wanawaza matumbo yao tu
Hivi CHADEMA kwani wanaongoza nchi hadi wajadili kutuvusha? Bunge na serikali si ndiyo zinawajibu wa kutuvusha, sasa CHADEMA inaingiaje?
Hapo wanaahidiwa hela tu hakuna jipya
Umejuaje kama wanaahidiwa hela?
Unafanya siri kwani vita hii
Kwani kikao na mkutano wa hadhara ni sawa??
 
Kuna siku CCM, CDM na ACT wataamka watajikuta wapo out of touch na wananchi.

Hawa vijana chini ya 30 watakuja kubadilisha siasa za hii nchi.
Vijana wajinga wajinga hata siasa hawazijui wao mkombozi wa nchi ni mheshimiwa Hayati John Pombe Magufuri.
 
Mkutano mkubwa kuongelea siasa eti maelewano wakati nchi ina hali ngumu

Hawajadili kutuvusha bali wanawaza matumbo yao tu
Hapo wanaahidiwa hela tu hakuna jipya
Unafanya siri kwani vita hii
Katiba mpya ni muhimu sababu matatizo tunayoyapitia kama Nchi, maji, mafuta, mfumuko wa Bei nk nk ni ya KIMFUMO hivyo ikiandikwa na kupatikana, itatibu hayo yote.
 
Kinana atakuwa anawafundisha siasa...waachane na harakati za mahakamani..wajue siasa..
Wajue Ku compromise madogo ili wapate makubwa...
Siasa sio kushinda Kesi mahakamani

Please acha kuongopa, mahakamani kaenda Nani Kama sio akina Mdee ndio waliofungua kesi mahakamani?. Acha kupotosha. Halafu kinana amfundishe Nani siaasa. Huyu aliyerekodiwa akimsema vibaya Mwenyekiti wake wa chama mpaka kusimamishwa uananchama.
 
KUBWA NI AMANI NA UPENDO KWA WATANZZANIA KUPINGANA NA UFISADI,UONEVU NA KUMALIZA KADHIA ZA MAJI NA UMME ONCE AND FOR ALL BADALA YA KUWA NA ZIMA MOTO TATIZO LINAPOTOKEA...
1.Tuwe na vyanzo vya maji vya kudumu
2.Taratibu nzuri na za wazi kwa mikataba mbalimbali ziheshimiwe
3.Swala la mafuta liangaliwe upya hasa BULK PROCUREMENT kuns issue kubwa ya kufnya bei z mafuta kuwa juu sana wakati tungefanya opren market bei ingekuwa nzuri mno na tukawa na NATIONAL RESERVE ya kutosha
 
Na tunasikia 4 t zimekopwa ndani ya wiki! Mtaani kuna mgao wa umeme, hakuna maji, hakuna dawa, .... Shida za kihistoria.
Hivyo vikao vyao havina manufaa kwa maisha ya mtanzania wa kawaida.

Ugumu wa maisha uko pale pale.
 
KWAO NI KUBORESHA MAZINGIRA YA SIASA.. SIO MAISHA YA MTANZANIA...

LILE SWALI MLIKUWA MNAULIZA WALE AKINA ZITO NA MBOWE MBONA KIMYA... HILI NDILO JIBU...

MAGUFULI ALIWANYIMA MAZINGIRA YA KUFANYA SIASA NA KULA PESA ZA BURE... SAMIA KAWAPA..

Magufuli hakuwanyima mazingira ya kufanya siasa, Bali aliogopa kufunikwa na CHADEMA maana show ya 2015 haikuwa ndogo, ndio maanampakaufa ni hao CHADEMA ndio walipiga kelele kwamba rais kafa.
 
Naamini viongozi wangu wa CCM lazima wamewafunda na kuwafundisha masuala ya kiuongozi ya kuwa na vifua na kuwa Wasiri wakati vikao vinaendelea, Bila Shaka lazima semina ilitangulia ya kuwapa viongozi wa chadema ili wajuwe umuhimu wa wao kushiriki katika vikao hivyo na Nini kinapaswa kufanyika wakati mazungumzo yanaendelea ndio maana unaona viongozi wa chadema wamegoma kusema kilichozungumzwa maana wameshalishwa madini toka CCM ya namna ya kuwa na subiri ya midomo yao,

Hicho ndicho huwa naandikaga humu kuwa kiongozi unapaswa kuwa na kifua ,Mtulivu,Busara,Subira na hekima, kujuwa wakati gani uongee na wakati gani ukae kimya, siyo kupelekeshwa tu na mihemuko ya vijana wao wanaowaka Kama Moto wa petroli, Naamini Nguli wa Siasa ndugu Kinana amefanya kazi kubwa ya kuwaelimisha viongozi wa Chadema ndio sababu ya kuona wamebadilika kitabia na kuwa Wasiri

Nawapongeza katika hili na waendelee hivi hivi mpaka mwisho wa mazungumzo yao, wawe wenye Subira,hekima,busara,utulivu na kujuwa umuhimu wa usiri wakati mazungumzo yanaendelea, siyo kukimbia tu kuripoti mambo ambayo hayapaswi kuripotiwa au kutolewa hadharani wakati bado hawajafika mwisho wa mazungumzo, lazima wajuwe hata mwisho wa mazungumzo Ni Nani atapaswa kuzungumza kwa kila upande hasa chadema maana kwa CCM hakuna shida maana ndio chama kiongozi kinachojuwa utaratibu unaopaswa kuwepo na kufuatwa

Kiukweli Mimi Lucas Mwashambwa Najivunia Sana kuwa mwanachama wa CCM, kwa kuwa hiki Ni chama kilichokomaa kisiasa, chenye hadhina ya viongozi katika kila idara ,CCM Ni chuo Cha uongozi na mahali pekee ambapo wanachama wote tuna nafasi sawa ,hakuna ubaguzi Wala unyanyasaji ndani ya CCM,

Kazi iendeleee
 
Back
Top Bottom