Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 21,470
- 40,593
Hili wameshasahau tayari.Ogopa sana CDM chama kilichokataa ruzuku ya dhuluma wakati ambao chama kina uhitaji mkubwa wa pesa.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hili wameshasahau tayari.Ogopa sana CDM chama kilichokataa ruzuku ya dhuluma wakati ambao chama kina uhitaji mkubwa wa pesa.
Kwani CHADEMA ndio wameshitaki mahakamani? au mahakama gani unaongelea?Kinana atakuwa anawafundisha siasa...waachane na harakati za mahakamani..wajue siasa..
Wajue Ku compromise madogo ili wapate makubwa...
Siasa sio kushinda Kesi mahakamani
My point is kwa nini chadema tu na sio vyama vingine?Ulitaka wafanyaje?? Njia aliyokuwa anatumia mwendazake haijaleta matunda yoyote yale. Umesahau enzi zile walivyotaka kumteka Msigwa akitokea Gereza la Segerea??
Kwa nini viwe vyama vingine na si CHADEMA??My point is kwa nini chadema tu na sio vyama vingine?
Kuna siku CCM, CDM na ACT wataamka watajikuta wapo out of touch na wananchi.
Hawa vijana chini ya 30 watakuja kubadilisha siasa za hii nchi.
Ajabu kabisa. Yaani kuna watu hawaiamini wala kuipenda CCM, lakini pia wana wivu kwamba CHADEMA iko tofauti na CCM.Hawa watoto wanaoshindia habari za Diamond na kondeboy?
HONGERA KWA MAJADILIANO MUNGU AYASIMAMIE YAPATE MUAFAKANini kinaendelea? Hili ni swali linalogonga vichwa vya Watanzania wengi wenye shauku ya kujua majadiliano baina ya viongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), yatahitimishwa lini.
Jana vigogo wa vyama hivyo wasiozidi 15 walijifungia kwa saa nne katika Hoteli ya Courtyard jijini hapa, kuendeleza majadiliano yaliyoanza miezi sita nyuma.
Majadiliano ya kwanza yalifanyika Ikulu ya Chamwino, Dodoma, Mei 20 mwaka huu kwa Rais Samia Suluhu Hassan akiambatana na viongozi waandamizi wa CCM na Serikali, ambao walikutana na ujumbe wa viongozi wa CHADEMA, ulioongozwa na Mwenyekiti wao, Freeman Mbowe.
======================
Tangu wakati huo, inaelezwa timu za viongozi wa vyama hivyo vyenye wanachama na wafuasi wengi nchini, zimekuwa zikikutana kwa siri kubwa katika majadiliano ambayo yamekuwa na lengo la kuboresha mazingira ya kisiasa nchini.
Usiri wa vikao hivyo umekuwa ukitawala pande zote na taarifa zao zimekuwa zikifunikwa na zile za kikosi kazi kilichokuwa na jukumu la kupitia maoni ya wadau wa demokrasia ambacho ripoti yake ikiwa na masuala mbalimbali, imekabidhiwa hivi karibuni kwa Rais Samia.
Jana, vigogo wa CCM wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti-Bara, Abdulrahman Kinana na upande wa Chadema, ukiongozwa na Mbowe waliongoza wajumbe wao kujifungia katika kikao hicho cha siri.
Kikao hicho, kilianza saa sita adhuhuri mchana na kukamilika 10:06 jioni katika hoteli hiyo.
Awali, kabla ya kuanza kwa kikao hicho, viongozi wa CCM walikuwa wa kwanza kuwasili wakiongozwa na aliyewahi kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Andrew Chenge aliyewasili saa 5:14 asubuhi.
Saa 5:17 alifika Naibu Katibu Mkuu wa zamani wa CCM-Zanzibar, Vuai Ali Vuai akiwa na baadhi ya viongozi wengine waandamizi wa chama hicho.
Gazeti hili lililokuwa limeweka kambi katika hoteli hiyo, lilimshuhudia Mbowe akiwasili saa 5:46 asubuhi akipishana dakika 11 na Kinana aliyefika saa 5:55 na wote walipoingia walikwenda moja kwa moja kwenye ukumbi wa Welington ambako kikao hicho kilifanyika.
Baada ya vigogo hao kuingia, saa 5:59 na saa 6:02 mchana, waliingia Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika na John Heche mtawalia. Heche ni mjumbe wa kamati kuu ya chama hicho.
Saa 6:07 mchana, wanasheria wa Chadema, Jeremiah Mtobesya na Jonathan Mdeme nao waliingia katika kikao hicho.
“Huu ni mwendelezo wa vikao vyetu, ni nini kimejadiliwa, subirini muda ukifika mtaambiwa,” alieleza mmoja wa wajumbe wa kikao hicho, ambaye hakutaka kuzungumza kwa undani.
Hata hivyo, taarifa ambazo gazeti hili linazo ni kwamba, majadiliano hayo yamefikia hatua nzuri na yatakapokamilika yatawekwa hadharani.
“Watu walijua baada ya kikosi kazi haya majadiliano hayapo, la hasha! Yanaendelea kama kawaida na sasa yapo hatua nzuri.”
“Mwisho Watanzania wataelezwa nini kinaendelea na bila shaka tutafanya mkutano na waandishi kwa pamoja,” alieleza kiongozi mmoja wa CCM ambaye si miongoni mwa wajumbe wa kamati hiyo.
“Mama kama alivyoahidi, anaendesha nchi kwa 4R, akiamini hiyo ndiyo njia ya kuwaleta wananchi pamoja. Nchi ni yetu sote na kila mmoja ana wajibu wa kuijenga.”
4R hizo ni (Reconcilation - maridhiano, Resiliency - ustahamilivu, Reforms -mabadiliko na Rebuilding - kujenga upya) ambazo alizielezea katika makala yake maalum aliyoandika kuadhimisha miaka 30 tangu kurejea kwa mfumo wa vyama vingi vya siasa nchini.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Shaka Hamud Shaka alipoulizwa na gazeti hili alisema hana uhakika kama kuna kikao hicho kwani, yeye si mjumbe wa vikao hivyo.
“ Lakini ninachojua kama wamekutana ni mwendelezo wa majadiliano na kama kimefanyika muda ukifika tutawajulisha.”
Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika alipoulizwa kuhusu kikao hicho hakuwa tayari kufafanua chochote zaidi ya kusema: “Aliyekwambia kuwa kuna kikao kimefanyika, atakuwa na uwezo wa kukueleza zaidi. Asante.”
Baada ya kumalizika kwa kikao hicho, waliokuwa wa kwanza kutoka ndani ya ukumbi ni Mbowe na ujumbe wake ikiwa ni saa 10 jioni kisha wakafuatia Kinana na wenzake. Wakati wote wa kikao hicho ukiendelea, hali ya ulinzi ilikuwa wa kawaida na shughuli nyingine zilikuwa zikiendelea kama kawaida, huku magari ya viongozi hao yakijazana eneo la mapokezi.
MWANANCHI
Mkuu 2025 utakuwa kwenye kinyanganyiro?CHADEMA kimekuwa ni chama NDOIGE. Ukikipenda ndiyo umekipenda na ukikichukia ndiyo umekipenda pia!!
Inshaalah!!Mkuu 2025 utakuwa kwenye kinyanganyiro?
Hawahawa wengi wao wanaishi kwa shemeji zao? Haitawahi tokea believe meKuna siku CCM, CDM na ACT wataamka watajikuta wapo out of touch na wananchi.
Hawa vijana chini ya 30 watakuja kubadilisha siasa za hii nchi.
Jambo lipi dogo la ku compromise na lipi kubwa watalipata?Kinana atakuwa anawafundisha siasa...waachane na harakati za mahakamani..wajue siasa..
Wajue Ku compromise madogo ili wapate makubwa...
Siasa sio kushinda Kesi mahakamani
Sasa nani kashitaki ?Hii ya wabunge 19 wameshtakiwa?
Kizazi cha hivyo hakipo.Kuna siku CCM, CDM na ACT wataamka watajikuta wapo out of touch na wananchi.
Hawa vijana chini ya 30 watakuja kubadilisha siasa za hii nchi.
Sie tangu mwanzo hatufungamani, hata Israel Juzi waligoma kupeleka majeshi Ukraine.Je ni kwasababu hatukuchagua upande!!?
Kule wanakopigana!?
Mtu wa vita huyo karudi.View attachment 2407469
Bibi comes back to power, coincidence? I don't think so..
Ila chama tawala kipo!!??Hakuna upinzani Tanzania.
Vyama vingine si vimechagua upande ule wa kikosi kaziMy point is kwa nini chadema tu na sio vyama vingine?