Kinana: Tusipendeleane, tusibebane

Kinana: Tusipendeleane, tusibebane

Simba mnyama

JF-Expert Member
Joined
Jul 14, 2012
Posts
348
Reaction score
129
Ule usemi wa "nyani haoni kundule" umedhihirika pale Katibu Mkuu wa CCM, Abdallahaman Kinana alipowachana wanachama wa CCM katika mkutano alioufanya hapo jana mjini Kigoma kwa kuwaambia wanachama wa chama hicho waache kupendeleana wala kubebana kwani kwa kufanya hivyo tutazalisha makundi mengi ndani ya chama hicho, kitu ambacho sio afya kwa chama na pia kwa kufanya hivyo kunaweza kuchangia kuchukiwa kwa chama na kupelekea upinzani kupata nguvu!

Kinana anasahau kuwa ndani ya chama hicho (hasa ngazi ya juu) wamekuwa wakibebana na kupendeleana hasa pale ambapo kumekuwa kukifanyika madudu ya kukichafua na kukipaka matope chama. Rejea orodha ya mafisadi iliyotajwa na CCM, Rejea orodha ya mawaziri mizigo iliyotajwa na Kinana mwenyewe, n.k. Ni hatua gani madhubuti zilizochukuliwa na chama kwa watu hao? Huko sio kubebana? Huko sio kupendeleana?

Kauli hii ya Kinana ya "Tusipendeleane, Tusibebane" inaonesha kana kwamba CCM inatufanyia usanii.
 
Katika ziara yote anayozurura huyu Kinana anaendelea kutoa ahadi za uongo kwa wananchi, "anasema nimeshaongea na Magufuli kuanzia wiki ijayo mkandarasi atakuja kuanza kazi"
 
Nadhani amechelewa kusema na amesemea mahali pasipostahili,angeanzia kwenye viongozi wenzake kwa kuwaambia waache kuwabeba vijana wao au vijana wa viongozi wenzao na waache wananchi wafanye uamuzi vinginevyo tunatengeneza taifa lenye pepo kwa wachache na wengi kiama.
 
Katika ziara yote anayozurura huyu Kinana anaendelea kutoa ahadi za uongo kwa wananchi, "anasema nimeshaongea na Magufuli kuanzia wiki ijayo mkandarasi atakuja kuanza kazi"
utatawalaje nchi bila kutumia urongo?
 
mbona wanabebana wao napia yy anabebwa?kwnye ishu ya tembo?
 
mbona wanabebana wao napia yy anabebwa?kwnye ishu ya tembo?

MSIGWA alidai ana ushaidi ndani ya BUNGE,KINANA Jangili alipoburuzwa na KINANA Mahakamani akadai kesi ifutwe yeye anakinga ya KIBUNGE.CDM walaghai,WANDISHI HABARI na WASOMI wamewastukia.
 
Kama yeye hapendi kubebana,mbona meli yake iliyoshiriki ujangili haijakamatwa kama sio kulindana??
 
Kama yeye hapendi kubebana,mbona meli yake iliyoshiriki ujangili haijakamatwa kama sio kulindana??

Kamuulize Msigwa kwanini aliamua kukataa kwende mahakamani na kutumia kinga ya bunge
 
Wewe tatizo lako nini mkuu amesema wasibebane kama walikuwa wanafanya hivyo kawaambia waache shida yako sasa nini.
 
Kama yeye hapendi kubebana,mbona meli yake iliyoshiriki ujangili haijakamatwa kama sio kulindana??
Msigwa anayo majibu yako mpigie anamjua vema kinana amebaki mdogo kama njiwa kwa kumhofia kinana.
 
Kubebana imekua tabia ya watawala siku hizi,mtu anavurunda hapa anapelekwa pale,kutoa mfumo huu ni jambo zito,linahitaji uwe na moyo mkubwa kama wa mwenda-wazimu
 
unanitisha mkuu!!! Msigwa anamhofia Kinana??? Basi mwambie huyo Kinana nipo chini ya miguu yake,asije kunipumzisha mapema hii mkuu.
Nilikuwa natania tuu jamani,Kinana hana hata mashua sembuse meli? Katibu mkuu wa ccm ni mtu msafi nje na ndani ila watu wanamwonea wivu tuu.
Mkuu mjempo nafikiri hapo niko sawa sana,Ngoja nitampigia Msigwa nimwambie asirudie tena.
hahahahahahahaha!!Mjepo??/
 
Dubai - DP WORLD waanza kuchanganya watu huku..

Hebu mtazame na msikilize mwenyewe.

Bila shaka Mungu wetu amesikia maombi yetu

Mnara wa Babeli unaanza kuanguka. Tuendelee kuombea anguko kamili (total & complete fall) la utawala huu wenye roho ya kishetani chini ya CCM
 
Back
Top Bottom