Simba mnyama
JF-Expert Member
- Jul 14, 2012
- 348
- 129
Ule usemi wa "nyani haoni kundule" umedhihirika pale Katibu Mkuu wa CCM, Abdallahaman Kinana alipowachana wanachama wa CCM katika mkutano alioufanya hapo jana mjini Kigoma kwa kuwaambia wanachama wa chama hicho waache kupendeleana wala kubebana kwani kwa kufanya hivyo tutazalisha makundi mengi ndani ya chama hicho, kitu ambacho sio afya kwa chama na pia kwa kufanya hivyo kunaweza kuchangia kuchukiwa kwa chama na kupelekea upinzani kupata nguvu!
Kinana anasahau kuwa ndani ya chama hicho (hasa ngazi ya juu) wamekuwa wakibebana na kupendeleana hasa pale ambapo kumekuwa kukifanyika madudu ya kukichafua na kukipaka matope chama. Rejea orodha ya mafisadi iliyotajwa na CCM, Rejea orodha ya mawaziri mizigo iliyotajwa na Kinana mwenyewe, n.k. Ni hatua gani madhubuti zilizochukuliwa na chama kwa watu hao? Huko sio kubebana? Huko sio kupendeleana?
Kauli hii ya Kinana ya "Tusipendeleane, Tusibebane" inaonesha kana kwamba CCM inatufanyia usanii.