Tetesi: Kinara wa kukwamisha Rais Magufuli asiwe Mwenyekiti wa CCM ni Rajab Luhwavi, NKM CCM Bara

Tetesi: Kinara wa kukwamisha Rais Magufuli asiwe Mwenyekiti wa CCM ni Rajab Luhwavi, NKM CCM Bara

Status
Not open for further replies.
sasa wamekuacha nin wewe mchonganishi na mvunja amani ya Tanzania, haya maneno hayafai kabisa nchini kwetu tuna amani na utulivu. si ungeenda ukaongee naye na wana ccm wote yaishe acha uchonganishi SIRRO mtu huyu asiachwe, TCRA mtu huyu anavunja utratibu weeetu
 
Huyu Luhavi zake sasa zimefika bora amejulikana mapema pesa zote alizoiba lazima zirudi mahakama ya mafisadi inamsubiri lazima asurubiwe.
 
Huyu Luhavi zake sasa zimefika bora amejulikana mapema pesa zote alizoiba lazima zirudi mahakama ya mafisadi inamsubiri lazima asurubiwe.
Luhwavi kwa Magufuli hatoboi hata kidogo
 
Naona mawakala wa mafisadi mnaweweseka sasa
sasa wamekuacha nin wewe mchonganishi na mvunja amani ya Tanzania, haya maneno hayafai kabisa nchini kwetu tuna amani na utulivu. si ungeenda ukaongee naye na wana ccm wote yaishe acha uchonganishi SIRRO mtu huyu asiachwe, TCRA mtu huyu anavunja utratibu weeetu
 
View attachment 365938
N.K/Mkuu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi
Wadau amani iwe kwenu,

Hivi karibuni, tumeshuhudia harakati kadhaa za baadhi ya wanasiasa wa ndani na nje ya CCM wakipaza sauti zao kutaka Rais Magufuli asiwe Mwenyekiti wa Chama hicho ili kumrithi Dr Jakaya Kikwete ambaye anatarajiwa kustaafu rasmi wadhifa huo Julai 23.

Awali kulikuwa na figisu figisu nyingi kuwa chama hakina fedha za kuendeshea Mkutano Mkuu ili tu lengo lao litimie. Thanks kwa jitihada zilizofanywa na Katibu Mkuu Abdulrahman Kinana na Makamu Mwenyekiti Bara Philip Mangula ambao wamehakikisha kuwa fedha zinapatikana na mkutano Mkuu unafanyika Julai 23.

Hata hivyo, tunapoelekea Julai 23, yapo Mambo kadhaa yanaendelea ndani ya CCM ambayo kwa hakika yanaweza kuvuruga utamaduni ambao imejiwekea wa kukabidhiana madaraka ya Uenyekiti pindi Rais anapomaliza muda wake. This time, zipo harakati za chini kwa chini zinazoendeshwa ili Kikwete aendelee kuwa Mwenyekiti na Magufuli abaki kwenye cheo cha Urais tu.

Binafsi baada ya kuona kuwa vuguvugu hilo linazidi, ikabidi niingie chimbo ili kumnasa anayeinjinia mkakati huo. Hakika nilichokibaini kinanishtua sana. Mchawi sasa kajulikana. Ni Rajab Luhwavi, Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara ambaye ametwaa madaraka hayo tarehe 9 Julai 2015 mara Baada ya Mwigulu Nchemba kujiuzulu nafasi hiyo wakati wa mchakato wa kumpata Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM. Mtakumbuka kuwa Luhwavi alikuwa Msaidizi wa Rais kwenye Masuala ya Siasa kabla ya nafasi hiyo kumuachia Martin Shigela Julai 2015.

Hoja za Luhwavi kutaka Magufuli asiwe Mwenyekiti wa CCM ni za kitoto sana. kwamba, Magufuli hakijui chama na hivyo yeye pamoja na genge lake wanaamini kuwa atakiharibu badala ya kukiimarisha. Hofu yao imeongezeka hasa kutokana na (kwa mtazamo wao) teuzi alizofanya Rais mpaka sasa kutozingatia kigezo cha Ukada wa CCM.

Hofu nyingine ya Luhwavi ni kupoteza madaraka ndani ya CCM. Luhwavi anaamini kuwa ikiwa Magufuli atakuwa Mwenyekiti wa CCM, hatakuwa na wadhifa wowote ndani ya chama na kwamba hata hiyo nafasi ya Unaibu Katibu Mkuu ataipoteza.

Pia Luhwavi ana hofu kubwa ya kufikishwa Mahakamani kutokana na kufuja fedha nyingi zilizotengwa wakati wa kampeni. Inaelezwa kuwa Luhwavi alikihujumu chama kwa kupeleka fedha kidogo kwenye majimbo ya uchaguzi tofauti na ilivyoidhinishwa na chama. Inadaiwa kuwa kwa baadhi ya mikoa, fedha hizo hazikwenda kabisa na hivyo kufanya baadhi ya wagombea kujigharamia hali iliyochangia kushindwa kwao.

Nani anampendekeza Luhwavi awe Mwenyekiti wa CCM? Hili lipo dhahiri. Luhwavi anataka Jakaya Kikwete aendelee kwenye wadhifa huo. Matarajio ya Luhwavi ni kwamba, ikiwa Kikwete ataendelea kuwa Mwenyekiti wa CCM, atamteua yeye (Luhwavi) kuwa Katibu Mkuu kujaza nafasi ya Katibu Mkuu wa sasa Abdulrahman Kinana ambaye ametangaza kuachia nafasi hiyo baada ya Mkutano Mkuu wa Julai 23.

Mpaka sasa, Luhwavi amezunguka kwenye mikoa kadhaa ya Tanzania Bara kuhamasisha wajumbe wa Mkutano Mkuu wasiridhie hoja ya Magufuli kuwa Mwenyekiti wa CCM. Inasemekana kuwa mpunga wa kutosha umetembea kwa wajumbe wa Mkutano Mkuu ili wamkwamishe Rais Magufuli.

Hata hivyo, inaonekana dhahiri sasa kuwa mkakati wa Luhwavi na Timu yake umegonga mwamba. Mwenyekiti wa sasa Jakaya Kikwete amesema hataongeza hata sekunde moja na kwamba dhamira yake ya kwenda kulala usingizi baada ya Magufuli kushinda Urais iko pale pale. Hana mashaka hata kidogo na Rais na anawabeza wale wanaodhani kuwa Magufuli hana uzoefu wa kutosha kuongoza chama. Kwamba, kama amechaguliwa kuwa Rais wa nchi, atashindwaje kuongoza chama?

Nani walio nyuma ya harakati hizo? Nitaendelea kuwajuza kwa kadri tunavyokaribia Julai 23. Stay with me. Niwapongeze tu na kuwatia moyo baadhi ya wajumbe wa Mkutano Mkuu wa mikoa ya Njombe, Iringa, Dar es Salaam, Tanga, Manyara, Kilimanjaro, Mbeya na Dodoma ambao wamenipa ushirikiano wa kutosha wakati ninafuatilia jambo hili mpaka mchawi amejulikana. Mikoa hii ni miongoni mwa mikoa ambayo Luhwavi alitembelea kufanikisha mkakati wake.
UNAFIKI UNA TABIA MBAYA SANA SASA NAONA MWAANZA TAFUTANA LAZIMA MUUWANE SI MMEBAKI WENYEWE KAZI IPI
 
Luhwavi kwa Magufuli hatoboi hata kidogo

Wewe unasemaje? Kwamba Naibu Katibu mkuu wa chama Taifa hatoboi kwa mwanachama wa kawaida ambaye hana nafasi hata ya mwenyekiti wa kitongoji? Hapa ushindani si ni ndani ya chama?
Au unatudhibitishia kuwa kwenu serikali mnayoiunda mdiyo ina nguvu kuliko chama katika mambo ya chama? Hii statement yako ni ya aibu sana kama mwanachama. Au ndio sababu hata kwenye kikao cha Kamati kuu kule Dodoma Magu akamtuma Naibu spika kuhudhuria eti anamwakilisha Spika wakati utaratibu huo haupo na kina Kinana wakabaki kununa tuu?
 
Naona mawakala wa mafisadi mnaweweseka sasa
nyie ssm mlisema Gwajima afungiwe kanisa hafai yule leo yako wapi? unataka kutuaminisha kwamba Gwajima ni nabii hadi ulete tetesi hapa au na wewe umeota kama ASKOFU?
 
Fomu za kugombea uenyekiti zitatolewa lini ? Katiba ya CCM mbona inasiginwa ?
 
kwenye kundi la kondoo weusi akitokea mweupe bado ataitwa kondo na ukiwa mbali hutomtambua ssm ni umoja wa kondoo weusi mweupe mmoja hana madhara kweenu
 
Ni muda mwafaka kwa JPM kuweka mguu mmoja CCM na mwingine nje!!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom