Katiba Mpya inataka Rais apunguziwe madaraka ya kuteua. Sawa lakini mfumo wa watu kuingia holela katika idara hata wasipoweza kufanya kazi (siyo wasizoziweza-tofautisha hapa) ni hatari.
(Mfano mwepesi ni kumpa Mchaga ajira huria namna hiyo, nchi itaingizwa biashara na mwenendo usio na mwelekeo sahihi kama ukabila, wizi wa fedha na hata maangamizi ya makabila mengine. Siyo kuwa mchaga hawezi kazi bali akiipata anafanya mambo mengine yenye madhara kwa raia wengine (sasa hivi nimenunua butter ya karanga kutoka Super Market ya Mchaga amefungua makopo yale na kuongezea madawa ya kupoteza fahamu)).
Kasoro iko katika namna Rais anavyochaguliwa na kinga anazopewa. Rais anachaguliwa na wananchi halafu katika ndoto za ujinga wote wananchi wanashangilia kuwa wana demokrasia ya kuchagua mpaka Rais wao.Lakini Rais huyo huyo akishaingia Ikulu anakuwa kama Mungu-Mtu, wananchi waliomchagua hawawezi kumfukuza na hashauriwi na yeyote katika kazi zake isipokuwa akina-Rweyemamu. Na kama Bunge likijazwa mahela ya kwenda mpaka Dubai kukutanisha wapendanao basi hata ukasirike namna gani kuhusu tabia ya Jakaya Ikulu unapoteza wakati wako. Sana sana ukionyesha wazi chuki zako kwa Jakaya unajipalia makaa utaishia kama Ulimboka au Kibanda.
Mahela yamejaa Uswiss lakini Rais hata aibe na wewe ukapata data zote huna chombo cha kumsikiliza raia wa kawaida kuhusu tabia ya wizi wa Rais. Mahakama yote anateua yeye, na Jaji Kiongozi ni Mstaafu aliyepewa Ruzuku na Rais huyo huyo kurudi kazini.Ukifungua madai Jaji Kiongozi anakubana, jinai huwezi kwa sababu Rais hashitakiwi kwa jinai, na Yeye Rais ndiyo Mwendesha Mashitaka Mkuu wa jinai, ndiyo anamteua DPP.
Hivyo -------- yeyote akishapata kura za wananchi kuwa Rais kaula na hana kikwazo mpaka miaka mitano ipite. Wakati wa kutoa mapendekezo kuhusu Katiba Mpya mimi niliwahi kupendekeza kwenye mtandao wa Tume husika kuwa:
!.Kuwe na utaratibu Rais kufukuzwa na wale waliomchagua. Sheria zote za ajira nchini zinasema hivyo, kila mwajiriwa atafukuzwa na mamlaka iliyomwajiri.
2. Rais asitokane na Chama cha Siasa kwa sababu majukumu yake ni ya Kitaifa siyo ya kisiasa wala kimkoa. Hivyo Rais achaguliwe na ushirika wa nyanja zote zinazounganisha wana siasa wote na asasi zote zinazoweka mskumo katika nchi. Tukishindwa kueleka huko basi Rais achaguliwe na Bunge kama ambavyo anafukuzwa na Bunge.
3. Rais anapokurupuka kwa wiki mbili kwenda kuomba kura kwa watu wasiomjua kuna hatari ya Rais huyo huyo kurudi huko akigawa pesa za walipakodi kwa wakulima wa korosho kama shukrani kwa kumsaidia kuingia Ikulu.
4.Utawala wa ki-Demokrasia ndiyo unaotokana na wananchi moja kwa moja na hapa wananchi ndiyo wanaweza kuonyesha tofauti kati ya ubora wa mawazo yao. Hata ndani ya nyumba tofauti za kimawazo zipo lakini baba huwa hazitakiwi kumfanya mbaguzi. wote ni watoto na huyo ni Mama yao. Na mtoto mmoja akimpenda kaka yake na mama yake na kumchukia HUYO ZURIAT haina noma, nyumba itadumu tu. Hivyo watawala wa kisiasa ndiyo wachaguliwe na wananchi. Na hapa ilitosha kabisa Mmasai kuchagua Mbunge wake Monduli kwa sababu anamjua, siyo mkazi wa Mpanda kumchagua mtu wa Kilosa aliyepita siku moja tu akijinadi kwake, ni urongo huo. Waziri Mkuu akitokana na Chama Chenye Majority Bungeni ndiyo utaratibu unaotumika na kwingine. Waziri Mkuu wa namna hiyo atakuwa makini kuhakikisha Chama chake hakiingii migogoro ya uchumi na raia kwa ujumla kwa sababu chama kitapoteza umaarufu.
5. Raia wamshitaki Rais mahakamani na Mahakama iwe na uwezo wa kumpa mdai hukumu dhidi ya Rais, halafu hukumu hiyo apewe Spika wa Bunge kwa ajili ya kuona hukumu inatekelezwa kwa kiwango cha hata kumwondoa Rais madarakani. Hapo Rais atawaheshimu hata raia wa nchi yake.
Mkiendelea na utaratibu wenu wa sasa itakuwa Rais anateua Mawaziri halafu wahuni na mafisadi waliomweka Rais madarakani wanaharibu na waziri husika anajiuzulu halafu Rais anateua Mawaziri wengine. Huo ndiyo huitwa mzunguko wa umaskini.