Kinga kwa Rais aliyeko madarakani na wastaafu ni kichocheo cha uvunjaji haki, Iangaliwe upya

Kinga kwa Rais aliyeko madarakani na wastaafu ni kichocheo cha uvunjaji haki, Iangaliwe upya

Tanroard wamebomoa nyumba za wakazi wa kimara wakati kuna zuio la mahakama,hii ni zarauuuuu kubwa sana kwa mahakama zetu,chombo cha serekali kukataa kutii na kutekeleza amri halali ya mahakama nashindwa hata kuelezea,na kuamini kama kweli
Umejiridhisha kuwa nyumba zilizobomolewa zina zuio au unafuata mkumbo wa magazetini tu
Mh sumaye waziri mkuu mstaafu wa jamhuri ya muungano wa tanzania mashamba yake yana zuio la mahakama,lkn amenyanganywa mashamba yake kukiwa kuna amri halali ya zuio la mahakama,hivi ni mifano gani watanzania wanataka kupewa ili wajue mahakama yetu imedharaulika
Rudia maamuzi ya rufaa ya kesi ya mbunge wa arusha mjini,majaji walisema serekali inanajisi sheria
Ushawahi kuona hata mfano wa zuio la mahakama?unajua kuwa lina muda maalum
Ningekushauri ungejielekeza kwenye kesi husika ukapata data za kina kabla ya kufungua thread na kulaumu kinga ya Rais huku ukisahau kuwa ardhi ni mali ya serikali wewe unakodishwa tu.Kasome sheria ya ardhi dada utapata uelewa mpana
 
ikiwa aridhi ni mali ya serikali kwa nini ikikutwa mmea wa bangi serikali hukana umiliki wake ?
 
Ukumbuke pia mahakamani ndio kunaongoza kwa rushwa ikifuatiwa na polisi, usishangae kuona inapuuzwa na serikali ata na wananchi wa kawaida. Kwa nakupa mfano mmoja. ivi karibuni mahakama imeamuru kulipwa kwa mabilioni ya fedha kwa kampuni iliotengeza ARV feki. Na mkuu amesema ivo pesa halipi je hapa utasemaje wapewe au wanyimwe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mleta mada umetuelimisha jambo nzuri.. lakini kinga ya rais huwa iko kwenye katiba ya nchi kama sikosei.. kama ndio nafikiri huyu mkulu wa sasa hivi hiyo kinga haina ulazima kwake kwa sababu nchi anaendesha kwa kauli zake siyo kutokana na katiba ya nchi

counter attack siyo mbaya akistaafu
 
Nanukuu"nakulipa mshahara harafu unitukane???"mwisho wa kunukuu.
Waliopo kwenye mihimili mingine wanalinda ugali wao,kwa sababu mhimili uliojichimbia zaid ndiyo uliwaweka hapo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
nchi hii Mtukufu amekua kila kitu, MAHAKAMA yeye, BUNGE yeye, SERIKALI yeye, Msemamaji mkuu YEYE.......Hivi tunaelekea wapi???akimaliza wa huku lazima atakufikia na wewe
tusikae kimyaa kukemea upuuzi huu
 
Huu wote ni upuuzi wa wabunge wenye akili ndogo kabisa kutoka CCM lakin wakwanza ni muasisi aliye liacha taifa likiwa na katiba ya kipuuzi kabisa
 
Ukumbuke pia mahakamani ndio kunaongoza kwa rushwa ikifuatiwa na polisi, usishangae kuona inapuuzwa na serikali ata na wananchi wa kawaida. Kwa nakupa mfano mmoja. ivi karibuni mahakama imeamuru kulipwa kwa mabilioni ya fedha kwa kampuni iliotengeza ARV feki. Na mkuu amesema ivo pesa halipi je hapa utasemaje wapewe au wanyimwe

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwanini serekali ikatae amri halali ya mahakama?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Katika nchi yetu kuna sheria za ajabu sana, mojawapo ni hii ya kumlinda Rais Mstaafu kutokana na makosa aliyoyafanya akiwa Rais. Habari juu ya Ufisadi uliofanyika katika awamu ya tatu ya Uongozi wa nchi yetu ni dira tosha ya kutufanya tufikirie upya juu ya Kinga ya Rais Mstaafu ya kutoshitakiwa.

Kashfa za kufanya biashara akiwa Ikulu, Wizi wa Mgodi wa Kiwira uliokuwa na thamani ya mabilioni ya shilingi kwa Mkapa-Yona kujiuzia kwa shilingi milioni 700 tu, Uundaji wa Kampuni za wizi na utapeli za Meremeta na Tangold, Wizi wa EPA BoT na Ujenzi wa Twin Towers za BoT, Ubinafsishaji wa NBC kwa Bei ya kutupa,Ununuzi wa Rada kwa bei ya kuruka, Ununuzi wa ndege ya Rais kwa gharama ya Watanzania "kula nyasi" na nyinginezo ni sababu za kutosha kabisa za kutufnaya Watanzania kupigania kuondolewa kwa sheria ya kinga inayomlinda Raisi mstaafu kutoshiotakiwa kwa wizi, ubadhirifu na Ufisadi aliofanya Rais Mstaafu wakati akiwa madarakani.

Sheria ya Kinga ni Msingi mkuu wa Ufisadi na Utawala wa hovyohovyo kwa gharama za Watanzania kama kashfa hizo nilizotaja hapo juu zilivyotugharimu Kiuchu na Kimaadili. Kuvuja kwa Habari za juzi kuhusu Utajiri wa Waziri Chenge kumiliki dola milioni moja katika akaunti nje ya nchi ni ushuhuda mwingine juu ya Sheria hii Fisadi ambayo inaweka misingi ya Wizi na Uhujumu wa mali ya Umma kwa hasara ya Wananchi wa Tanzania. Hebu tujiulize; Je, itawezekana kumshitaki Chenge aliyekuwa MWanasheria Mkuu wakati wa Mkapa bila kumgusa Mkapa (ambaye sheria inamkinga dhidi ya kushitakiwa?), Tunaweza kumshitaki Daniel Yona kwa kujiuzia Kiwira kwa bei ya bure bila kumshitaki Mkapa ambaye ni "Mjasiriamali" na Mbia mwenzake? KAtika haya mawili haiwezekani kutenda haki maana haiyumkiniki na ni vigumu sana kuwatia watu hawa hatiani (Yona na Chenge) na kumwachia huru Mkapa ambaye ama alishirikiana nao au alishindwa kuwajibika kwa Makusudi na kuwaachia "Wajasiriamali" na Mafisadi kama Chenge kujineemesha kupitia mikataba hewa na feki ambayo naamini kuwa Aliisaini kwa ahadi ambazo ndizo leo imemfanya Chenge kutuhumiwa kuwa na USD Milioni 1 kwenye akaunti zake nje ya nchi!

Kuondolewa kwa shria hii Fisadi, pia kutasaidia kupunguza idadi ya Wagombea urais ambayo wakati wa kinyam]ng'ang'anyioro cha kwenda kugombe Urasi huwa kunakuwa na orodha ndefu ya watu wanaotaka kuwa Marais maana wanajua fika kuwa wakipata nafasi hiyo Ufisadi wao hautakumbukwa milele. Hii itatusaidia kuwa na Wagombea safi na wnaojiamini kuwa ni Waadilifu na ni safi.

Wito wangu kwa Viongozi wa Dini, NGOs, Wananchi, Wabunge na Wanaharakati wengine ni kuwa wakati umefika wa Kushinikiza kufutwa kwa sheria FISADI inayomkinga Rais dhidi ya Rais Mstaafu. Tuanze sasa na ikiwezekana hata kutumia Mahakama ili sheria hiyo iondolewe haraka na kabla hatujapata Rais wa Awamu ya Tano.

Tukifanikiwa kuondoa sheria hiyo Fisadi, tuanze na Mkapa ambaye ndiye chimbuko, Founder na Pioneer wa Ufisadi tunaouona sasa na unaotula kama kansa Watanzania.
Likifanikiwa hili lazima limkute la yule wa Romania wakati ule
 
Kudharaulika kwa mahakama kunatokana na kinga ya rais,kinga ya rais kutokushitakiwa inachangia sana kudharaulika kwa mahakama
Nchini tanzania,sasa hivi mahakama imefanywa kama takataka,nitatoa mfano kudhibitisha tuhuma nilizozitoa kuhusu mahakama kufanywa takataka

Mfano (1)
Tanroard wamebomoa nyumba za wakazi wa kimara wakati kuna zuio la mahakama,hii ni zarauuuuu kubwa sana kwa mahakama zetu,chombo cha serekali kukataa kutii na kutekeleza amri halali ya mahakama nashindwa hata kuelezea,na kuamini kama kweli

Mfano (2)
Mh sumaye waziri mkuu mstaafu wa jamhuri ya muungano wa tanzania mashamba yake yana zuio la mahakama,lkn amenyanganywa mashamba yake kukiwa kuna amri halali ya zuio la mahakama,hivi ni mifano gani watanzania wanataka kupewa ili wajue mahakama yetu imedharaulika
Rudia maamuzi ya rufaa ya kesi ya mbunge wa arusha mjini,majaji walisema serekali inanajisi sheria

Wako wapi kina jaji warioba,wako wapi majaji wetu wastaafu,jaji Ramadhani,jaji barnaba samata,jaji bomani,na majaji wengine wastaafu?
Liko wapi baraza la maaskofu,liko wapi jukwaa la wakristu tanzania?

Sent using Jamii Forums mobile app
Wakati unakula huruhusiwi kuongea. Maintain table manners!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakuna Mtanzania yeyote anayestahili kuwa juu ya sheria pamoja na Rais wa Tanzania. Katiba yetu ina mapungufu mengi sana hata Mzee Warioba ameshatamka kwamba kuna umuhimu mkubwa wa kuandika katiba mpya. Na kwa maoni yangu hiki kipengele chenye kinga ya Rais kutoshtakiwa kwa yale aliyoyafanya alipikuwa Rais inabidi kiondolewe. Hatuwezi kuwa na Marais mafisadi kama Mkapa wanafanya biashara wakiwa Ikulu wanaiba rasilimali za Watanzania mchana kweupe, halafu wasifunguliwe mashtaka na kufilisiwa kwa ufisadi walioufanya walipokuwa madarakani.

Tunataka viongozi waadilifu ambao wanagombea nafasi za juu za uongozi ili kuwatumikia Watanzania kwa moyo mmoja, na siyo mafisadi ambao wanataka kutumia nyadhifa tulizowakabidhi kujitajirisha wao, familia zao, marafiki na jamaa zao.
swadakta mkuu .
 
Back
Top Bottom