Tundu Lissu au mbunge mwingine yoyote wa upinzani,nawashauri mpleke hoja binafsi Bungeni kutaka kinga ya Raisi iondolewe.
Nashauri muandae hoja yenye maelezo ya kutosha na yenye mifano ya kuthibitisha ni kwanini kinga hii ni lazima iondolewe na msisahau kutaja mfano wa mataifa makubwa ambayo viongozi wao hawana kinga.
Nasema hoja hii iwe na maelezo ya kutosha kwasababu moja tu.Najua hoja ya aina hii si rahisi kuruhusiwa hata kuingia tu Bungeni hivyo wakiisha ikataa nyie muisambaze mitandaoni ili wananchi waisome,waielewe na kisha wapime dhamira ya watu hawa katika hiki kinachoitwa "vita ya uchumi."
Tumieni nafasi zenu kama wabunge kuwaonyesha watanzania dhamira halisi ya viongozi tulioanao ili wasichotwe akili na hizi press conference za kila siku.
Tena nawashauri na nyinyi muitishe press conference na kuuleza umma nini kilichotokea iwapo hoja za aina hiyo zitakataliwa.
Wapinzani ni wakati wa nyinyi sasa kubadili mbinu za kuendesha siasa maana hawa wenzetu sasa wamebadili mbinu na nyie ndio watu pekee wa kuwasaidia na kuwafumbua macho watanzania.
Mnaweza pia kupeleka hoja ya kutaka mikataba ya Bombadier,ununuzi wa radar,ujenzi wa Airport Chato,n.k viwasilishwe Bungeni.
Nyie mjifanye kama wajinga kupeleka hoja hizo Bungeni na zikikataliwa wananchi wenyewe watapima.
Tuachane na mbinu ya kutegemea tu mikutano ya kisiasa bali ni wakati wa nyie sasa kukutana na kubuni mbinu mpya na kuweka mikakati ya namna ya kuendesha shughuli zenu za kisiasa.