Kinga kwa Rais aliyeko madarakani na wastaafu ni kichocheo cha uvunjaji haki, Iangaliwe upya

Kinga kwa Rais aliyeko madarakani na wastaafu ni kichocheo cha uvunjaji haki, Iangaliwe upya

..haki tusipoondoa hii kinga ya rais tutaendelea kuliwa mpaka...kila rais atakuwa anakuja anatuvuna anaondoka...tunahitaji amendments za katiba ama katiba mpya kuondoa hii kinga na pia kuwa na provision ya kupeleka wizi wa kura za rais mahakamani... Haki hatuponi kwa katiba Na ccm tuliyonayo...
 
Tundu Lissu au mbunge mwingine yoyote wa upinzani,nawashauri mpleke hoja binafsi Bungeni kutaka kinga ya Raisi iondolewe.

Nashauri muandae hoja yenye maelezo ya kutosha na yenye mifano ya kuthibitisha ni kwanini kinga hii ni lazima iondolewe na msisahau kutaja mfano wa mataifa makubwa ambayo viongozi wao hawana kinga.

Nasema hoja hii iwe na maelezo ya kutosha kwasababu moja tu.Najua hoja ya aina hii si rahisi kuruhusiwa hata kuingia tu Bungeni hivyo wakiisha ikataa nyie muisambaze mitandaoni ili wananchi waisome,waielewe na kisha wapime dhamira ya watu hawa katika hiki kinachoitwa "vita ya uchumi."

Tumieni nafasi zenu kama wabunge kuwaonyesha watanzania dhamira halisi ya viongozi tulioanao ili wasichotwe akili na hizi press conference za kila siku.

Tena nawashauri na nyinyi muitishe press conference na kuuleza umma nini kilichotokea iwapo hoja za aina hiyo zitakataliwa.

Wapinzani ni wakati wa nyinyi sasa kubadili mbinu za kuendesha siasa maana hawa wenzetu sasa wamebadili mbinu na nyie ndio watu pekee wa kuwasaidia na kuwafumbua macho watanzania.

Mnaweza pia kupeleka hoja ya kutaka mikataba ya Bombadier,ununuzi wa radar,ujenzi wa Airport Chato,n.k viwasilishwe Bungeni.

Nyie mjifanye kama wajinga kupeleka hoja hizo Bungeni na zikikataliwa wananchi wenyewe watapima.

Tuachane na mbinu ya kutegemea tu mikutano ya kisiasa bali ni wakati wa nyie sasa kukutana na kubuni mbinu mpya na kuweka mikakati ya namna ya kuendesha shughuli zenu za kisiasa.
 

Mbunge wa Nzega kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Hussein Bashe amefunguka na kutaka katiba ya nchi kubadilika ili ikiwezekana kinga ya Rais iondolewe kwenye katiba kwa kuwa kinga hizi zinawafanya viongozi hao kufumbia macho baadhi ya vitu.

Bashe amesema hayo jana mjini Dodoma baada ya kamati za bunge kutoa ripoti juu ya biashara za madini ya Tanzanite na Almasi ambapo katika ripoti hizo baadhi ya mawaziri wa serikali mbalimbali wametajwa kuhusika katika kufanya maamuzi ambayo yamelitia hasara taifa kwa maslahi yao binafsi.

"Umeona maamuzi yaliyofanywa na mawaziri waliotajwa kwenye hizo ripoti unatakiwa kujiuliza swali la msingi hivi maamuzi yote yale ya kuvunja sheria yaliyofanywa na mawaziri hivi Marais waliokuwa madarakani walikuwa hawajui?

"Leo Rais Magufuli asingekuwa tu amesukumwa na moyo wake kufanya haya anayofanya kwenye uwekezaji wa madini tungeyajua haya? Umefika wakati kama nchi wa kuangalia uwezekano kufanya mabadiliko ya katiba, tuangalie mabadiliko ya sheria tuangalie tunapowapa marais hawa kinga haya mambo ndiyo hutokea" alisema Bashe

Bashe anaamini kuwa maamuzi ambayo hufanywa na mawaziri hao ili kufanya mabadiliko makubwa katika baadhi ya mikataba ambayo imeigharimu serikali na nchi kiujumla kuwa ni lazima viongozi wao wa juu ambao ni Marais walikuwa wakitambua mambo hayo.


Mpekuzi
 
She ria hiyo haiwezi kupitishwa sababu haiwezi mwacha mtu salama hata baba J hatapona akimaliza mdawake
 
Safi Bashe, umekua ukiwakilisha maoni ya wazalendo wengi sana, hongera kwa kutokua mnafiki
 
rais aliyafahamu mengi ila kinga iliwanda mpaka washikaji zake akina rostam na lowassa!
 
Tunaishi kizamani sana, mambo mengi ya kubadilisha kwenye katiba.Hivi kweli kipengele kuwa mbunge ujue tu kusoma na kuandika kipo au ninaota? Naomba hata mwenyekiti wa kitongoji katiba itaje kiwango cha elimu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ikithibitika kuwa rais aliemaliza mda wake, au ambae yupo madarakani amevunja katiba basi akimaliza muda wake apelekwe kortini.

ilivo kwa sasa ni ngumu mno.

tunaomba katiba irekebishwe ili kila MTU awe chini ya sheria hapo haki itatamalaki.

tazama sasa ivi Donald triumph anachunguzwa kwa kuvunja sheria za marekani kwa kujihusisha na warusi wakatiwa kampeni.

au nyie wadau mnaonaje?
 
I wish ingekuwa hivi ulivyosema naona hata kuku angetii sheria na katiba za nchi
 
Back
Top Bottom