Habari wakuu!
Mimi ni raia mwema wa nchii hii ya Tanzania.
Kuna Rais mstaafu pia ni marehemu ninataka kumshitaki.
Najua katiba yetu inatoa kinga kwa Rais pindi awapo madarakani na akistaafu pia, sijui kama ile kinga anakuwa nayo hata baada ya umauti. Kama ile kinga inaisha pindi anapofariki basi nitamshitaki kwa kosa la kushindwa kuilinda katiba au kwa kosa la kushindwa kuwalinda wananchi.
Mfano: Watu wamepotea , kuuwawa na wengine kutekwa kipindi cha uongozi wake lakini hajawahi hata kulaani, kukemea au kuwawajibisha aliowapa kazi ya kuzuia vitendo hivi.
Kwa ufupi naweza kumuhusisha na vitendo hivi haramu
Nitamshitaki ili mahakama itutafsirie kama atatiwa hatiani au la!
Ok