Kinga kwa Rais aliyeko madarakani na wastaafu ni kichocheo cha uvunjaji haki, Iangaliwe upya

Kinga kwa Rais aliyeko madarakani na wastaafu ni kichocheo cha uvunjaji haki, Iangaliwe upya

Mwanasheria mkuu atashitakiwa instead of presd. Sababu ya kinga hii ni kumfanya Rais afanye kazi yake kwa weledi na kujiamini wakati wa utawala wake. Ova!

#nafaham mtakosoa hili, but hainishtui
 
Mwanasheria mkuu atashitakiwa instead of presd. Sababu ya kinga hii ni kumfanya Rais afanye kazi yake kwa weledi na kujiamini wakati wa utawala wake..ova

#nafaham mtakosoa hili,but hainishtui
Weledi huo unafuata katiba au unafuata matakwa yake?
 
Naomba wataalamu wa Sheria wanisaidie, ni kwa namna gani aliyekuwa Rais Magufuli anaweza kushitakiwa? Ninamaanisha hasara ya Fedha za umma iliyobainishwa na CAG ya Shirika letu la ndege?

Nasema hivi maana mara zote Marehemu alituambia kuwa tunapata faida kubwa. Alitudanganya? Maana wasishitakiwe watendaji tu kumbe mwelekezaji alikuwa mwingine.

Sheria zinasemaje maana huyu alikuwa ni taasisi na mawakili wake. Tusijenge Utamaduni kwamba mtu keshakufa basi inakuwa mwisho wa story ili iwe fundisho.

Tukumbuke muswada aliopeleka Bungeni kwa hati ya dharura ikitaka viongozi wa Kitaifa wasishitakiwe kwa makosa waliyofanya wakiwa madarakani baada ya kustaafu. Kumbe ndiyo haya. Mnisaidie maana huko Italia kaburi la Marehemu kiongozi liliwahi kuchapwa viboko kwa hasira ya umma!
#FreedomIsBack!
 
Habari wakuu!

Mimi ni raia mwema wa nchii hii ya Tanzania.

Kuna Rais mstaafu pia ni marehemu ninataka kumshitaki.

Najua katiba yetu inatoa kinga kwa Rais pindi awapo madarakani na akistaafu pia, sijui kama ile kinga anakuwa nayo hata baada ya umauti. Kama ile kinga inaisha pindi anapofariki basi nitamshitaki kwa kosa la kushindwa kuilinda katiba au kwa kosa la kushindwa kuwalinda wananchi.

Mfano: Watu wamepotea , kuuwawa na wengine kutekwa kipindi cha uongozi wake lakini hajawahi hata kulaani, kukemea au kuwawajibisha aliowapa kazi ya kuzuia vitendo hivi.

Kwa ufupi naweza kumuhusisha na vitendo hivi haramu

Nitamshitaki ili mahakama itutafsirie kama atatiwa hatiani au la!

Ok
 
Kweli Tanzania ni nchi ya kuingwa, rais mstaafu wa afrika kusini Jacob Zuma amefungwa jela kwa miezi 15 huku kwetu ukifanya makosa kama hayo ya zuma hufungwi kinga itafanya kazi. Ndio maana katiba mpya inapigwa vita na watawala.
 
Maccm yanaogopa Katiba Mpya kuliko hata kifo!! Inashangaza sana.
 
Hizi Kinga ndizo zinazofanya afrika haiwezi kuendelea.
Afrika itaendelea siku viongozi wake watakapoanza kuishia jela kama mabara mengine.
 
Kweli TANZANIA ni NCHI ya KUINGWA,Rais Mstaafu wa AFRIKA KUSINI Jacob Zuma AMEFUNGWA Jela kwa MIEZI 15 huku Kwetu Ukifanya Makosa kama Hayo ya ZUMA hufungwi KINGA ITAFANYA KAZI.Ndio Maana KATIBA MPYA inapigwa VITA na WATAWALA.
Ni muda wao wakudemka,ila sisi tunaitaka katiba mpya, wakielewa wanayofursa ya kuanzia hapa, walipo , wasipoelewa tutaitumia hiyo katiba mpya kufukua makaburi, pamoja na Kinga zao.
 
Hakika Mpaka leo huwa Najiuliza Kwanini Magufuli na Viongozi Wenzake Walipeleka Muswaada Bunge wa kujiwekea kinga ili Wasishtakiwe.

Je, Wamepanga kutufanyia nini ili tusiwashtaki?

Mbona AWAMU zilizopita Hazikufanya hivyo?
 
Mauaji makubwa yangekuja kutokea maana wasingetoka madarakani kwa Amani. Na uwezekano huo bado upo, ila muovu namba moja ndio kaondoka.

Mazingira ya unyama kurejea nchi hii ni makubwa maana katiba bado inaruhusu mtu muovu kushika madaraka ndani ya nchi hii, na amri yake ndio final.,
 
Hivi ndugu zangu ni kwanini uwezo wetu wa kufikilia unakuwa duni sana kiasi hichi.

Unataka kuniambia hawa wabunge na viongozi wengine wote hawaoni upungufu wa sheria hii kuwa ni mwanzo wa maovu kama haya, angalia mambo ambayo mkapa kayafanya mpaka anaona aibu kuongea na watu, lakini eti sheria inamlinda.

Nadhani sheria hii ilikuwa inastaili enzi hizo za Baba wa Taifa waliokuwa waadilifu na wazalendo kweli ambao mpaka sasa tunatamani wangekuwepo, lakini sio enzi hizi za akina mkapa kikwete, tunaoomba hata wapate matatizo yoyote na watoweke muda wowote kwa jinsi walivyotutesa na wanavyoendela kututesa watanzania,

Na ni kwanini hata wabunge wasishirikiana hata katika hili jamani, hii katiba yetu mbona mbovu namna hii jamani, watu wanaiangalia tu kwa sababu ndo inawapa ulaji tu sio

Poa, ila iko siku itafika tu na mambo yataenda kama tunavyotaka
Mpaka nafsi ikamsuta akaamua kuandika aliyofanya ndipo akafa
 
Back
Top Bottom