Kinga kwa Rais aliyeko madarakani na wastaafu ni kichocheo cha uvunjaji haki, Iangaliwe upya

RAIS ni kielelezo NO 1 cha maadili ya taifa. Wafanye haraka kuweka hiyo kitu maana nchi hii ipo katika QUANTUM LEAP (Wanasayansi wanaelewa). Tunataka kutoka kwenye level Moja ya chini Kwenda ya juu kwa Hatua kubwa na ya muda mfupi.
Kizuizi NO 1 Ni kuwepo kwa watu wenye option ya kuzuia hili na sheria inawalinda. Naunga Mkono Hoja.
Ila umakini unahitajika katika kila jambo jipya.
 
Salary huu umungu aliopewa Mtukufu, hakuna wa kuwa na wazo hilo
 
Salary huu umungu aliopewa Mtukufu, hakuna wa kuwa na wazo hilo
Ni ujinga tu huu.Iweje nchi zilizoendelea maraisi wao wanashitakiwa alafu sisi nchi ombaomba maraisi hawaguswi ili hali kila kukicha wanatuhmiwa?
 
Unajua unaweza ukawa unatumia muda na nguvu nyingi kuwaza mambo ambayo unadhani ni ya muhimu na kuwacha mambo ambayo yanatakiwa kuwa kipaumbele kwa wakati uliyopo.
 
Ni ujinga tu huu.Iweje nchi zilizoendelea maraisi wao wanashitakiwa alafu sisi nchi ombaomba maraisi hawaguswi ili hali kila kukicha wanatuhmiwa?
Sslary huu umungu tunaompa Mtukufu nadhani humu JF kuna watu akisema mimi ndiye baba yako watawakana baba zao. Kufikiri kumekufa kuwa presidents are not infallible
 

JPM atafanikiwa kuleta mabadiliko endelevu kama atarejea kwenye mchakato wa katiba mpya kwa kuitupilia mbali katiba ya Six na macho ya makengeza na kurejesha rasimu ya Warioba tu.
 
Hawawezi kuondoa kwani kipenzi chao mstaafu kitamgusa hiyo sahau.
 
atakayepinga hili.....sitafatilia tena mchango wake humu JF
Mie napinga, nachosema watete mchakato mpya wa katiba mpya, vyote hivyo vitajibiwa humo. Kutoa kinga ya rais bado haijatatua tatizo la Dira la taifa letu i-wapi
 
Kumbuka bunge linweza kumwondolea kinga Rais mstaafu.
 
Ndio maana nimependekeza hiyo hoja ianzie Bungeni badala ya hoja hii kuanzia serikalini.
Katiba ya sasa ipo wazi kwenye hilo. Inaweza kupelekwa hoja ya kuondoa kinga ya Rais mstaafu ili ashitakiwe. Zambia walishawahi kufanya hivyo kwa short chassis Chiluba.
 
Kama ulikuwepo kwenye kijiwe chetu cha jana mkuu! Hili suala tulilijadili sana kuwa wakati sasa umefika wa bunge kumwondolea kinga rais na kumpunguzia madaraka! Ifike wakati wabunge waweke vyama kando na kuungana katika mambo muhimu kama haya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…