Kinga kwa Rais aliyeko madarakani na wastaafu ni kichocheo cha uvunjaji haki, Iangaliwe upya

Kinga kwa Rais aliyeko madarakani na wastaafu ni kichocheo cha uvunjaji haki, Iangaliwe upya

Kwa Tz hayawekani maana vyama vya siasa havipendi kuona mtu anayetoka chama chao anashitakiwa mf.rasimu ya katiba ya Warioba iliweka kila kitu lakini wabunge wa chama fulani wakatumia uwingi wao kuikataa nchi ya wajinga itabaki hivihivi hadi akili ziwarudie
Na hao wengine wanaitaka hiyo katiba kwa sababu ya serikali tatu.
 
Mtugani wewe hukubali kazi ya Magufuli?? Uko kwenye Payroll ya Ufipa wewe unajifanya unataka mabadiliko kumbe njaa kali kibaka mzoefu wewe
IMG-20160412-WA0000.jpg

Uko wapi umakini wa John Pombe, kwa maana naona hatekelezi sera za chama chake kama alivyozinadi.
 
Ili kuleta uwajibikaji kuanzia Ikulu mpaka ofisi ya serikali mtaa, nawashauri wabunge wa CCM na wale wa UKAWA kuungana pamoja na kuifutilia mbali kinga ya Raisi.

Marekebisho hayo pia yaruhusu hata maraisi waliostaafu huku wakiwa na hii kinga nao waweze kushitakiwa iwapo kutakuwa na tuhuma zinazowahusu na zinazostahili wao kufikishwa mahakamani.

Ni matumaini yangu kuwa Magufli atakuwa wa kwanza kuunga mkono hoja/hatua hii kama kweli anaamini katika usawa na anataka kuridisha nidhamu serikalini.

Tujifunze kutoka Afrika kusini kwani inawezekana watu aina ya Zuma waliwahi ishi pale magogoni au wakaja kuishi siku zijazo.

NB:Nimeleta habari kuunga mkono wazo la mwandishi,Prudence Karugendo katika makala yae katika gazeti la Mwanahalisi la leo iliyoko katika ukurasa wa 14 wa gazeti hilo.Makala hiyo mwandishi ameipa kichwa cha habari kinachosomeka: "JPM atumbue kinga ya maraisi wastaafu."

Tofauti na alivyopendekeza mwandishi Karugendo,mimi nimeona ni vizuri hoja hii ianzie Bungeni moja kwa moja badala ya kusubri serikali ndio ipeleke hoja hiyo Bungeni ili kumtomjenga raisi uadui unaoweza kujitokeza baina yake na watangulizi wake.
Bunge la jmt lina wabunge wa ukweli kutoka upinzani tu,hao wengine ni bora liende
 
JPM atafanikiwa kuleta mabadiliko endelevu kama atarejea kwenye mchakato wa katiba mpya kwa kuitupilia mbali katiba ya Six na macho ya makengeza na kurejesha rasimu ya Warioba tu.
Labda kama alikuwa mgombea huru/binafsi lkn kama alivaa nguo za kijani hilo jambo sahau
 
Ili kuleta uwajibikaji kuanzia Ikulu mpaka ofisi ya serikali mtaa, nawashauri wabunge wa CCM na wale wa UKAWA kuungana pamoja na kuifutilia mbali kinga ya Raisi.

Aliyekwambia Raisi hashtakiwi ni nani? Raisi hushtakiwa lakini mashtaka yake hupelekwa kwa wawakilishi wa wananchi ambao ni wabunge Ambako mashtaka yake yatasomwa bungeni ,kujadiliwa na ikionekana yana mantiki watapiga kura ya kutokuwa na imani na raisi.

Ukitaka raisi ashtakiwe mahakamani ni wehu.Atakuwa kila siku anakesha mahakamani badala ya kufanya kazi zake Ikulu.Chukulia wiki hii anatakiwa Mwanza labda alizaa na mtu kamtelekeza mwanae anatakiwa aende.Keshokutwa Raisi labda ana shamba mtwara jirani kamshtaki mahakamani kuwa hilo shamba alimpora anatakiwa aende mahakani mwenyewe ,keshokutwa kuna kesi kigoma kuna mwalimu analamika raisi alimpiga kibao siku alipotembelea shule yake! Sasa kutwa raisi atakuwa ni kushinda kwenye kesi atafanya kazi saa ngapi.

Anyway salary slip mwanzisha hii mada unajulikana vizuri kwa uchochezi unaeleweka vizuri tu.Sababu zako za kuwa hivyo unazijua mwenyewe na.................Anyway niishie hapo.
 
Wakati huo huo wapitishe ile sheria ya kuwawajibisha wabunge wasiotimiza wajibu wao majimboni mwao
 
Katiba ya sasa ipo wazi kwenye hilo. Inaweza kupelekwa hoja ya kuondoa kinga ya Rais mstaafu ili ashitakiwe. Zambia walishawahi kufanya hivyo kwa short chassis Chiluba.

Sheria inasemaje? Hivi kosa na sheria kipi kinachotangulia? Nadhani ikiondolewa itaanza kufanya kazi kwa watakaostaafu baada ya kinga hiyo kuondolewa.
 
Sheria inasemaje? Hivi kosa na sheria kipi kinachotangulia? Nadhani ikiondolewa itaanza kufanya kazi kwa watakaostaafu baada ya kinga hiyo kuondolewa.

Rais ana kinga ya kutoshitakiwa kikatiba. Lakini katiba hiyo hiyo, inaruhusu kuondolewa kwa kinga hiyo iwapo inabidi afunguliwe mashitaka. Azimio la kuondoa kinga kwa muda lazima liungwe mkono na majority (2/3?) bungeni.
 
ni wazo zuri lakini hapo usitegemee kuungwa mkono na mwana ccm yeyote kwa jinsi navyowafahamu wana ccm na viongozi wao watasubiri mpaka waone Makufuli anaelekea wapi katika hiyo hoja ndio waunge mkono wa ndio maana wao kutoa wazo tofauti na rais wao ni kosa kubwa sana kwa sasa wamejikita kuunga mkono kila kitu kinachosemwa na Rais
 
Aliyekwambia Raisi hashtakiwi ni nani? Raisi hushtakiwa lakini mashtaka yake hupelekwa kwa wawakilishi wa wananchi ambao ni wabunge Ambako mashtaka yake yatasomwa bungeni ,kujadiliwa na ikionekana yana mantiki watapiga kura ya kutokuwa na imani na raisi.

Ukitaka raisi ashtakiwe mahakamani ni wehu.Atakuwa kila siku anakesha mahakamani badala ya kufanya kazi zake Ikulu.Chukulia wiki hii anatakiwa Mwanza labda alizaa na mtu kamtelekeza mwanae anatakiwa aende.Keshokutwa Raisi labda ana shamba mtwara jirani kamshtaki mahakamani kuwa hilo shamba alimpora anatakiwa aende mahakani mwenyewe ,keshokutwa kuna kesi kigoma kuna mwalimu analamika raisi alimpiga kibao siku alipotembelea shule yake! Sasa kutwa raisi atakuwa ni kushinda kwenye kesi atafanya kazi saa ngapi.

Anyway salary slip mwanzisha hii mada unajulikana vizuri kwa uchochezi unaeleweka vizuri tu.Sababu zako za kuwa hivyo unazijua mwenyewe na.................Anyway niishie hapo.
Maneno mengi point sifuri!Kila kitu kwako wewe ni uchochezi!Wewe unawakilisha fikra na mawazo ya watanzania wengi na watu kama nyinyi ndio sababu ya CCM kuendelea kutawala nchi hii.
 
Back
Top Bottom