Kinga kwa Rais aliyeko madarakani na wastaafu ni kichocheo cha uvunjaji haki, Iangaliwe upya

Kinga kwa Rais aliyeko madarakani na wastaafu ni kichocheo cha uvunjaji haki, Iangaliwe upya

Hiyo hoja naiunga mkono. Wabunge waondoe kinga ya Rais. Maana kwa vile magu kaanza figisu figisu, sasa iwe kazi tu. Maana Rais hana cha u CCM wala ukawa. Ana sura ya utaifa mbele.
 
Rais ana kinga ya kutoshitakiwa kikatiba. Lakini katiba hiyo hiyo, inaruhusu kuondolewa kwa kinga hiyo iwapo inabidi afunguliwe mashitaka. Azimio la kuondoa kinga kwa muda lazima liungwe mkono na majority (2/3?) bungeni.

Mkuu naomba unifafanulie vizuri, iwapo kinga hiyo itaondolewa hawa wastaafu(waliofanya kazi wakati wa kinga hiyo) wanaweza kuwa hatiani.?
 
Kinga ya Rais kutokushtakiwa mahakamani kwangu mimi naona ni tatizo kubwa kwa nchi kama hii ya kwetu ambayo wakati mwingine ni rahisi sana kupata marais wababaishaji na ambao wanajali maslahi yao na familia zao tu. Ni ajabu na kweli kuwa nia ya kuwepo kwa kinga ya namna hiyo ni kulinda heshima ya ofisi ya Rais lakini ni kuwa mtu anayeshika nafasi hiyo ni wajibu wake kutunza heshima ya ofisi hiyo. Kwa msingi huo ni wazi kuwa sheria ya kumlinda mtu anayeshika ofisi ya Rais inapaswa kubadilishwa na kuhakikisha kuwa Rais wa nchi anapaswa kufuata maadili yaliyopo naye mwenyewe akiwa kielelezo cha kufuatwa pasipo kuwekewa kinga ya kumlinda.
Aidha ni kuwa Rais akiwa ofisini ni vigumu sana kutofautisha alichokifanya kwa mamlaka yake kama Rais na ambacho amekifanya kama yeye binafsi. Jambo hilo ni la muhimu kutengananishwa na kuwekwa bayana kwani ni rahisi kuona kuwa labda katiba ya nchi inatoa ruhusu ya kumshtaki Rais mara anapomaliza kipindi chake cha uongozi kwa mambo aliyoyafanya kama yeye binafsi. Ila kwa mambo aliyoyafanya kama Rais hayo hawezi kushtakiwa kwayo. Swali mtari wa kupima kuwa jambo fulani amelifanya binafsi na jambo fulani amelifanya kwa capacity ya Urais ni upi?
Naunga mkono hoja kuwa sheria hiyo ibadilishwe kila mtu awajibike kwa matendo yake yasiyofaa aliyoyafanya katika ofisi kama ambavyo wastaafu wanashtakiwa kwa matendo waliyoyafanya wakiwa ofisini.
 
ni wazo zuri lakini hapo usitegemee kuungwa mkono na mwana ccm yeyote kwa jinsi navyowafahamu wana ccm na viongozi wao watasubiri mpaka waone Makufuli anaelekea wapi katika hiyo hoja ndio waunge mkono wa ndio maana wao kutoa wazo tofauti na rais wao ni kosa kubwa sana kwa sasa wamejikita kuunga mkono kila kitu kinachosemwa na Rais
Hivyo ndivyo inavyokuwa kwa vyama vyote,na ndiyo maana wengine sasa wanaitwa wasaliti kwa waliyoenda kinyume.
 
Mkuu naomba unifafanulie vizuri, iwapo kinga hiyo itaondolewa hawa wastaafu(waliofanya kazi wakati wa kinga hiyo) wanaweza kuwa hatiani.?

Maana ya kuondolewa kinga ni kwamba wanakuwa kama raia mwingine yeyote wa Tanzania. Hivyo wanaweza kutiwa hatiani. Kumbuka wote walifanya kazi wakati kinga ipo kikatiba lakini inaweza kuondoloewa kama ilivyotokea kwa Chiluba, Zambia.
 
NB:Nimeleta habari kuunga mkono wazo la mwandishi,Prudence Karugendo katika makala yae katika gazeti la Mwanahalisi la leo iliyoko katika ukurasa wa 14 wa gazeti hilo.Makala hiyo mwandishi ameipa kichwa cha habari kinachosomeka: "JPM atumbue kinga ya maraisi wastaafu."

Madhalani yeye kashaanza kuonyesha namna nzuri ya utumbuaji majipu na nadhani ni wakati mzuri kabisa uwanja wa kutimiza haki kwa wengine uweze kuwa wazi.

Mtakumbuka hili. Raisi Mstaafu Ben alikuwa mmoja wa mashahidi na kwa namna hii huku nikuifunga mkono Mahakama na vile vile kuwaepusha watuhumiwa wengine kwa vile tu ikulu ilikuwa mshirika!

balozi proffesa costa mahalu ashinda kesi ya uhujumu uchumi
 
Mkuu naomba unifafanulie vizuri, iwapo kinga hiyo itaondolewa hawa wastaafu(waliofanya kazi wakati wa kinga hiyo) wanaweza kuwa hatiani.?
(3) Except where he ceases to hold the office of President pursuant to the
provisions of Article 46A(10) it shall be prohibited to institute in court criminal or
civil proceedings whatsoever against a person who was holding the office of
President after he ceases to hold such office for anything he did in his capacity as
President while he held the office of President in accordance with this
Constitution.

Jambo linalogomba hapa "anything he did in his capacity as President while he held the office of President" sijajua watafsiri wa sheria watatafsiri vipi. Ila naona kama kuna mlango wa kuwawajibisha hao waliotangulia iwapo tu unaweza kutofautisha jambo alilolifanya kwa capacity yake kama Rais na ambalo alilifanya binafsi. Hapo ndipo shida inapotokea. Aidha ni kweli kuwa kwa mfumo wa nchi hizi za kiafrika ambapo wanajijengea dhana ya kuwa mkubwa hakosei itaonekana ni kama utovu wa nidhamu kumfungulia mashtaka kiongozi aliyekuwa mkuu wa nchi. Jambo la msingi kwanza tafsiri ya kifungu hicho cha katiba ikoje. Ni kweli kuwa Rais wa nchi akishastaafu hawezi kufunguliwa mashtaka au la?
Nchini Zambia walikuwa na sheria inayofanana na hii ya kwetu, lakini Chiluba alipoondoka madarakani aliondolewa kinga akashtakiwa. Kinga inaweza kuondolewa kwa marais waliotangulia na wakashtakiwa.
 
Kama kuna wanasheria watujuze. Lakini nadhani kinga ikiondolewa kifunga au tafsiri yake vinapoteza maana hivyo anakuwa kama raia mwingine yeyote.

Umesema kifungu cha katiba kinafanana na cha kwetu. Kama Chiluba alishitakiwa baada ya kumwondolea kinga kwenye kifungu kama cha kwetu, nina imani hata Tanzania inawezekana kufanya hivyo.

Na inaposemwa aliyofanya akiwa Rais wa nchi, kuna vitu vinaangaliwa pia. Kwa mfano, kama alitumia nafasi hiyo kujinufaisha binafsi au familia yake au kudhulumu watu, ni rahisi kumshitaki kinga ikiondolewa. Lakini kuna vitu vingine kama kuamuru vita ili kulinda maslahi ya nchi. Hapo hata kama kuna watu wamedhurika si rahisi kumshitaki.
 
Maneno mengi point sifuri!Kila kitu kwako wewe ni uchochezi!Wewe unawakilisha fikra na mawazo ya watanzania wengi na watu kama nyinyi ndio sababu ya CCM kuendelea kutawala nchi hii.

Fuatilia Jamii forums yote.Wachochezi waliobakia humu wasiobadilika ni wewe.Watu humu wanatoa hoja za kueleweka hata kama za mawazo tofauti lakini zimetulia zimeenda shule.Angalia post zako linganisha na za wengine.Wewe Uko nyuma ya wakati.Historia imebadilika Tanzania na kule nafikiri unakuelewa.Umebaki wewe tu na uchochezi wako.

Matarajio yako na wenzio hayakutimia.Hii ndio Tanzania uwaambie na wenzio.
 
kama hilo litakua suluhisho la matatizo yetu yote kama watanzania na iondolewe. lakini madhara yake yanaweza kua makubwa sana kuliko faida.
 
Ili kuleta uwajibikaji kuanzia Ikulu mpaka ofisi ya serikali mtaa, nawashauri wabunge wa CCM na wale wa UKAWA kuungana pamoja na kuifutilia mbali kinga ya Raisi.

Marekebisho hayo pia yaruhusu hata maraisi waliostaafu huku wakiwa na hii kinga nao waweze kushitakiwa iwapo kutakuwa na tuhuma zinazowahusu na zinazostahili wao kufikishwa mahakamani.

Ni matumaini yangu kuwa Magufli atakuwa wa kwanza kuunga mkono hoja/hatua hii kama kweli anaamini katika usawa na anataka kuridisha nidhamu serikalini.

Tujifunze kutoka Afrika kusini kwani inawezekana watu aina ya Zuma waliwahi ishi pale magogoni au wakaja kuishi siku zijazo.

NB:Nimeleta habari kuunga mkono wazo la mwandishi,Prudence Karugendo katika makala yae katika gazeti la Mwanahalisi la leo iliyoko katika ukurasa wa 14 wa gazeti hilo.Makala hiyo mwandishi ameipa kichwa cha habari kinachosomeka: "JPM atumbue kinga ya maraisi wastaafu."

Tofauti na alivyopendekeza mwandishi Karugendo,mimi nimeona ni vizuri hoja hii ianzie Bungeni moja kwa moja badala ya kusubri serikali ndio ipeleke hoja hiyo Bungeni ili kumtomjenga raisi uadui unaoweza kujitokeza baina yake na watangulizi wake.

"KILA MTU ABEBE MZIGO WAKE."
Naunga hoja 100%
 
Labda kama alikuwa mgombea huru/binafsi lkn kama alivaa nguo za kijani hilo jambo sahau
Kama ni hivyo haya mapambano yake hayawezi kuwa endelevu, akimaliza muda wake ataondoka nayo! It shall have been some effort to futility!
 
JPM anpambana kwa kuangalia mbele yadi 100. laiti angegeuka nyuma, kushoto na kulia naamini angeelekeza mtutu huku nyuma kushoto na kulia na kwa muda angewasahau maadui walioko mbele. Angewamiminia risasi za rashasha hawa wa kulia kushoto na nyuma na kubakiwa na wachache tu. pengine yeye mwenyewe!
akifanya hivyo, na kugeuka mbele atakuta wote wamenyosha mikono na kusalimu amri.
tatizo anaweza kweli kufanya hivyo na je kishindo chake kitakuwaje?
 
Back
Top Bottom