Karne
JF-Expert Member
- Jun 13, 2016
- 8,118
- 13,547
Kama umeipitia rasimu ya katiba pendekezwa sura ya Nane sehemu ya kwanza kipengele b (Rais) kifungu cha 94(1) Bunge linaweza kupitisha azimio la kumuondoa Rais madarakani endapo itatolewa hoja ya kumshtaki Rais na ikapitishwa kwa mujibu wa masharti ya Ibara hii. Isome hiyo attached file ni rasimu_ya_katiba_inayopendekezwa_na_bunge_maalum
Lakini kifungu cha 93(3) ndiyo kinaifanya sheria hii ikose maana.
Kama rais hakuondolewa madaraka na bunge akiwa madarakani,akistaafu huwezi kumshitaki kwa lolote hata kama madudu yake yatabainika baada ya yeye kustaafu.
Hivi kwa aina ya siasa za nchi hii ambayo wabunge hawawezi ku-cross the floor(hawawezi kwenda kinyume na matakwa ya vyama vyao hata kamA hayana maslahi kwa taifa) unadhani rais anaweza ondolewa madarakani kupitia bungeni?
Kwa nini matakwa ya kisheria yasiendane na mazingira halisi tuliyonayo sasa kama kweli dhamira ya kumshitaki rais ipo?