Kinga kwa Rais aliyeko madarakani na wastaafu ni kichocheo cha uvunjaji haki, Iangaliwe upya

Kinga kwa Rais aliyeko madarakani na wastaafu ni kichocheo cha uvunjaji haki, Iangaliwe upya

Kama umeipitia rasimu ya katiba pendekezwa sura ya Nane sehemu ya kwanza kipengele b (Rais) kifungu cha 94(1) Bunge linaweza kupitisha azimio la kumuondoa Rais madarakani endapo itatolewa hoja ya kumshtaki Rais na ikapitishwa kwa mujibu wa masharti ya Ibara hii. Isome hiyo attached file ni rasimu_ya_katiba_inayopendekezwa_na_bunge_maalum

Lakini kifungu cha 93(3) ndiyo kinaifanya sheria hii ikose maana.

Kama rais hakuondolewa madaraka na bunge akiwa madarakani,akistaafu huwezi kumshitaki kwa lolote hata kama madudu yake yatabainika baada ya yeye kustaafu.

Hivi kwa aina ya siasa za nchi hii ambayo wabunge hawawezi ku-cross the floor(hawawezi kwenda kinyume na matakwa ya vyama vyao hata kamA hayana maslahi kwa taifa) unadhani rais anaweza ondolewa madarakani kupitia bungeni?

Kwa nini matakwa ya kisheria yasiendane na mazingira halisi tuliyonayo sasa kama kweli dhamira ya kumshitaki rais ipo?
 
Hapo ndipo kuna utata na changamoto mkuu
 
Rais Mstaafu Kikwete hata asipoambiwa na Magufuli anakila sababu ya kuondoa hofu.

Kwa mujibu wa ibara ya 46 ya katiba ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 inasema kwamba Rais akiwa madarakani hawezi kushitakiwa kwa makosa ya jinai wala madai kuhusiana na jambo lolote ambalo Rais alilifanya ama kabla ya kushika kiti cha urais au baada.

Na kama Kesi ilikuwa mahakamani ikimhusu Rais toka mwanzo mara tu mtu huyu anapokuwa Rais kesi hiyo inatakiwa isimame.

Makosa ya jinai ni kama mauaji, wizi, ubakaji nk. wakati makosa ya madai ni kama kutolipa deni, kuvunja mkataba, ugoni nk.

Lakini katiba inatoa mwanya wa kumshitaki Rais kwa makosa ya madai mfano Rais hajalipa deni lako na unataka kumshtaki unatakiwa umtumie notisi mwezi mmoja kabla ya kufungua kesi ukijitambulisha jina lako na anuani yako na ueleze unataka kumshtaki kwa kosa gani.

Hii ni ili kama anaweza akayamaliza ayamalize kabla ya kwenda mahakamani.
Kuhusu Rais Mstaafu ibara hiyohiyo ya 46(3) inasema kama Rais alimaliza muda wake wa Urais kwa njia ya kawaida (hakuondolewa madarakani na bunge) basi hakuna mashitaka yoyote yatakayofunguliwa mahakamani dhidi ya mtu aliyekuwa Rais kwa jambo lolote alilolifanya akiwa madarakani kama Rais.

Na hata kama sheria na katiba ikibadilishwa kuondoa kinga ya kushtakiwa kwa Marais wastaafu sheria hiyo mpya haiwezi kumgusa Rais mstaafu wa awamu ya nne na waliomtangulia maana sheria hufanya kazi kwenda mbele ikianzia pale ilipotungwa hairudi nyuma. ( The law does not operate retrospectively).

Hivyo Marais wastaafu wanatakiwa wawe na amani tu hata wasipoambiwa na Rais Magufuli.
 
huo ndo ukweli.marais wastaafu kushtakiwa mahakamani labda katiba ibadilishwe vingine utumike udikteta....
 
huo ndo ukweli.marais wastaafu kushtakiwa mahakamani labda katiba ibadilishwe vingine utumike udikteta....
Hata ikibadilishwa haitawahusu wale ambao weshatangulia so kuwashtaki ni swala ambalo halipo unless otherwise atokee dictator asuspend katiba then afanye yake.
 
Mtoa Mada hili mbona linajulikana sana tu ila ndugu zetu hawa UKAWA akili zao zipo likizo.
 
Kwa hiyo hata rais akimpiga mtu na fimbo na yule mtu akafa bado hatashtakiwa nauliza tu wanasheria
 
Kwa hiyo hata rais akimpiga mtu na fimbo na yule mtu akafa bado hatashtakiwa nauliza tu wanasheria
Hatashtakiwa kwa kosa la jinai. Ila kama marehemu ameacha wategemezi itabidi wafungue shauri la madai ili awape fidia for the losses ya kumpoteza tegemeo lao mradi tu watimize masharti ya kumtumia Rais notice ya mwezi mmoja kabla ya kufungua shauri
 
Mwacheni Mzee wangu mpendwa Prof. Dr. Mh. Rais mstaafu JK apumzike kwa Amani. Alifanya alichoweza kwa weledi mkubwa. Hakuna kama yeye.
 
Kama tafsiri yako ni sahihi basi katiba yetu haina macho BTW nashukuru kwa kunijibu
 
Back
Top Bottom