Kinga kwa Rais aliyeko madarakani na wastaafu ni kichocheo cha uvunjaji haki, Iangaliwe upya

Kinga kwa Rais aliyeko madarakani na wastaafu ni kichocheo cha uvunjaji haki, Iangaliwe upya

Mkuu sasa Jenerali ulimwengu alikua anamaanisha nini?
Pengine Jenerali alitaka kushangiliwa na wahudhuriaji. Fuatilia walioshangilia kauli yake, wengi walikuwa ni vijana wetu walioko vyuo vikuu and the like. Kumbuka upeo wa vijana wetu bila kujali wako vyuoni ama mtaani unazidi kwenda chini, na yawezekana pia hata wanaosoma degree za sheria walimshangilia jenerali na hawakubaini kwamba alikuwa anafuka moshi ama upupu. Inaonekana kama Jenerali kapoteza uono wake hasa baada ya wakati fulani kuvuliwa uraia.
 
Rais Mstaafu Kikwete hata asipoambiwa na Magufuli anakila sababu ya kuondoa hofu.

Kwa mujibu wa ibara ya 46 ya katiba ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 inasema kwamba Rais akiwa madarakani hawezi kushitakiwa kwa makosa ya jinai wala madai kuhusiana na jambo lolote ambalo Rais alilifanya ama kabla ya kushika kiti cha urais au baada.

Na kama Kesi ilikuwa mahakamani ikimhusu Rais toka mwanzo mara tu mtu huyu anapokuwa Rais kesi hiyo inatakiwa isimame.

Makosa ya jinai ni kama mauaji, wizi, ubakaji nk. wakati makosa ya madai ni kama kutolipa deni, kuvunja mkataba, ugoni nk.

Lakini katiba inatoa mwanya wa kumshitaki Rais kwa makosa ya madai mfano Rais hajalipa deni lako na unataka kumshtaki unatakiwa umtumie notisi mwezi mmoja kabla ya kufungua kesi ukijitambulisha jina lako na anuani yako na ueleze unataka kumshtaki kwa kosa gani.

Hii ni ili kama anaweza akayamaliza ayamalize kabla ya kwenda mahakamani.
Kuhusu Rais Mstaafu ibara hiyohiyo ya 46(3) inasema kama Rais alimaliza muda wake wa Urais kwa njia ya kawaida (hakuondolewa madarakani na bunge) basi hakuna mashitaka yoyote yatakayofunguliwa mahakamani dhidi ya mtu aliyekuwa Rais kwa jambo lolote alilolifanya akiwa madarakani kama Rais.

Na hata kama sheria na katiba ikibadilishwa kuondoa kinga ya kushtakiwa kwa Marais wastaafu sheria hiyo mpya haiwezi kumgusa Rais mstaafu wa awamu ya nne na waliomtangulia maana sheria hufanya kazi kwenda mbele ikianzia pale ilipotungwa hairudi nyuma. ( The law does not operate retrospectively).

Hivyo Marais wastaafu wanatakiwa wawe na amani tu hata wasipoambiwa na Rais Magufuli.

pia katiba inazuia serikali kuingilia mihimili mingine (mihimili kuingiliana) lakin je nini kinatokea kwa hii sirikali ya sasa?! kwa dikiteta yote yanawezekana
 
pia katiba inazuia serikali kuingilia mihimili mingine (mihimili kuingiliana) lakin je nini kinatokea kwa hii sirikali ya sasa?! kwa dikiteta yote yanawezekana
Serikali ya kidicteta huvunja katiba na haizingatii utawala wa sheria hivyo wanafanya lolote
 
pia katiba inazuia serikali kuingilia mihimili mingine (mihimili kuingiliana) lakin je nini kinatokea kwa hii sirikali ya sasa?! kwa dikiteta yote yanawezekana

Uko sahihi.

Kuwa na katiba nzuri ni jambo moja. Kuifuata katiba hiyo nzuri ni jambo jingine....
 
Yaani Rais akibaka kachanga anawalk free kabisaaa!Siku tukipata Rais kichaa tutatia akili
 
Mtoa Mada hili mbona linajulikana sana tu ila ndugu zetu hawa UKAWA akili zao zipo likizo.
Sasa kama nilajulikana kuna sababu gani ya Mtukufu Rais kulizungumzia kana kwamba yeye ndiye mwenye madaraka ya kuamua kuwashtaki au la? Ni nani mwenye akili zilizopo likizo kati ya UKAWA na Mtukufu?
 
Siamini km JK anaogopa kishitakiwa, kwanza pesa za mchakato wa katiba hakutia tumboni mwake, pili mchakato bado unaendelea, na kwamba ulisitishwa tu kwa muda. Nahisi mkuu wa kaya amesema atamlinda JK ili ku make up aliyoyaongea alipokuwa akizindua maktaba udsm. Na pia kuonesha kuwa yupo pamoja na wastaafu. Nionavyo mimi mkuu wa kaya anapaswa kuweka akiba ya maneno hasa maamuzi yaliyofanywa na watangulizi wake na akumbuke ipo siku naye atastaafu na ukizingatia style yake ya uongozi.
 
"Sioni umhimu wa mahakama ya mafisadi Tanzania, kwakuwa naona hadi sasa hakuna nia ya dhati ya kutenda haki katika mahakama hiyo ya mafisadi, hii imetokana na Mh Rais John Pombe Magufuli kunikosesha imani kupitia hotuba yake jana"

Rais anaposema atawalinda marais wastaafu anamanisha nini? Hii ina maana hata kama watathibitika kuwa marais hao ni mafisadi Rais atazuia mahakama kuwapa hukumu au atatengua hukumu. Na hii inaonesha kwamba nia ya katiba mpya ni F,wazo la kupunguza majukumu na kinga ya rais ndo baaasi
 
Hivi mlivoambiwa CCM ni ile ile inamaana hamkuelewa?

Ndo hivo sasa.... mmeipenda wenyewe, chaguo lenu wenyewe.....

Kilichobaki ni kuisoma namba tu
 
"Sioni umhimu wa mahakama ya mafisadi Tanzania, kwakuwa naona hadi sasa hakuna nia ya dhati ya kutenda haki katika mahakama hiyo ya mafisadi, hii imetokana na Mh Rais John Pombe Magufuli kunikosesha imani kupitia hotuba yake jana"
Rais anaposema atawalinda marais wastaafu anamanisha nini? Hii ina maana hata kama watathibitika kuwa marais hao ni mafisadi Rais atazuia mahakama kuwapa hukumu au atatengua hukumu. Na hii inaonesha kwamba nia ya katiba mpya ni F,wazo la kupunguza majukumu na kinga ya rais ndo baaasi
Hivi kweli unategemea lolote kutoka kwa Mheshimiwa? Time will tell soon!
 
Bora ukanunue sigara ukavute tuu maana mpaka sisi tunakufa Tanzania bado inacheza makida tunabadilisha majina ya Sera za kilimo
 
Anamaanisha atawalinda kwenye maovu yao yote ya ufisadi walipokuwa madarakani. Kama utakumbuka Salma Kikwete na Ridhwan ni shareholders wa UDA ambayo imekwapuliwa kinyemela kutoka halmashauri ya jiji la Dar na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali katika ripoti yake ya mwaka aliandika kuhusu ufisadi huu. Jamaa kaamua ile ripoti iendelee kupigwa na vumbi pale Ikulu ili kuendelea kuwakingia kifua wakwapuzi wa shirika la UDA, na huyu ndiye aliyejinadi kwamba kajitoa kafara ili kupambana na ufisadi nchini.

"Sioni umhimu wa mahakama ya mafisadi Tanzania, kwakuwa naona hadi sasa hakuna nia ya dhati ya kutenda haki katika mahakama hiyo ya mafisadi, hii imetokana na Mh Rais John Pombe Magufuli kunikosesha imani kupitia hotuba yake jana"
Rais anaposema atawalinda marais wastaafu anamanisha nini? Hii ina maana hata kama watathibitika kuwa marais hao ni mafisadi Rais atazuia mahakama kuwapa hukumu au atatengua hukumu. Na hii inaonesha kwamba nia ya katiba mpya ni F,wazo la kupunguza majukumu na kinga ya rais ndo baaasi
 
Lowasa ana kashfa nzito sana ya ufisadi wa Richmond...mahakama ya mafisadi itaanza nae
 
Mnafahamu sheria na katiba inasemaje? Hapo angewashtaki mngesema anavunja katiba na dikteta. Uwezo mdogo
 
Back
Top Bottom