Kinga kwa Rais aliyeko madarakani na wastaafu ni kichocheo cha uvunjaji haki, Iangaliwe upya

Kinga kwa Rais aliyeko madarakani na wastaafu ni kichocheo cha uvunjaji haki, Iangaliwe upya

kwani ukiwaita watu uliokuwa ukiwaongoza kuwa ni MALOFA na WAPUMBAVU wewe uliyekuwa ukiwaongoza au huyo anayewaongoza kwa sasa ataitwa nani? Jibu jepesi ni kiongozi mkuu wa MALOFA na WAPUMBAVU kwa hiyo kamwe hawezi kuliepuka hilo tusi kumrudia mwenyewe.
 
Nataka kuwasiliana na mwanasheria wangu nione jinsi gani naweza kumfungulia mashtaka BM kwa kutukana. Na Fanya hivyo kwa niaba ya Watanzania tuliotukanwa.
Ila nijue kwanza, jee baada ya kukabidhi ofisi bado ana Kinga dhidi ya makosa ya jinai na madai?
Nataka niiombe mahakama pia izuie asilipwe pension yake kwa kuwaita hao wanaomlipa kwa kodi zao wapumbavu.
Hana kinga yoyote ile , kinga ilikuwa alipokuwa kiongozi , baaasiiii !!!!!

Niko tayari kuchangia pesa taslimu kwenye mchakato wako .
 
fungua tuu ndugu hiyo kesi
Mkuu nafungua kwa niaba ya wote tuliokerwa na matusi. Tutanyamaza mpaka lini? wakati ule tulichukulia kuwa ni mihemko ya kampeni ambayo kila mtu anaweza kusema lolote, lakini sasa basi! unless kama sio tusi basi nasi tuliseme hadharani kwake na kwa viongozi waliopo.
 
  • Tunaaminishwa tuko vitani, tunaaminishwa nchi inanyoshwa, tunaaminishwa lazima tupige about-turn kwani tulikokuwa tunaendelea siko na tunaaminishwa katika hii vita hakuna cha msalimie mtume.
  • Tumesimamisha shughuli za siasa, tunawakamata na kuwasweka ndani wote ambao kwa namna moja ama nyingine tunawaona kama vikwazo kwenye hii vita yetu katika kupambana na ufisadi.
  • Tumeapa kuwashughulikia bila huruma wote wale watakaotajwa kuhusika na kulifikisha taifa hapa lilipo bila kujali nyadhiza zao, sura zao na nafasi zao katika jamii.
Swali ni je, tutawezaje kufanikiwa katikaa hii vita bila kwanza kuwashughulikia vinara waliotuongoza kulifikisha taifa kwenye hali hii ya kusikitisha? Kwa nini tuko tayari kuwalaumu maaskari waliokuwa wakitii tu amri za jemadari wao mkuu?
 
Nataka kuwasiliana na mwanasheria wangu nione jinsi gani naweza kumfungulia mashtaka BM kwa kutukana. Na Fanya hivyo kwa niaba ya Watanzania tuliotukanwa.
Ila nijue kwanza, jee baada ya kukabidhi ofisi bado ana Kinga dhidi ya makosa ya jinai na madai?
Nataka niiombe mahakama pia izuie asilipwe pension yake kwa kuwaita hao wanaomlipa kwa kodi zao wapumbavu.
Hivi kweli mkapa aliposema wapumbavu,alikutaja jina lako? wewe kweli ndo mlipa kodi au unajisemea tu,nafikiri hii ya kuwawekea kinga ni nzuri maana kuna watu wanaweza kutuma chuki binafisi dhidi ya hawa viongozi ili kuwakandamiza wanapomaliza vipindi vyao vya uongozi japo na wao pia wanatakiwa kuongoza katika misingi ya utawala bora,ili kuondoa wasiwasi kwa wananchi
 
....lakushangaza wanajinadi wazalendo wa daraja la juu,mzalendo wa kweli hawezi kujiegemeza kwenye sheria egemezi kutetea uzalendo wake
 
Wanasema No One is Above The Law lakini tunajua Pakiwa na mtu ambaye hawezi shtakiwa maana yake huyo yupo above the law
 
Manung'uniko na mijadala mingi imeonekana ikisema Mheshimiwa Rais Mstaafu angefaa kupelekwa mahakamani, na wengine hudiriki kusema 'angestahili kuozea jela'.

Jambo ambalo najiuliza hata akiondolewa kinga,je katiba inaruhusu rais mstaaf kushtakiwa?

na kama inaruhusu, DPP atamshtaki kwa kosa gani na lililopo katika sheria ipi?, Je ushaidi upo wakutosha?

Adhabu ya makosa au kosa hilo ni ipi?, kifungo au fine?

je na kama kinga yakatiba ikitolewa itakua applied retrospectively?yani namaanisha itamgusa Mpaka Rais mwinyi au ni kwa marais wanaofuatia?

Dhumuni lakuuliza maswali haya ni kwasababu inaonekana kama jamii ya Kitanzania tunashabikia tu kwakusema Mkapa apelekwe mahakamani bila ya kusema kwa kosa lipi na lililokatika sheria ipi, na kujua ugum wa kikatiba unaomlinda. Si maanishi kusema tu Kiwira, la hasha hiyo haitoshi. Si maanishi kufungua kampuni ikulu, tunaweza kusema hayo yote, lakini cha muhimu sheria zetu zinasemaje kuhusu mambo kama hayo? na process yake ikoje ya kikatiba?kama nilivyouliza hapo juu.

Naomba tujadili bila matusi au shutuma.
Asanteni.
 
MTU anafanya maovu halafu anapigana apate urais,inakua kinga tosha.Raid unajiuzia mgodi kiwira
 
Back
Top Bottom