Kingo za daraja la Tanzanite zimegongwa

Kingo za daraja la Tanzanite zimegongwa

Nikikumbuka mwaka 1986 nikiwa masomoni havard nilipata kutembelea brooklyn nikapita kwa lile daraja lao nikaambiwa linatimiza miaka 100 at that time, nikiangalia na hizi picha za daraja letu halina ata chrismas tatu mtaani na kila nikifikilia uharibifu unafanywa na vijana waendesha alteeza za mwaka 1996 naumia sana
Hata Mkapa Stadium inatia aibu. Kiwanja hakijatimiza miaka 20 lakini uharibifu wa viti, masink ya vyoo, madirisha ni kielelezo cha UAFRIKA wetu.

Waafrika hatuna sense of value, period
 
Hizo chini ni baadhi ya picha zinazoonyesha kingo za chuma zilivyogongwa kwenye daraja la Tanzanite linalounganisha Coco Beach na Aghakhan Hospital.

Kuna uendeshaji wa hovyo na wa kizembe unaofanyika na vijana wanaofanya mashindano wakiendesha magari aina ya Altezza.

Samia Suluhu Hassan, alizindua mnamo March 2022 daraja jipya la TANZANITE, lenye urefu wa kilomita 1.03 ambalo limetumia sh.bilioni 243 ambazo sehemu kubwa ni concessionary loan kutoka Serikali ya South Korea.

Kama Serikali haitachukua hatua dhidi ya vitendo hivi, wale wanaotudharau watanzania watakuwa na sababu ya kutudharau.

Mtu unajenga madaraja eti kuupamba mji!
 
Daaah yaani kilometa 1 tuu imekula zaidi ya bilioni 240??? Wakati huo huo kuna mikoa bado haijaunganishwa kwa lami???
Hili ni swali fikirishi sana mkuu,nasubiria jibu makini hapa, huku lingusenguse kipindi cha masika ni balaa, kweli mwenye nacho anaongezewa,daraja la salender lipo na bado wakaongezewa jingine, la jangwani pale ni ahadi tu
 
Daaah yaani kilometa 1 tuu imekula zaidi ya bilioni 240??? Wakati huo huo kuna ikoa bado haijaunganishwa
Kwanza ni mradi wa hovyo wa JPM sawa tu na Chato Airport. Rais mwenye akili hawezi kumwaga 250 Billion kipuuzi hivyo ndani ya nchi maskini km hii wakati barabara nyingi za kuunganisha mikoa bado ni vu

Kwanza ni mradi wa hovyo wa JPM sawa tu na Chato Airport. Rais mwenye akili hawezi kumwaga 250 Billion kipuuzi hivyo ndani ya nchi maskini km hii wakati barabara nyingi za kuunganisha mikoa bado ni vumbi.
Nitajie mkoa ambao hauna lami ..next time usipost utoto humu..hiyo project JPM kaikuta kutoka kwa JK .
 
Hata daraja la kigogo-busisi ni mradi wa ubinafsi kwasababu ni kwao. Unatumia 700 Billion kujenga kilomita 3.2? Ndani ya nchi iliyojaa shida km hii? Watanzania na vyeti vyao wanahahaha mitaani wanatukanwa kila aina ya matusi. Yule atalaaniwa mpaka vitukuu vyake
nyie hamna akili kwani Tanzania kuna madaraja mangapi ..kilombero,wami,kigamboni, Tanzanite,Mkapa,rusumo.

Kanda ya ziwa ilitakiwa iwe mbali sio hvyo unavyoiona ...ndo kanda yenye madini mengi Tanzania, idadi ya watu .
Hilo daraja lilichelewa sana ..kule kuna gari nyingine sana .
 
Huu ni mradi wa JK kuanzia planning, financing hadi jiwe la msingi. JPM alikuja ku implement tu
Unaposema ni mradi wa JK una maanisha nn ...kama ulikuwa ni wake mbona hakujenga...planning sio deal tunataka results.
 
Hata daraja la kigogo-busisi ni mradi wa ubinafsi kwasababu ni kwao. Unatumia 700 Billion kujenga kilomita 3.2? Ndani ya nchi iliyojaa shida km hii? Watanzania na vyeti vyao wanahahaha mitaani wanatukanwa kila aina ya matusi. Yule atalaaniwa mpaka vitukuu vyake
flyovers za dar,daraja la wami,mji wa serikali Dodoma, njia nane kibaha,BRT phase 2&3,bwawa la nyerere,SGR,Hospitali kila kona,ndege mpya 11,Elimu bure, kufufua reli ya Arusha dar,daraja la wami,darja la pangani,stendi za kisasa+masoko nchi nzima,umeme kuunganishwa kwa elfu 27 vijijini,rada mpya 4,meli mpya za kisasa mfano MV mwanza,ukarabati wa shule kongwe,barabara za mitaa mijini, umeme wa uhakika nchi nzima,sheria mpya za madini,ujenzi wa masoko ya madini nchi nzima...

JPM hakuwa mbinafsi kijinga hivyo kama baadhi yenu mnavyomkandia kunguni.
 
Kwanza ni mradi wa hovyo wa JPM sawa tu na Chato Airport. Rais mwenye akili hawezi kumwaga 250 Billion kipuuzi hivyo ndani ya nchi maskini km hii wakati barabara nyingi za kuunganisha mikoa bado ni vumbi.
Miradi mingi Afrika ipo kiupigaji ....angalia SGR labda kwa uelewa wa kiwango changu ni vipi ilishindikana kufanya kituo kikuu kujengwa PUGU kuliko hizi gharama za kujengwa yale madaraja mf. Pale vingunguti,njia panda ya segerea,airport na kwingineko
 
Back
Top Bottom