Kuna dalili kama issue ya Tume Huru ya uchaguzi vyama vya upinzani wanataka kuiweka pembeni na kuzungumzia petty issues kama ongezeko la vituo na blabla kibao.
Nadhani sasa tuwaambie vyama vya upinzani kwa pamoja kuwa tumechoka na nyimbo, mamalamiko na kususiana kusiko na mwisho tunataka Tume huru tuu, maana hiyo ikiwepo mambo hayo ya vituo na mengine hayatakuwepo!
Sasa mheshimiwa Mbowe, Zitto, Maalimu, Mbatia, Lissu, Dovutwa nk achaneni na mengine piganieni Tume huru la sivyo bora na nyie tuwasusie tuiache nchi iliwe tuu na wachache hao ccm labda mpaka itakapotokea kizazi kingine kikaamua kutumia njia nyingine ya kuwaondoa.
Vikao vianze kwa makatibu wakuu wa vyama, iundwe secretariate ya kupanga mkakati kisha viongozi wakuu mkishirikisha asasi za haki za binadamu kulipigania hilo kwa pamoja.
Hivi hao viongozi nilio wataja hapo juu wakifikia mahali wameitisha press kwa pamoja au mkutano mkubwa wa hadhara pamoja mnadhani nini itakuwa repercussion yake kwa serikali, CCM na hata jumuia ya kimataifa?
Inaonekana propaganda ya CCM kuwa wengine hawarudi bungeni imewachanganya sana mpaka mnaona wao ndio wapiga kura!
Tume huru ikiwapo wabunge wazuri wa CCM watarudi na wazuri wa upinzani wataingia na ikiwezekana utawala unaotakiwa na sisi wananchi ukaingia madarakani.
Sasa ni eitha Tume huru au na nyie tuwasusie basi!
Sent using
Jamii Forums mobile app