Kingunge: Mchakato wa kumpata Mgombea Urais CCM ulikuwa batili! Lowassa si fisadi kama inavyodhaniwa

Kingunge: Mchakato wa kumpata Mgombea Urais CCM ulikuwa batili! Lowassa si fisadi kama inavyodhaniwa

Mbona hao kina Nchimbi, Kimbisa na Sophia wamesema wameridhia na kumkubali Bw. Magufuli? Kama utaratibu uliharibiwa kwanini wamtambue mgombea aliyepatikana kwenye utaratibu mbovu?

Navuta harufu ya unafiki hapa.
 
Sasa aone utamu wa kuvuruga taratibu na mchakato.

Kingunge ulishiriki kuvuruga mchakato wa katiba pendekezwa... Sasa usilalamike, muosha uoshwa.

Manano kunchu hayo. Tunapenda watu wenye kumbukumbu kama wewe.
 
Alipewa pesa ndefu na Lowassa kwa hiyo hivyo vikao na press conferences anazofanya ni kujustify matumizi ya hela wenyewe watakapotaka mrejesho
 
amechokA KWELI MZEE WETU AMECHOKA MWILI NA akili
 
Umenichekesha tu hapo uliposema Amemalizia kwa kusema. Mbona alichomaliza nacho ndicho umeripoti muda wote kwenye mada yako? Haya mambo ya copy and paste mabaya sana.
 
Mzee Kingunge anakuwa ndumila kuwili na anasahau katika kila jambo kuna sacrifice ambayo ni lazima itokee ili kama ni ushindi uwepo
 
TAFAKURI: Je haya ndiyo Lowassa alitaka kuyasema akashindwa hapo jana (wengine wanadai ali[pigwa 'stop')? Kwa hiyo ameona yatiokee kwa Mzee mwenye 'busra'. Aliyoyasema Mzee Kingunge hata hivyo ni ya busara na pa kuanzia kutafuta mwafaka si ndani ya Chama tu lakini pia hata katika taifa. Nanukuu nilipopapenda zaidi:

"...Nchi ili itengamae lazima chama kinachoongoza kijiendeshe kwa misingi ya haki na demokrasia, yaliyojiri Dodoma yametia dosari kabisa. Yaliyotokea Dodoma ni uvunjani wa misingi ya haki..."
 
Why only Lowasa mbona wagombea wengine 33 hawasemei?

Umeisoma hiyo taarifa vizuri au unajibu kwa haraka bila tafakuri. Rejea tena na utakuta anasema Kamati ya maadili ilifanya kazi isiyo yake na Kamati Kuu ilikosea kutowapa nafasi waombaji wote 38!
 
[Mzee kingunge ameongeza kuwa Lowassa yupo tayari kushirikiana na Chama kusaidia Chama kupata ushindi wa kishindo kwenye uchaguzi mkuu, lakini yaliyotokea lazima yazungumzwe kwa uwazi ndani ya vikao vya Chama ili watu watoe madukufuku yao.]

nadhani haya maneno ni ya busara zaidi katika maana kwamba huwezi kurudi nyuma na kubadilisha mambo yalivyokuw lakin pia hauwezi kuacha hali hii iendelea ya watu kuwa na madukuduku, migogoro inapotokea au viashiria njia ya MAZUNGUMZO na MARIDHIANO ndani ya vyam vya siasa ni jambo la msingi sana!ubabe na umimi hautasaidia katika kukuza demokrasi na kuleta mwaka ndani ya vyama vya siasa
 
Mzee kingunge ameongeza kuwa Lowassa yupo tayari kushirikiana na Chama kusaidia Chama kupata ushindi wa kishindo kwenye uchaguzi mkuu, lakini yaliyotokea lazima yazungumzwe kwa uwazi ndani ya vikao vya Chama ili watu watoe madukufuku yao.

Kingunge anadai Mkutano Mkuu umetamka Mgombea ni Magufuli, lakini ili kupata ushindi - chama kitahitaji nguvu na ushirikiano wa ndugu Lowassa na kuongeza kuwa anaamini Ndugu Magufuli atafurahia suala hilo na ataandaa mazingira mazuri ya kuipata sapoti hiyo.

Anadai Kabla ya Uchaguzi inabidi CCM kufanya mazungumzo ili wakubaliane na kukosoana lakini mwisho wa siku watoke tukiwa wamoja ili kupambana na adui.

Hapo naona ndiyo kwenye ujumbe muhimu. (1) Kwa kusema Lowasa yuko tayari........ ina maanisha hii statement ina mkono wa EL. (2) Inaelekea support ya EL na wanaomuunga mkono ni CONDITIONAL. Je Magufuli na CCM watakuwa tayari ku-meet conditions zilizotolewa? Vinginevyo watakosa SUPPORT ya EL. Hii imekaaje.
 
Angeanza kusafisha familia yake kwanza hususani na kashfa za Dawa za Kulevya. Niliwahi soma mahala iwapo Nyerere akifufuka hata dakika 5 tu na wakutane na Kingunge,Kingunge atakufa hapohapo wa kihoro cha mambo machafu aliyoyafanya baada ya Nyerere kufa. Pia namkumbusha kuwa CCM ni mabingwa wa kuiba kura akumbuke naye alivyoshiriki kuiba kura wakati wa BMK ingawa walikuwa wenyewe CCM watupu
 
Kingunge ameamua kusema Ukweli na ukweli pekee ndio unaweza kuwaweka huru wanaCCM. Japokuwa simuungi Mkono Lowassa lakini hakutendewa haki kabisa.

Kama kweli Lowassa na wenzake wenye nguvu na ushawishi ndani ya CCM waliokuwa wanagombea walikuwa hawafai, ilikuwa ni busara sana kuwapa nafasi wajumbe wa Kamati kuu, Halmashauri Kuu au Mkutano Mkuu kuamua hilo na sio kuwakata majina yao kwenye kamati ya Maadili kinyume kabisa na kanuni, taratibu na Katiba ya CCM.

Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni.
Ukifanya mambo ya hovyo utasulubiwa tu, mbona Zitto alisulubiwa ilihali ni kipenzi cha wengi? na sasa katulia tu? Kingunge kapauka kisiasa
 
Back
Top Bottom