Kingunge: Mchakato wa kumpata Mgombea Urais CCM ulikuwa batili! Lowassa si fisadi kama inavyodhaniwa

Kingunge: Mchakato wa kumpata Mgombea Urais CCM ulikuwa batili! Lowassa si fisadi kama inavyodhaniwa

kingunge ni janga,kwenye bunge la katiba alikuwa yumo wakati kanuni zinakiukwa, watu wanabaguliwa mbona hatukumsikia akipinga? Leo anapinga kwasababu lowasa MTU wake kaenguliwa,nasema huu ni unafiki.

Tena ni mfaniki aliyetukuta..wakati kanuni zinafunjwa bunge la katiba(kwa marehemu kupiga kura ya ndio) aliona ni sawa sababu haikugusa maslahi yake binafsi..sasa limemrudia ndo anaona manyinyiemu yenzake yanapindisha kanuni...shem on him...!kwendraaa huko
 
Mzee amelalamikia taratibu kutofuatwa ........ hajalalamikia Lowasa pekee kukatwa .....
Yeye alifuata taratibu kuanza kumnadi Lowasa kabla ya vikao rasmi vya UTEUZI? Mwacheni aendelee ku-retire imprest alookatiwa.
 
"Hadithi ya Lowassa kuwa ni fisadi haina mashiko, ilianza kwa kashfa ya Richmond. Kamati Teule ya Bunge iliundwa na kutoa taarifa za ovyo sana, na hatimaye kwa kulinda heshima ya serikali na chama akajiuzulu.
Kamati ilitoa ripoti ya ovyo sana. Huyu mzee amezeeka hadi ubongoni, ripoti ya ovyo ndo ikoje
 
"Hadithi ya Lowassa kuwa ni fisadi haina mashiko, ilianza kwa kashfa ya Richmond. Kamati Teule ya Bunge iliundwa na kutoa taarifa za ovyo sana, na hatimaye kwa kulinda heshima ya serikali na chama akajiuzulu.

nimeona....
 
Chama cha CCM kina wenyewe,Mzee Kingunge pammoja kuwa na kadi namba 8 hawezi kusikilizwa sababu hayupo ndani ya chama kimkakati.Pili unyeti wa kamati kuu na maamuzi yake tokea enzi za Mwalimu hadi leo hayatabiriki na mara nyingi ni kinyume cha matarajio ya wananchi.Tatu mara nyingi msimamo wa mwenyekiti ndio ulikuwa msimamo wa Kamati kuu,NEC na mkutano mkuu hata kama walikuwa na maoni tofauti.Nne kumkosoa mwenyekiti ilikuwa utovu wa nidhamu.Wajumbe waligundua kuwa ili kuwa salama kichama bora kuunga mkono mwenyekiti ili wazidi kutumikia chama.Mizengwe au viini macho ni kawaida ndaniya chama chao.Japo Mzee Kingunge aliuunda sera za chama hicho,lakini hakujua kuwa ipo siku maamuzi ya chama yatakuwa kama haya.Nani wa kumlaumu?Pole Mzee Kingunge ndio ukubwa.
 
haya sio mambo ya kudharau, kwa kuwa hakuna mwingine wa kutoa haya.! Kwa kweli anajiamini..! Ndio tunataka watu wenye msimamo kama wa huyu mzee..!
#Bg Up
 
Niliamini na nitaendelea kuamini kuwa Lowassa hafai na hakufaa kuwa mgombea wa CCM hata kama mimi si mwanachama wala si mpenzi wa CCM. Niliamini pia kuwa jina la Lowassa litakatwa hata tano bora asingefika. Ndicho kilichotokea. Kwanini niliamini hivyo? Kwanza alikuwa tayari ana afya mbovu. Pili alikuwa anatumia njia haramu kusaka uraisi wa nchi. Tatu ana visasi jambo ambalo niliamini kuwa hata kama Kikwete hawakukutana barabarani lakini suala la nchi lazima lipewe kipaumbele kuliko urafiki. Nne, nchi hii isingekuwa salama kwa Loawassa kuwa rais na lakini kubwa zaidi CCM ingekuwa chama cha upinzani kwa asilimia 90% niliamini hivyo. Tano, Lowassa alikuwa anatumia vitisho vingi kuwatisha watu wa maamuzi. Hili lilikuwa kosa.
 
Yawezekana kanuni hazikufuatwa, lakini kama kanuni hizi zingetumika kutuletea mtu asiyefaa, basi kamati ya maadili na kamati kuu walikuwa sahihi kabisa. Haiwezekani mgombea urais awe na wafuasi kama huyu mzee wasioheshimu utarartibu wa chama katika kufikisha malalamiko. Kama hivi anapoitisha vyombo vya habari na kutoa malalamiko yake kwenye media je haya ndio maadili ya CCM?
 
Hata Kingunge mwenyewe ni batili. Mtu gani haamini wala biblia takatifu wala Quran tukufu. Tunajua kwa nini anashabikia hiyo kambi sababu ni kwamba mwanaye Kinjekitile ni msafirisha madawa ya kulevya mkubwa. Na katika wagombea ambao wangemsaidia wasimkamate mwanae ni Lowassa tu kwa sababu naye ni Fisadi.


Sasa mtu akikuita mpumbavu utakasirika kweli?.Kwa hiyo wewe unaamini duniani zipo dini mbili tu Ukristo na Uislam?.

Ningekuelewa kama ungekosoa bila ya kuchanganya udini ambao ni mapokeo tu.
 
MZEE ANALIA, WAHENGA WALSEMA MKUKI KWA NGURUWE KWA BINADAMU MCHUNGU.
NI KWA SABABU HAWA WAZEE WALIISHI KWENYE MFUMO WA CHAMA NA SRIKALI UNAOFAVOUR INTEREST ZAO BILA YA KUJALI MASLAHI MAPANA YA NCHI, KWA VULE MAMBO YAMEWAENDEA KINYUME NDO WANALIALIA
KUNA MAMBO MAWILI YAYAKO SAWA HATA KAMA MZEE HATAKI KUFUNGUKA
1. KATIBA YA CHAMA CCM MWENYEKITI NI KAMA MUNGUMTU, ANA MAMLAKA NA MADAAKA MAKUBWA MNO.SIJUI KAMA HILI MZEE ALILIONA MAPEMA NA KUSHAURI MABADILIKO

2. KATIBA YA NCHI NI MBOVU KAMA ILIVYO KATIBA YA CHAMA, KWA KATIBA HII RAISI NI MFALME, MZEE, ANASEMA "KITENGO' KAMA RAISI NI MWENYEKITI WA CHAMA LAZIMA ATUMIE KITENGO KUJINYOOSHEA MAPITO, NDO MAANA KWENYE RASIMU YA WARIOBA TULITAKA RAISI APUNGUZIWE MADARAKA YEYE NA WAPUMBAVU WENZIE WAKAUVURUGA MCHAKATO.NA BADO IPOSIKU ATAKUJA RAISI ATAKAYE WAUMIZA ZAIDI KWA KATIBA HII MBOVU, AMINI NAWAAMBIENI WATAITAFUTA NA KUISUJUDIA RASIMU YA WARIOBA

3. KAMA LOWASA HAKUUSIKA NA RICHMOND, WALISHINDWA NINI KUMWAJIBISHA RAISI, KWANZA KWA KUMVUA UENYEKITI WA CHAMA THENI KUMSHINIKIZA AJIUZULU, KULALAMILA WAKATI HUU KUNASAIDIA NINI??

4. NI KWANINI RAISI KUWA MWENYEKITI WA CHAMA WANASHINDWA NINI KUTENGANISHA HIZO KOFIA MBILI ILI HIZI TAASISI MBILI ZIHESHImiANE ENZI YA SIASa za ukommonist zimeisha

5.mbona kwenye hitimisho hajatoa ushauri ya nini kifanyike ili haya yaliyojitokeza yasijitokeze. ukweli nikuwa makundi yote ni ya kifisadi, mafisadi wameziana kete fisadi mmoja kawazidi kete wenzie.sisi wananchi wazalendo hayo maugonvi yao ni huko huko, 25 october ni ukawa
 
Yawezekana kanuni hazikufuatwa, lakini kama kanuni hizi zingetumika kutuletea mtu asiyefaa, basi kamati ya maadili na kamati kuu walikuwa sahihi kabisa. Haiwezekani mgombea urais awe na wafuasi kama huyu mzee wasioheshimu utarartibu wa chama katika kufikisha malalamiko. Kama hivi anapoitisha vyombo vya habari na kutoa malalamiko yake kwenye media je haya ndio maadili ya CCM?

Tunataka mambo kwa uwazi kama hivi ,hii habari ya kulalamikia katika chama ndio matatizo huanzia hapo.Kama chama kimekwambia mfuchiane siri ili kukilinda chama mtashiriki wizi na mtalindana kwa maslah ya chama wakati Wapo wananchi wasiokuwa na chama..
 
Ukifanya mambo ya hovyo utasulubiwa tu, mbona Zitto alisulubiwa ilihali ni kipenzi cha wengi? na sasa katulia tu? Kingunge kapauka kisiasa

Malinyingi naona unaandika vitu vya ajabu. Ukweli ni Ukweli tu na unatabaki kuwa ukweli tu. Lowassa ni Fisadi kabisa lakini bado ni mwanaCCM muaminifu kwa chama chake. CCM ilipaswa kufuata kanuni, taratibu na katiba yake katika kumwondoa Lowassa na sio kufanya uhuni kama ule.

Kuhusu Zitto ni kweli ni Msaliti kwa CHADEMA dhambi mbaya zaidi katika uaminifu lakini bado kanuni, taratibu na Katiba ya CHADEMA ilitumika kumfukuza.

Alichokisema Mzee Kingunge ndio ukweli wenyewe, na utabaki hivyo hivyo siku zote. Kama humpendi Mzee Kingunge hilo ni sawa, lakini jaribu kuupenda hata ukweli wake.
 
Last edited by a moderator:
Hata Kingunge mwenyewe ni batili. Mtu gani haamini wala biblia takatifu wala Quran tukufu. Tunajua kwa nini anashabikia hiyo kambi sababu ni kwamba mwanaye Kinjekitile ni msafirisha madawa ya kulevya mkubwa. Na katika wagombea ambao wangemsaidia wasimkamate mwanae ni Lowassa tu kwa sababu naye ni Fisadi.

Mmmh sasa mbona hajakamatwa huyo dogo msafirishaji wa sembe.
 
Huyu nae sasa atuambie kwanini alijiuzuru kama alikuwa msafi si angewapeleka mahakamani waliomwaribia jina.

Hakuna jipya ikija ufisadi hajajisafisha kwa wengi, bora angeliongelea hili jambo bila kulikwepa wakati anazunguka kusalimia watu hakuna kitu kizuri kama kusafisha jina lako ukijijua hauna makosa kabisa.

Re CCM naona bado makundi yanaendelea, ni vizuri waungane sasa kuchukua nchi. Kosa lake kubwa kuzania yeye ni yeye kabla hata ya mkutano wa Chama wa uchaguzi walioufanya juzi.


hoja nyengine za kuchekesha sana, hivi mtu akijiuzulu ina maana ndio yy alietenda hayo makosa? au yy ndie alifisidi hicho kilichofisidiwa?

sasa Mwinyi kina shamsi na wengine walijiuzulu kwa kua na wao walikua mafisadi ?

iko wazi lowassa amejiuzulu kwa kuwajibika kisiasa iko wazi
 
Back
Top Bottom