Kingunge: Mchakato wa kumpata Mgombea Urais CCM ulikuwa batili! Lowassa si fisadi kama inavyodhaniwa

Kingunge: Mchakato wa kumpata Mgombea Urais CCM ulikuwa batili! Lowassa si fisadi kama inavyodhaniwa

Hivi alikatwa mtu mmoja tu au zaidi ya watu 30??????

Mkuu heshima kwa maneno yako mazito. Kiukweli sijamsoma mzee Kingunge kwa maelezo yake. Yeye aseme tu imemuuma sana kukatwa EL. Angekuwa kweli anapigania haki ya watia nia angegusia wote waliofyekwa na si kung'ang'ana na EL. Ifikie wakati aone aibu kwa hoja dhaifu kama hizi. Huyu mzee angekuwa msafi angetusaidia kukemea matukio ya ufisadi yanayotokea nchini mwetu likiwemo la wizi wa mapato ya kituo kikuu cha mabasi yaendayo mikoani cha Ubungo ambalo lilisababisha Waziri Mkuu Pinda kuunda tume.
 
Kamati ilitoa ripoti ya ovyo sana. Huyu mzee amezeeka hadi ubongoni, ripoti ya ovyo ndo ikoje

Ripoti ya hovyo ndo kama aliyotoa Mwakyembe iliyoficha ukweli ili "serikali yote isianguke!" Na hili alilikiri Mwakyembe mwenyewe kwamba hawakusema yote! Nina imani ni swala la muda tu na ukweli wote kuhusu Richmond, IPTL, Simba Trust etc utajulikana kwa uwazi kwa Watanzania!
 
nimekumbuka nassor moyo yy kadi yake namba saba alisema na kule zanzibar wamemng'oa sasa kingunge ansema kadi yake namba nane sijui kama na yy hafuatii kupokonywa kadi

maana wenye chama wa leo ni watu wasiovumilia kuambiwa ukweli. wakiambiwa ukweli na hasa walioasisi chama kama kina kingunge warioba butiku moyo na mfano wao huhamaki na kuamaua kuwafanyia visa na vituko na mmoja kasema kama watampiga risasi na wampige ila yy haachi kusema ukweli

na kamchana live mwana kundi mtandao kua walianzisha kundi la kihuni tokea zamani
 
Naona CCM kinaenda kufanya na hali so shwari! Watu wanajifariji tu na sasa mabadiloko yanakwenda kupatikana nje ya CCM. Hata pale walipo kwenda Zakhiem walifanya makusudi kwa sababu uwanja ilikuwa mdogo na pia walisomba watu kwa kutumia UDA zaidi ya sabini!

Mpaka wakati Wa kampeni ufike Mengi yatakuwa yamejitokeza. Kwa sababu wengi hawajaridhika na kura nyingi za chuki zitapigwa dhidi ya CCM.

Tusubiri UKAWA wamtangaze mgombea wao wa urais.
 
Angeulizwa zabuni ya kukusanya ushuru kwenye kituo cha mabasi ubungo...aliipata kihalali? au alisaidiwa na Lowasaa ndio maana anampigania!!
 
Huyu mzee amechoka hajui lowassa alishainunua demokrasia na kilichobaki ni kutumia mbinu mbadala kumtoa na kundi lote la mafisadi
 
Ukiona hvyo ujue wengine hawakua siriaz na huo uraisi.
si tu kua hawakua serious ila inaonyesha ilipangwa kimkakati ili iwe rahisi kumchinjia lowassa baharini. na wao wanashikilia walikua wengi na tumewakata wengi na hakukuwa na malalamiko kwa nn alalamike yy tu. hii yote ilikua strategic ili wahalalishe waliokua wanataka kuyatenda na mwisho wakayatenda
 
Tunataka mambo kwa uwazi kama hivi ,hii habari ya kulalamikia katika chama ndio matatizo huanzia hapo.Kama chama kimekwambia mfuchiane siri ili kukilinda chama mtashiriki wizi na mtalindana kwa mas looplah ya chama wakati Wapo wananchi wasiokuwa na chama..

Chama lazima kife kwa rough zilizochezwa na kinachopatikana kwa haramu kitayeyuka kwa haramu.

Hata Mwenyekiti alipoambia kuhusu kudhibitisha tuhuma za Lowassa alishindwa alisema Ana Mali nyingi zaidi. Alipoambiwa kuna wenye fedha nyingi kuliko Hazina alinyamaza kimya.
 
Hata Kingunge mwenyewe ni batili. Mtu gani haamini wala biblia takatifu wala Quran tukufu. Tunajua kwa nini anashabikia hiyo kambi sababu ni kwamba mwanaye Kinjekitile ni msafirisha madawa ya kulevya mkubwa. Na katika wagombea ambao wangemsaidia wasimkamate mwanae ni Lowassa tu kwa sababu naye ni Fisadi.
Hoja yako haina mashiko ndugu. Huwezi kuwa batili kwa sababu tu huamini wala kufuata dini na miungu wa kigeni.
 
Hili ni FUNZO kwa wote wanaounda Sheria kandamizi, ipo siku zitawarudia. Kingunge bado haamini sheria zao za kiimla walizotunga mwaka 70 zingekuja kumuadhibu mwaka 2015.

It's called karma,and its such a ...,
 
Tayari history imeshaandikwa!
Kingunge anatafuta nini?
 
hakika "mkiijua kweli itawaweka huru". kama wenyewe mwatendeana haya, itakuwa vipi kwa wapinzani? Naam, naamini mtawatendea mabaya kupitiliza.
 
Hivi waandishi wa habari huwa wanataarifiwa vipi kama mtu unataka kuongea nao? Nataka kuongea na waandishi wa habari
 
Mzee ukweli siku zote ndio unao mueka mtu huru amini mutashinda la msingi kueka nia ya dhati kusema ukweli.
 
"Selective Amnesia" ya WaTZ inafurahisha.

Kingunge kaanza kueleza ubatili wa mchakato uliopeleka majina matano kamati kuu. Hii inamaanisha ni wale 33 waliokatwa.

Lakini kwa kuwa tunaliangalia jambo hili kwa shauku ya kumnyonga zaidi Lowassa, maelezo yake kuhusu Lowassa yanachukua nafasi ya juu na kupindisha alishokisema.

Kingunge amesema "Kamati ya Maadili huko nyuma ilikuwa ni chombo cha kuandaa taarifa ili kuisadia Kamati Kuu ktk kuwajadili wagombea"

Amesema Kamati ya Maadili ya safari hii imefanya kazi isiyowahusu kikatiba - kukata majina ya wagombe.

Kingunge amesema Kamati ya Maadili ya CCM yenyewe imekosa maadili ya kuheshimu katiba na taratibu za chama.

Amesisitiza Kamati ya Maadili haikuwa na madaraka ya kupeleka majina 5 kwenye kamati kuu, ambayo ilipaswa kuhoji wagombea wote 38.

Kwa mujibu wa Kingunge, Kuna baadhi ya watu waliamua kuitumia Kamati ya Maadili kuandaa watu wao na kuwakata wengine kwa sababu zao.
 
CCM hawajawahi kufuata sheria au taratibu kwenye mambo makubwa.... kuwa wanaangalia upepo unaendeje!! Huyu mzee anatakiwa kulijua hili vizuri kabisa kwa vile amekuwa part ya maamuzi ya design hizi ndani ya CCM kwa muda mrefu!!!!
Well said Mr. Zero
 
Last edited by a moderator:
Kingunge nimempenda kwa kusema ukweli huu na kwa ujasiri bila uoga, ila nimembeza kwa kutokusimamia ukweli wa aina hii wakati bunge la katiba liliposigina kanuni, katiba, sheria na hata kanuni za asili.
Maoni ya wananchi yalipuuzwa, katiba pendekezwa ikapitishwa kwa ghiliba, marehemu wakapigishwa kura, na uchafu wote ambao watu wastaarabu wasingerhusu kufanyika katika ulimwengu huu wa leo. Yote haya Kingunge hakuyasemea alichekelea, leo yamemrudi ya wala nyama za watu chembilecho Nyerere alisema mkishaanza kubaguana hamtaishia kwa hao mnaowabagua bali mtafikia kubaguana wenyewe.
Leo linaongelewa goli la mkono la Nape hakuna aliyekemea, si Kingunge wala Sofia au Lowasa mwenyewe kwa sababu ya kufikiria goli la aina hiyo litaelekea upinzani, Mungu asiyemnafiki ameruhusu lianzie kwenu nanyi mnalalama. Sasa Kingunge na wenzio tumieni ujasiri huo huo kutujuza wizi wa kura hufanykaje kupora maamuzi ya wananchi na hapo ndipo tutawaonea huruma mnayoitafuta sasa vinginevyo mgangamale kivyenu mnaponyolewa bila maji.
 
Back
Top Bottom