Kingunge: Mchakato wa kumpata Mgombea Urais CCM ulikuwa batili! Lowassa si fisadi kama inavyodhaniwa

Kingunge: Mchakato wa kumpata Mgombea Urais CCM ulikuwa batili! Lowassa si fisadi kama inavyodhaniwa

Kingunge anasahau kamati iliyomchinja lowassa ndio iliyomchinja malecela akiwa makamu mwenyekiti wa chama taifa na yeye kingunge hakupaza sauti kumlilia!

Kinachoonekana sasa ni mbinu mbadala ya kundi LA mafisadi wanaomzunguka lowasa kutaka wasisahaulike kwenye utawala mpya

Pia kasahau kutuambia yeye na mwalimu walitumia busara gani kumfunika lowassa!

Hoja za msingi kabisa
 
Sometyms the end justify the means. Kwa kukiuka hizo taratibu tumeweza kumpata mgombea asie na makundi wala si fisadi kama maamvi. Hata kama mapungufu si kama ya edo au membe. I pray to God awe na speed ile ile na in three years nchi itapata mwelekeo.
Kinachonifurahisha Mimi ni kuona wale walioitwa mafisadi na wale wasio mafisadi yaani kwa lugha nyepesi unaweza kusema Nuru na Giza wakiungana pamoja kupata ccm moja-hii imekaaje ndugu du!!!!!!!!!!!!!!!
 
Kwisha habari yao hamna jipya tena, mbona wengine wameridhika na matokeo, yeye ni nani katika nchi hii, mgombea amepatikani basi tuendelee na mambo mengine
 
analia ulaji hautokuwepo na anajuwa anatuadaa na kilichofanyika ni dhihaka
 
Nakubaliana na Mzee Kingunge kabisa,watanzania wengi wanatumika na waroho wa madaraka kumchafua Lowasa,ufisadi ni ilani ya maccm!
 
Kwa muda mrefu watu ndani ya sisiem wamekuwa wakifurahia jinsi Watanzania wanavyoburuzwa ili kukidhi matakwa yao wasisiem.

Na wamekuwa wakikataa kukiri kwamba kuna mambo yanayoenda kinyume cha demokrasia. Hawa wanaojidai leo taratibu hazikufuatwa, wenyewe wamekuwa msitari wa mbele kuvuruga taratibu au kutokemea uovu.

Tulichokishuhudia Dodoma ni kwamba madhambi yale yanaanza kuwatafuna wenyewe sasa. Na matumizi ya pesa kulazimisha watu wadhani kwamba mtu fulani ndiye anakubalika na walio wengi hayasaidii kufuta dhambi hiyo. Itaendelea kuwatafuna. Hatuwataki watu wanaoabudu pesa namna hiyo.

Hatuwataki watu wanaozungukwa na watu waliothibitika kuwa ni waharibifu. Walioanzisha mitandao hawakujua kwamba walicreate a monster, a shapeless monster. Linakua na linajigawa na kila kitengo kinapigana kutokomeza kingine. Mnavuna mlichopanda.

Usipande bangi halafu utegemee kuvuna karanga.
 
inaonekana kingunge anajenga hoja kuwa bila kuungwa mkono na lowassa magufuli hawezi kushika dola.

sijui anaongelea watanzania walio wengi au anataka lowassa awe accomodated kwenye serikali itakayoundwa na magufuli! kama anajua hesabu ccm ni sehemu ndogo ya wapiga kura na sio lazima wanazi wa lowassa wawe na magufuli ili ccm ishinde. afadhali watoke kabisa mgonjwa wao kuliko kuendelea kulea watu wasioaminika. track record ya magufuli ishaonesha jinsi gani inavyobadili upepo.

cha ajabu kwanini wapambe wa lowassa wanalazimisha wakati kuna wagombea wengine wenye uwezo,uadilifu na wamehudumu muda mrefu kwenye siasa na utumishi wa umma hawasemi lolote! please mzee you are barking at a wrong tree. lowassa and his minions should just find a way to accept the process is done and they are not relevant to the current aspirations of majority ya watanzania.

Na MAGUFULI do away kabisa na majamaa wa lowassa na lowassa mwenyewe. sidhani kama watanzania walio wengi wanawahitaji
 
Katikati ya Maneno ya huyu Mzee Edo hatoki CCM anachotaka Tingatinga akapige magoti ili kuonyesha nguvu yake na yeye ahakikishiwe maslahi yake hizi ni siasa chafu

Hakuna maneno mazuri zaidi kumwita kingunge mpuuzi.mwaka 1995 kama lowasa walimtaka hivyo kwa nin hakumtetea badala yake ndiye aliyemkandamiza?huyu ameshakuwa fisadi lazima atetee mafisadi wenzao.eti chama kimwangukie lowasa kuvunja makundi.kwa lipi?
 
Kama Kingunge asingekua na mgombea angeheshimika sana lakini kwa sasa atadharaulika sana hakuna atakaye msikiliza, huyu ni mnafiki.

Yeye alihusika sana kuweka utaratibu mbovu wa kuingia CCM alishauri kwa JK enzi hizo kwamba ili kua Mwanachama lazima mtu asome miezi 3 yeye na JK walikua miungu mtu tena alikua mnoko sana kuwasema vibaya wenzake kwa JK. Enzi zimebadilika Ubungo haitarudi tena mikononi mwake atulie wakati umepita, alisaidia sana kujenga makundi ndani ya CCM kwa maslahi binafsi.

Kamati ndogo ya maadili ile ya watu 5 ndiyo inafanya kazi ya kushauri lakini kamati ya Usalama na maadili inaruhusiwa kupunguza kwa sababu inaongozwa na Mwenyekiti wa Chama, kwa hiyo hakuna uhalali wa kusema hayo, lugha nzuri ya kumwambia huyu Mzee ni kwamba aache kuropoka muda wake umekwisha.

Kabisa mkuu.huyu mzee anajidhalilisha tu,eti utaratibu umrkiukwa yani kamati ya maadili ipeleke jina kwenye vikao vya uamuzi ambavyo vimeshajaa wachumia tumbo?nani hajui watu wanalipwa kwa kumfanyia kazi lowasa?dharau za kutisha chama atwambie kingunge zimeanza lini?wapi kwenye katiba yao pameandikwa MTU kwanza chama baadae?ukiwa na mzee wa namna hii huwezi kwenda kuomba ushauri.
 
Magufuli kumkaribisha Lowassa kwenye kampeni zake ni ishara ya kuling'ang'ania gamba.Zama za Lowassa zimeisha na sasa nchi imerudi kwa wananchi.Wezi wakubwa nyie.
 
Kabisa mkuu.huyu mzee anajidhalilisha tu,eti utaratibu umrkiukwa yani kamati ya maadili ipeleke jina kwenye vikao vya uamuzi ambavyo vimeshajaa wachumia tumbo?nani hajui watu wanalipwa kwa kumfanyia kazi lowasa?dharau za kutisha chama atwambie kingunge zimeanza lini?wapi kwenye katiba yao pameandikwa MTU kwanza chama baadae?ukiwa na mzee wa namna hii huwezi kwenda kuomba ushauri.

hahahaa et ukiwa na mzee kama huyu huwez kuomba ushauri..hahahaaa
 
Watu wanam-puuza/dharau/kejeli Kingunge kwa sababu ya kuegemea kwake kwa Lowassa! Ila katikati ya mstari anafikisha ujumbe kuwa ccm hawako wamoja kama wanavyodhani! Kuna wale waliokuwa na matarajio makubwa na pengine walishaahidiwa kwa namna fulani, lakini wakakatwa na "Kitengo" katika hatua za mwanzo kabisa bila hata kupewa haki ya kusikiliwa!

Hawa hawajasema chochote hadharani, na pengine hawana guts za kusema, ila ndani wana maumivu na hakuna mwenye kujua gizani watafanya nini kulipiza kisasi!

CCM wasijidanganye, panapofuka moshi...............!
 
kwa kifupi sana


wakati wa kikao cha maadili kujadili report za watia nia kusomwa membe na lowasa wote walikatwa majina ...report zao zilikuwa mbaya sana..tena mbaya mno...ila ya lowasa ilikuwa mbaya zaidi kuliko.....mtu aliyeongoza kwa kuw ana alama za juu kwenye maadili ni Makongoro,magufuli, makamba, migiro na huyo amina... kamati ikaazimia kuchuku majina hayo kwa sababu walizozijua wao...baada ya mda mweneyekiti akaonekana kutoridhika na hiyo tano bora..akamwita mstaafu wa awamu ya tatu na ya pili na pia kina malecela...akalamimika kuwa tano bora yote imejaa watu ambao wao wazee wastaafu waliwataka..yeye kama mwenyekiti hana mtu...iweje tano bora awe na mtu mmoja tena mwanamke..mvutano kidogo ukatokea...mwenyekiti akapewa uhuru wa kuamua anachotaka...ndipo akasema namuondoa mmoja na kuweka mwingine...akaliondoa jina la Makongoro na kuweka la membe..wazee wastaafu wakashangaa sana ...ili amani ya yerusalemu iendelee kudumu wakakubaliana na mawazo ya mwenyekiti japo kwa shingo upande...
wakarudi chumba cha mkutano wakawaeleza wajumbe wa maadili juu ya mabadiliko hayo ...minong'ono ikatokea mle ndani..gafla mwenyekiti akafunga kikao.... na kutoka na hiyo tano bora iliyochachuliwa kwa kuondolewa makongoro na kumwingiza membe...hii ni kwa kifupi sana hivyo ndivyo ilivyokuwa...badae huko mbele nikipata mda ntaeleza kwa nini lowasa alikatwa tena kwa kutumia ''collecting ink''...


mmhh..kaazi kwey kwey...yalifika huku?...
 
Kwisha habari yao hamna jipya tena, mbona wengine wameridhika na matokeo, yeye ni nani katika nchi hii, mgombea amepatikani basi tuendelee na mambo mengine

Tanzania weeeee....Jomo Kenyata kwa Nyerere..."mimi natawala wajinga najua siku moja watakuwa werevu...wewe unatawala vipofu hawatakaa waone milele"
 
Watu wanam-puuza/dharau/kejeli Kingunge kwa sababu ya kuegemea kwake kwa Lowassa! Ila katikati ya mstari anafikisha ujumbe kuwa ccm hawako wamoja kama wanavyodhani! Kuna wale waliokuwa na matarajio makubwa na pengine walishaahidiwa kwa namna fulani, lakini wakakatwa na "Kitengo" katika hatua za mwanzo kabisa bila hata kupewa haki ya kusikiliwa! Hawa hawajasema chochote hadharani, na pengine hawana guts za kusema, ila ndani wana maumivu na hakuna mwenye kujua gizani watafanya nini kulipiza kisasi! CCM wasijidanganye, panapofuka moshi...............!


pengine roho zao zimesuuzika baad aya kuona flani na flan hawakupita...kwa kuwa flani na fulan hawakupita mioyo yao imeridhika..maana hatusikii wakilalamika kabisa...
 
Mzee anatapatapa, asome alama za nyakati, wenzie hiyo chapter imeshafungwa ndio maana Sophia Simba alishiriki mapokezi ya John Magufuli.
Huyu mzee anajisahau!
Wakati wake umepita sana.
He is no longer a prime mover, mbaya zaidi yuko upande ambao ni socially and politically unacceptable.

Nafikiri inabidi akumbushwe tena na tena kuwa yeye ni irrelevant.
 
Wewe mzee wetu, tunakuheshimu sana sana. Ndio maana tunakaa kimya. Lakini wagombea walikuwa 38. Mmoja tu, uliyemnadi kwa nguvu sana, kaenguliwa. Mbona Waziri Mkuu hasemi? Makamu wa Rais halalamiki? n.k . Wewe ulishaonyesha bias. Na hilo linakunyima consiousness ya kuyasema haya. Wewe nyamaza, usikivuruge chama. Unataka watu tuandamane? Kwa lipi?
 
Back
Top Bottom