Nyamizi
Platinum Member
- Feb 19, 2009
- 9,186
- 13,757
Kwenye hatua ya kwanza huwa hamna kupiga kura majina yote yanachukuliwa na kuangaliwa moja baada ya jingine na wale wote wenye tabia mbovu mbovu na ambao Tume ya maadili inaona hawafai huwa majina yao hayarudi, wale ambao majina yanarudi ndio hupigiwa kura sasa, nilivyoelewa mimi!
Siyo kweli,kamati ya maadili haina mamlaka ya kuchuja majina isipokuwa inafanya tathmini ya kila mgombea na inapeleka taarifa yake kwenye Kamati kuu,wenye mamlaka ya Kukata majina ni Kamati Kuu.Kilichofanyika Dodoma ni Kamati ua Maadili kujitwisha jukumu la Kamati kuu ambalo si sawa,na hapa ndio point ya Mzee Kingunge ilipo.