Kingunge: Mchakato wa kumpata Mgombea Urais CCM ulikuwa batili! Lowassa si fisadi kama inavyodhaniwa

Kingunge: Mchakato wa kumpata Mgombea Urais CCM ulikuwa batili! Lowassa si fisadi kama inavyodhaniwa

Mtu wake kakatwa na pesa amekula Mzee wa watu! Ha ha ha

Wote 38 wanalalamika isipokuwa wenyewe ni Wanafiki wakubwa sana wanalalamika chini chini Kwa kuhofia kukosa Vyeo kwenye Serikali ya magufuli , Mzee kingunge yeye kaamua kutokuwa Mnafiki ndiyo maana kaamua kumwaga radhi .
 
Halafu kamati ya maadili ina "wakata" Makamu wa Raisi & Waziri Mkuu ila inampitisha Naibu Waziri!!! Hivi hawa wanajisikiaje sasa wanapolazimika kufanya shughuli za kiserekali?? Nafikiri kujiuzulu kungewaletea heshima zaidi kuliko kuendelea kung'ang'ania madaraka ambayo hayathaminiwi hata na aliyewateua! Kwa sasa Baraza la Mawaziri halijavunjwa, je, Pinda atakuwa na moral authority ya kumkemea/kosoa/elekeza Naibu Waziri Makamba??? Only possible in Tanzania!

Ndugu yangu umesahau kuna swala la marupurupu yao ya kustaafu. Sasa inabidi kwa siku zilizobaki watumikie ------ ------ wapate mradi.
 
Huyu mzee sasa apumzike tuu,aache uroporpo wake,kamenganganiaaaaa....hiv vizee vingine bana
 
Hahahaaaaaaaaaaaaaa mnawashwa mtashindwa na mtalegea boriti liwaingie. Majibu ya serikali za mitaa ni hatua ya kwanza ya ushindi na inafuatia uchaguzi mkuu. Kuliko kura yangu iende kwa chama kinachomilikiwa na wachaga bora nimpigie mbwa. Kafieni mbele huko. Tingatinga linakuja halibakizi kitu. Babu yenu kafikia mwisho na mwambieni kabisa makengeza ajiandae kubadilisha katiba au mwenyekiti wa milele
 
Wana jamvi poleni na majukumu,

Kuna ule msemo unaosema mfadhili mbwa lakini binadamu, nimeamini huu usemi ni wa kweli CCM ili mfadhili mzee Kingunge kumpatia tenda kubwa ya kukusanya ushuru pale Ubungo na ushuru wa parking za magari Dar es salaam yote kupitia kampuni yake na NATIONAL PARKING SERVICES-NPS.

Lakini pamoja na fadhila zote sasa anakisambaratisha chama kisa swahiba wake kukatwa na kamati kuu pale Dodoma, nafikri mzee amelewa tunaomba CCM itangaze tenda tena ili akashike adabu na atambue CCM ndiyo mpango mzima yeye kuishi bongo.
 
Huyu mzee sasa apumzike tuu,aache uroporpo wake,kamenganganiaaaaa....hiv vizee vingine bana

Mzee kapumzika tayari hana mda tena wa kuhangaika na magumashi ya ccm , yeye kaamua kuanika Ukweli hakutaka kapumzika na Unafiki Kama kamati ya maadili , kasema Ukweli na siku zote Ukweli Tanzania huwa unauma sana kuliko Uongo ni tofauti na Nchi zingine ambapo waongo , longolongo, magumashi vinachukiwa sana , Mzee kingunge kasema Ukweli lakini cha Ajabu wapo watu wanamkejeli !
 
Hahahaaaaaaaaaaaaaa mnawashwa mtashindwa na mtalegea boriti liwaingie. Majibu ya serikali za mitaa ni hatua ya kwanza ya ushindi na inafuatia uchaguzi mkuu. Kuliko kura yangu iende kwa chama kinachomilikiwa na wachaga bora nimpigie mbwa. Kafieni mbele huko. Tingatinga linakuja halibakizi kitu. Babu yenu kafikia mwisho na mwambieni kabisa makengeza ajiandae kubadilisha katiba au mwenyekiti wa milele

Huu ubaguzi wako wa chadema una uhusiano gani na kamati ya maadili ? Hapa tunazungumzia mapungufu ya mchujo wa mgombea Urais kupitia ccm , huyo tingatinga Safari hii atalima juu wa mawe hata Kama atashinda itakuwa ni Kwa mbinde sana.
 
Ni Tanzania pekee Hakuna Nchi yeyote Duniani Msema Ukweli hupingwa na kumkejeli . Wasema Ukweli hapa Nchini ni maadui wa wale wanaopenda magumashi , ndiyo maana watangaza Nia wengine 37 wameamua kuwa Wanafiki Kwa kukaa kimya wakinung'unika chini chini kimya kimya wanaogopa kumuudhi magufuli asije akawanyima vyeo.ukweli utabakia Ukweli licha ya wanafiki kuwa wengi saana
 
Wanafiki oyee.... Nchi hii ni number one Kwa Unafiki Duniani Hata yakitokea mashindano ya unafiki nina imani Tanzania itazoa medali nyingi na wale watangaza Nia 37 wazatoa medali za dhahabu zote.
 
Ili kuondoa machungu ya moyoni lazima aseme, bora yeye kasema kilichomkera kuliko kuwa mnafiki na kushangilia huku roho inauma. Hongera mzee Kingunge
 
Upeo duni sana huu.
Akipewa mtanzania fadhila, akipewa mzungu ndio halali.
 
Ili kuondoa machungu ya moyoni lazima aseme, bora yeye kasema kilichomkera kuliko kuwa mnafiki na kushangilia huku roho inauma. Hongera mzee Kingunge

Mfumo wa unafiki umelelewa,ukapaliliwa,ukatiwa mbolea na mwaasisi wa taifa letu.Mavuno ndio hayo.Walitukuzwa wale waliounga mkono hata bila kutambua,na walisurubiwa wale waliokuwa na maono.Ukipanda bangi usitegemee kuvuna mchicha.Maadamu sasa tunao wahitimu wa unafiki kwa ngazi ya PHD tutegemee kwanza mkanyagano mbaya sana katika chama chao na hata mapinduzi ya uongozi ndani ya CCM.CCM ikibidi kubomoka itabomolewa na wenyewe kwa muda mfupi sana.
 
Unakuja hapa unasema waziwazi jinsi hawa mafisidi waccm wanavyolipana fadhila kwa kuwatumia wananchi wewe ukiwa mmoja wao au wewe uko kwenye kundi la kulipwa fadhila?

Akili zako zina akili kweli? Kwa nini usifikirie maslahi ya Tanzania kwanza kabla ya kufikiria kusambaratika kwa chama tena chama ambacho hakina msaada kwa mtanzania wa kawaida. Ndio maana viongozi mandezi mnaowachagua kila siku wanashindwa kuwachukulia majambazi wa kawaida hatua achilila mbali mafisadi wa mabilioni kisa wanalipa fadhila.

Wana jamvi poleni na majukumu,

Kuna ule msemo unaosema mfadhili mbwa lakini binadamu, nimeamini huu usemi ni wa kweli CCM ili mfadhili mzee Kingunge kumpatia tenda kubwa ya kukusanya ushuru pale Ubungo na ushuru wa parking za magari Dar es salaam yote kupitia kampuni yake na NATIONAL PARKING SERVICES-NPS.

Lakini pamoja na fadhila zote sasa anakisambaratisha chama kisa swahiba wake kukatwa na kamati kuu pale Dodoma, nafikri mzee amelewa tunaomba CCM itangaze tenda tena ili akashike adabu na atambue CCM ndiyo mpango mzima yeye kuishi bongo.
 
Hahahaaaaaaaaaaaaaa mnawashwa mtashindwa na mtalegea boriti liwaingie. Majibu ya serikali za mitaa ni hatua ya kwanza ya ushindi na inafuatia uchaguzi mkuu. Kuliko kura yangu iende kwa chama kinachomilikiwa na wachaga bora nimpigie mbwa. Kafieni mbele huko. Tingatinga linakuja halibakizi kitu. Babu yenu kafikia mwisho na mwambieni kabisa makengeza ajiandae kubadilisha katiba au mwenyekiti wa milele

Pole,kwanza hakuna kabila la WACHAGGA.Kama unamaana watu waishia KILIMANJARO basi kuna WAPARE,WAGWENO,WAUSANGI,WAMARANGU,WAKIBOSHO,WAKIRUA,WAMACHAME,WAROMBO,WAMASAI,WAMERU,WASIHA.Haya ndiyo makabila yapatikanayo Mkoa wa Kilimnajaro............Period.Hilo lingine limetungwa na MaCCM
 
Mfumo wa unafiki umelelewa,ukapaliliwa,ukatiwa mbolea na mwaasisi wa taifa letu.Mavuno ndio hayo.Walitukuzwa wale waliounga mkono hata bila kutambua,na walisurubiwa wale waliokuwa na maono.Ukipanda bangi usitegemee kuvuna mchicha.Maadamu sasa tunao wahitimu wa unafiki kwa ngazi ya PHD tutegemee kwanza mkanyagano mbaya sana katika chama chao na hata mapinduzi ya uongozi ndani ya CCM.CCM ikibidi kubomoka itabomolewa na wenyewe kwa muda mfupi sana.

Baada ya Kuteuliwa Makufuli bado wako wamoja...................:A S-confused1::A S-confused1::flame::flame::flame:
 
Leo Mzee Kingunge kaongea na Vyombo vya Habari, ameanza kwa kupinga mfumo uliotumika kuwachuja wagombea wa urais kupitia CCM.

Kingunge amesema "Kamati ya Maadili huko nyuma ilikuwa ni chombo cha kuandaa taarifa ili kuisadia Kamati Kuu ktk kuwajadili wagombea"

Amesema Kamati ya Maadili ya safari hii imefanya kazi isiyowahusu kikatiba - kukata majina ya wagombe.

Kingunge amesema Kamati ya Maadili ya CCM yenyewe imekosa maadili ya kuheshimu katiba na taratibu za chama.

Amesisitiza Kamati ya Maadili haikuwa na madaraka ya kupeleka majina 5 kwenye kamati kuu, ambayo ilipaswa kuhoji wagombea wote 38.

Kwa mujibu wa Kingunge, Kuna baadhi ya watu waliamua kuitumia Kamati ya Maadili kuandaa watu wao na kuwakata wengine kwa sababu zao.

attachment.php

Mzee Kingunge Ngombale Mwiru akiongea na waandishi wa Habari - Julai 15, 2015

Kingunge amewapongeza sana kina Kimbisa, Nchimbi na Sophia kukataa maamuzi ya Kamati Kuu, waliisamamia Katiba ya Chama.

Kingunge anadai CCM ni chama cha wanachama wote, taratibu na kanuni zikipuuzwa na kufanya vitu kwa maamuzi ya kikundi fulani.

Kwa mujibu wa Kingunge, kwenye vikao vya CCM Ulifanyika uhuni na dharau kwa wanachama wengine. Wakubwa waliopewa madaraka wanaona hakuna lolote tunaloweza kufanya ila mimi nitasema.

Kingunge anasisitiza, Kilichofanyika Dodoma hakikuwa sawa, Kamati Kuu iliporwa kazi yake, hii ni dharau kwa wanachama na wagombea wote.

Anasema Kamati Kuu ya Taifa CCM, ipo chini ya Halmshauri Kuu ya Taifa yenye madaraka ya kujadili mapendekezo yalioletwa na Kamati Kuu; na Halmshauri Kuu ina madaraka ya kukataa au kukubali mapendekezo yalioletwa na Kamati Kuu, lakini utaratibu huo haukuwepo.

"Nawaheshimu sana Mzee Mkapa, Mwinyi, na Karume, lakini nasikitika waliotoa michango ya kutotoa haki kwenye Kamati Kuu. Waliogombea 1995 walikuwa 16, Kamati Kuu iliwasikiliza na kuandaa orodha ya watu 6," alisema Kingunge.

"Tulipofika NEC - wajumbe wakasema mbona Jina La Lowassa halikuwemo, mjadala ulikuwa mgumu, watu walisema lazima aingie kwenye orodha. Kwa mara ya kwanza muundo wa Chama ulikuwa tested baada ya wajumbe kutaka jina la Lowassa kwenye orodha ya majina 6,” aliongeza Kingunge.

"Mimi na Mwalimu tulishangaa kuona Lowassa anakubalika kiasi kile, Wajumbe wa Kamati Kuu walikuwa kimya na kushindwa kutetea mapendekezo yao. Mwalimu na Mimi ikabidi tuingilie kati na kusaida K'Kuu, tulifanikiwa kuwashawishi wajumbe wa NEC na wagombea wakaanza kujieleza," aliendelea kuongeza.

Kingunge ameendelea kudai kuwa, wote wakati huo walikubaliana kwamba NEC ina madaraka ya kukataa au kukubali mapendekezo ya Kamati Kuu.

"Safari hii tumeona wazi kwamba NEC yote msimamo wao ulikuwa wazi, lakini haikutumika busara, vitu vikaenda kama vilivyopangwa na “KITENGO”. KITENGO kilitoa maelekezo ya kumzuia Lowassa asipate haki yake ya msingi ndani ya Chama.

"Kuna watu wananiuliza kwamba Lowassa Fisadi, na wewe mzee unamuunga mkono, sasa ningependa kusema hivi:

"Hadithi ya Lowassa kuwa ni fisadi haina mashiko, ilianza kwa kashfa ya Richmond. Kamati Teule ya Bunge iliundwa na kutoa taarifa za ovyo sana, na hatimaye kwa kulinda heshima ya serikali na chama akajiuzulu.

"Lowassa sio kwanza kuwajibika kisiasa, ktk awamu ya kwanza ya Mwalimu - kuna viongozi wa kisiasa waliuzulu. Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwinyi, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga na Mkurugenzi wa Usalama Taifa wote walijiuzulu kisiasa na Mwalimu aliwashukuru kwa kuwajibika.

"Lowassa alijiuzulu kuwajibika kisiasa, lakini ikabadilishwa kuonekana ni yeye ndiye aliyefanya makosa, ndio ukaanza wimbo wa ufisadi. Serikali yenyewe ilimsafisha kupitia TAKUKURU, lakini wimbo wa ufisadi ukaendelea, wakaja na wimbo mwingine wa Gamba.

"Yote haya yalipangwa na 'KITENGO' kilichoandaa kashfa ya Richmond. Edward ana historia ndefu ndani ya Chama.” aliendelea mzee Kingunge.

Kwa mujibu wa Kingunge, Wilaya ya Monduli ni moja ya wilaya ambayo mambo ya Chama yanaenda vizuri sana, na Kinana alimsifu Lowasa kwa hilo kuwa amekitumikia chama.

Kingunge anadai Lowassa amekuwa mtendaji mzuri hata serikalini, kila sehemu aliyopitia alionyesha namna alivyoweza kushughulikia matatizo ya wananchi.

Anadai mradi wa maji wa Ziwa Victoria, walishindwa wakoloni lakini limewezekana chini yake Lowassa akiwa waziri wa maji.

Amesema Lowassa kila alipoenda amefanya vizuri, na huu mchakato huu wa juzi ndani ya CCM umeonyesha wazi Lowassa anapendwa na watu.

"Zipo hadithi za kijinga kwamba watu wanaojitokeza wamepewa pesa, ni mawazo ya watu waliofilisika. Watu wanamlilia Lowassa hawamjui, hizo zote pesa zote anatoa wapi? Ana kiwanda cha pesa - hata angekuwa Bakheresa asingeweza!” alisema mzee Kingunge.

Mzee Kingunge alisema Lowassa ana kila sifa ya kuwa Rais na mwenyekiti wa Chama, mwingine yeyote inabidi ajifunze sana haya. Akasisitiza kuwa 'Uongozi wa Chama na Nchi umetumia nguvu kubwa sana kupuuza wananchi wanataka nini na kuhakikisha wanayempenda hapati kitu.

"Yalitokokea Dodoma yametia doa kubwa ktk historia ya Chama chetu chenye kuheshimika sana nje na nchi kiujumla. Nchi ili itengamae lazima chama kinachoongoza kijiendeshe kwa misingi ya haki na demokrasia, yaliyojiri Dodoma yametia dosari kabisa. Yaliyotokea Dodoma ni uvunjani wa misingi ya haki - wagombea walipaswa kusikilizwa kwenye Kamati kuu, walivunjiwa heshima na kunyimwa haki…” alisema mzee huyo.

"Chama kilichofanya maamuzi ya Dodoma hakikuwa chama kinachozungumziwa kwenye Katiba. Nawaomba viongozi wetu warudi kusoma ahadi za mwanachama, warudi pia wasome utangulizi wa katiba ya CCM. Kilichotokea Dodoma hakikubaliki, si halali na si haki.” alisema mkongwe huyo ndani ya CCM.

Kwa mujibu wa mzee Kingunge, pamoja na haya yote lakini Chama lazima kiendelee. Amesema CCM imempata mgombea, ndugu Magufuli, maneno yake ya leo hayamhusu yeye, yeye hakuwepo ktk 'KITENGO' cha kuharibu mambo.

Mzee kingunge ameongeza kuwa Lowassa yupo tayari kushirikiana na Chama kusaidia Chama kupata ushindi wa kishindo kwenye uchaguzi mkuu, lakini yaliyotokea lazima yazungumzwe kwa uwazi ndani ya vikao vya Chama ili watu watoe madukufuku yao.

Kingunge anadai Mkutano Mkuu umetamka Mgombea ni Magufuli, lakini ili kupata ushindi - chama kitahitaji nguvu na ushirikiano wa ndugu Lowassa na kuongeza kuwa anaamini Ndugu Magufuli atafurahia suala hilo na ataandaa mazingira mazuri ya kuipata sapoti hiyo.

Anadai Kabla ya Uchaguzi inabidi CCM kufanya mazungumzo ili wakubaliane na kukosoana lakini mwisho wa siku watoke tukiwa wamoja ili kupambana na adui.

Mzee huyo amedai Lowassa pia aliwashinda wote waliomtaka kuvua gamba na akaendelea kubaki ndani ya Chama.

Kingunge ameulizwa wakati wa Richmond alikuwa mbunge lakini hakuonekana kumtetea Lowassa, kwanini? Amedai 'Vitu vingine havipaswi kusema hadharani, niliona mambo yameharibika, nikakaa na Lowassa nikamshauri awajibike kisiasa.’

Ameulizwa kama ana mpango wa kurudisha kadi ya Chama kuonyesha kutokuridhishwa na uvunjifu wa katiba ya Chama; akajibu 'Siku nikitaka kurudisha kadi yangu nitawaambia, mimi kadi yangu namba 8 na nilihusika ktk kuunda chama hiki, nikifikia maamuzi nitasema.’

Mwisho amemalizia kwa kusisitiza: “Yaliyotokea Dodoma si halali na si haki…”

Asanteni

JF: SAUTI YA MZEE KINGUNGE AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI
[/Q
huyo aliyekaa pembeni mwa Kingunge ni nani?
 
Back
Top Bottom