Kinondoni, Dar: Hamza Mohammed, Polisi Watatu na mlinzi mmoja wauawa katika Majibizano ya Risasi

Kinondoni, Dar: Hamza Mohammed, Polisi Watatu na mlinzi mmoja wauawa katika Majibizano ya Risasi

Guys I am informed there’s a guy shooting randomly near Stanbic Bank, anyone with more news?

Inadaiwa kuna watu wameuawa. Ni Karibu na Makao Makuu ya Stanbic.

========

Mtu mmoja ambaye alionekana kufyatua risasi karibu na Ubalozi wa Ufaransa Jijini Dar es Salaam amedhibitiwa na Vyombo vya Ulinzi na Usalama

Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, (IGP) Simon Sirro amethibitisha kuuawa kwa askari wawili kwenye mapambano ya kurushiana risasi yaliyotokea eneo la Daraja la Salenda jirani na Ubalozi wa Ufaransa, Dar es Salaam.

Tukio hilo limetokea leo Jumatano Agosti 25, 2021 baada ya mtu mmoja ambaye hajafahamika kuzua taharuki baada ya kufyatua hewani risasi huku akisikika akisema kuwa anawatafuta polisi.

Akizungumza katika kikao kazi cha maofisa wa polisi, Sirro amesema mtu huyo naye ameuawa kwa kupigwa risasi.

“Mmeziona clip zinaruka sasa hivi akaingia barabara kubwa akawa anatamba na SMG na yeye amepigwa risasi na askari wetu hivyo, askari wetu wamefariki na yeye amefariki” amesema IGP Sirro.

Ameeleza kuwa wanaendelea kufuatilia kufahamu mtu huyo ametokea wapi na baadaye watatoa taarifa kamili.

IGP Sirro amenukuliwa kupitia kipande cha video kilichorushwa kwenye mtandao wa kijamii wa Wasafi Fm.

PIA SOMA:
1. Mashuhuda wasimulia tukio la aliyekuwa akipiga risasi

UPDATE: Waliouawa ni Polisi Watatu na Mlinzi mmoja, wengine sita wajeruhiwa.
Jeshi la Polisi limesema idadi ya Watu waliouwawa na Mtu mwenye Bunduki aliekua akifyetua risasi ovyo karibu na Ubalozi wa Ufaransa Dar es salaam ni Watu wanne huku kati yao Watatu wakiwa ni Polisi na mmoja ni Mlinzi wa Kampuni binafsi ya ulinzi.

"Leo August 25 2021 tumekutwa na tukio baya kabisa, tukio la kihalifu ambalo limepoteza maisha ya Watu wanne na watatu kati yao ni Askari Polisi, limetokea katika makutano ya barabara ya Kenyatta na Kinondoni Askari wetu walikua kazini akatokea Mtu akawashambulia kwa Bastola na alipowashambulia na kuanguka alichukua Bunduki za Askari hao na kuanza kurusha risasi ovyo kuelekea Ubalozi wa Ufaransa"

"Ukiachia Watu wanne waliouwawa leo tuna Watu 6 ambao wamejeruhiwa kwenye tukio hili na wanaendelea na matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, taarifa zaidi tutaendelea kupeana kadri muda unavyokwenda, ni mapema sana kubaini kwanini alifanya vile lakini tumeshaanzisha Timu ya upelelezi na muda sio mrefu tutakamilisha"

"Kuhusu baadhi ya video kusema kwamba huyu Mtu ni Mkazi wa Upanga sisi hatuthibitishi mambo kupitia clips za video, tunathibitisha mambo kupitia upelelezi kwahiyo upelelezi ndio utakaoeleza, kuhusu swali la Waandishi kuhusu kuwepo kwa dalili zozote za ugaidi kwenye tukio la leo hatuwezi kusema chochote hii ni mapema lakini uchunguzi ndio utakaosema kama kuna ugaidi au hakuna ugaidi"

"Kwa sasa hatuwezi kusema amekutwa na kitu gani mfukoni, Polisi bado wapo eneo la tukio... ni mapema sana kusema amekutwa na nini kwasababu Wataalamu wapo kazini, kuhusu kama ni Raia kama sio Raia uchunguzi ndio utasema baada ya upelelezi kukamilika tunachojua sasa huyu ni Muhalifu"


View attachment 1907510
View attachment 1907511


View attachment 1907519


Hii ni developing news…

Kuna mtu mmoja, kapigwa risasi na kuanguka katikati ya barabara
View attachment 1907602
View attachment 1907621
View attachment 1907645View attachment 1907646
Huyu anadaiwa kauawa.
Aisee.
Sijui kwa nini hili tukio limenikumbusha lile la askari waliouawa huko temeke na watu wasiojulikana na kufuatia jingine kwa askari kuuawa huko pori la wapi sijui iliposemekana kuna nyumba inaaminiwa ina magaidi.
Matukio haya yalitokea wakati wa vugu vugu la maandamano yaliyotangazwa na chadema ya UKUTA.
Poleni ndugu za wafiwa na RIP marehemu wote
 
Pumbafu kabisa lieua askari wetu wawili, hili wangelikamata wakalinyoa ndevu kwanza, halafu minya pumbu mpaka aseme nani kamtuma, pumbafff
Askali Ni watatu[emoji116]
IMG-20210825-WA0025.jpg
 
Tatizo mama Samia anajifanya mjuaji kudharau watangulizi wake wote waliowakomalia migaidi hiyo mishehe ya uamsho

Raisi shein mwislamu mwenzao aliwakomalia ,Kikwete mwislamu mwenzao aliwakomalia , Magufuli akawakomalia yeye ndie anajitia mjuaji akawaachia

Walichofanya kimataifa ni kitu kikubwa .Ubalozi wa ufaransa unatazamana na ulipokuwa Ubalozi wa Marekani ambapo magaidi walishambulia .

Message wanayo send Ni kwamba ok all past presidents walitudhibiti we have our own president now we are back!!! To prove we attack the same place we attacked
Wewe utakuwa ni mccm. Na siasa za chuki zimekuingia vilivyo. Chuki dhidi ya principal muslim, hao uliowataja ni culture Muslim ambao wameathiriwa zaidi na imani ya kijamaa kuliko ya kiislam.

Tukio hili ni la kihalifu kama Uhalifu mwengine. Kunasibisha na ugaidi, tena wa waislam ni ujinga wa km sisiem tu ulionao.
 
nawapongeza sana Askari wetu kwa kazi nzuri.
nashauri Msako ufanyike nyumba kwa nyumba Hoteli kwa hoteli, bar kwa bar.
Majambazi tunaishi nao ktk maeneo yetu mitaa yetu, mahoteleni n.k.
Polisi wetu tunawaomba kamwe msilale. Badilisheni mbinu.
Majambazi sio wakuwachekea washa moto tu, pigeni risasi hawa watu wafe wote.
wasakeni hata wakiwa shimoni.
 
Hili gaidi kuua askari wawili ni uzembe wa askari... limezunguka muda mrefu, askari walikuwa wapi?

mkuu ni vyema tu uendelee kuwa unaangalia movie na kuziacha huko huko sebuleni.

neno"uzembe"kuna baadhi ya kazi halifai kuwekwa.either litapwaya au litabana kwenye maana yake.

wakati askari akifikiri namna bora ya kutatua changamoto zinazokukabiri ukiwa na mkeo na wanao,gaidi anapiga mahesabu ya kummaliza askari.shukuru hakuamua kuwageukia raia wengine.
 
Aisee.
Sijui kwa nini hili tukio limenikumbusha lile la askari waliouawa huko temeke na watu wasiojulikana na kufuatia jingine kwa askari kuuawa huko pori la wapi sijui iliposemekana kuna nyumba inaaminiwa ina magaidi.
Matukio haya yalitokea wakati wa vugu vugu la maandamano yaliyotangazwa na chadema ya UKUTA.
Poleni ndugu za wafiwa na RIP marehemu wote
Naanza kuunganisha dots kuwa uenda ni tukio la kupangwa ili kuandaa mazingira ya kuzuia makongamano ya katiba yaliyopangwa na CHADEMA.

Kwa suala la CHADEMA hawa policcm wanaweza fanya lolote baada ya excuse ya covid19 kuonekana imefeli.
 
Hapo mwisho umeamua kumalizia kisomali ki warrior kabisa?
Leo nimekuwa msomali baada ya awali kuniita mzanzibari mmakunduchi ?!!!

Yaani mkuu hujui maana ya "KEDI"?!! Khaa 😲😲😲

Kiswahili cha kawaida na kisicho lahaja za huko usemako......

Mkuu Brazaj banaa naamini wewe huna OBSESSIVE COMPULSIVE DISORDER!! 🤣

#KaziIendelee
#SiempreJMT
 
Back
Top Bottom