Kinondoni, Dar: Hamza Mohammed, Polisi Watatu na mlinzi mmoja wauawa katika Majibizano ya Risasi

Kinondoni, Dar: Hamza Mohammed, Polisi Watatu na mlinzi mmoja wauawa katika Majibizano ya Risasi

Huyo mtu alikuwa hana damu? Mbona haikuchuruzika kwenye lami,halafu alipogeuzwa alikunja goti.Tazama video vizuri.
Screenshot_2021-08-25-13-25-37-739_com.android.chrome.jpg

Hayo maji ?!
 
Achana na kwamba wangekua wawili...
Yaani yule yule mmoja angekua serious, angesumbua sanaa, Yule kutoka barabarani na wao ndio kumpiga ni sawa na kajiua mwenyewe,
Na kama umeangalia vzr hata wakati yupo pale katikati ya Barabara tena hafyatui anapiga kifua bado wanamkosa wanapiga Lami...

Wajitafakari,
Lakini kikubwa LimekufaView attachment 1908060
Kikubwa wamemuuwa ndiyo ila mtuhumiwa kama yule kumuuwa bila kutengeneza mazingira ya kumuhoji may be wapo watu nyuma yake ukapata pakuanzia police wamefamba.

Hatukatai chuma ni hatari ila kama taifa tuna snipers ilifaa watumie uzoefu wao kumletea majeruhi ili wamkamate hai asaidie upelelezi.
 
Kapigwa bastola na askari aliyekuwa bank ya stanbic bank ambako kulikuwa na maaskari wakirusha risasi, na yeye kuanza kuelekea zinakotokea hizo na wasingemuwahi angeingia stanbic maana askari aliyekuwa ukuta wa stanbic na aliyemleta ya kichwa angechelewa ingekula kwao

Mimi nikiwaza Askari Watatu na Mlinzi mmoja wa SGA wapo Mochwali inauma sana. Sasa sijajua, yule askari aliyepigwa pale nje ya Ubalozi wa Ufaransa, akijaribu kumuua huyo Mhalifu kwenye Kibanda sijui kapona? Maaana alipigwa Risasi na Hilo lijamaa.
 
Kulingana na hyo clip huyo kijana alikuwaga na akili ka zimeruka jeuri na msumbufu ndio akapelekwa Egypt kusoma dini na aliporudi Tanzania akawa anataja mambo ya jihadi
Itupie basi tuione
 
Jambo moja na la ajabu sana ni hili.
[emoji1484]
-Yule jamaa katoka wapi na siraha zile pasi kushukuliwa?.
-Kuna kitu kimejificha kutokana na tukio hilo?.
-Ametumwa kupima ulinzi wetu ukoje?.
-Kwa nini bakuwa na habari na raia waliokuwa jirani?.
-
Na tushukuru Mungu hakuhangaika na ile daladala iliyokuwa mbele yake alipokuwa anajipiga piga kifua tungekuwa saizi tunaongea mengine hapa.
 
Walikuwa wanawasema vibaya alishabaab, vita yao na wakenya lakini mmatumbi kutoka tandale na mitaa fulani anaingilia ishu yao,,,haya sasa kumekucha mammae,,,na walivyo waoga [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] Mungu atunusuru kwaakweli.
Kabisa mkuu tuombe MUNGU atunusuru.
 
Kuna askari mmoja ameenda kifara fara pale kwenye banda na kibastola chake halafu akawa anatoa ishara kwa wenzake huku kageukia huko huko kwa wenzake badala amwangalie adui..acha ale shaba ya mguu; akaanza kuruka ruka!!!!
 
Alikuwa na maamuzi ya kweli ktk maangamizi na kasomea Misri mambo ya Dini
IMG-20210825-WA0016.jpg
Screenshot_20210825-173012.jpg
 
Kuna askari mmoja ameenda kifara fara pale kwenye banda na kibastola chake halafu akawa anatoa ishara kwa wenzake huku kageukia huko huko kwa wenzake badala amwangalie adui..acha ale shaba ya mguu; akaanza kuruka ruka!!!!
Pale hata mimi nilishangaa amemuachia adui mgongo je angepigwa ya kisogo
 
Guys I am informed there’s a guy shooting randomly near Stanbic Bank, anyone with more news?

Inadaiwa kuna watu wameuawa. Ni Karibu na Makao Makuu ya Stanbic.

========

Mtu mmoja ambaye alionekana kufyatua risasi karibu na Ubalozi wa Ufaransa Jijini Dar es Salaam amedhibitiwa na Vyombo vya Ulinzi na Usalama

Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, (IGP) Simon Sirro amethibitisha kuuawa kwa askari wawili kwenye mapambano ya kurushiana risasi yaliyotokea eneo la Daraja la Salenda jirani na Ubalozi wa Ufaransa, Dar es Salaam.

Tukio hilo limetokea leo Jumatano Agosti 25, 2021 baada ya mtu mmoja ambaye hajafahamika kuzua taharuki baada ya kufyatua hewani risasi huku akisikika akisema kuwa anawatafuta polisi.

Akizungumza katika kikao kazi cha maofisa wa polisi, Sirro amesema mtu huyo naye ameuawa kwa kupigwa risasi.

“Mmeziona clip zinaruka sasa hivi akaingia barabara kubwa akawa anatamba na SMG na yeye amepigwa risasi na askari wetu hivyo, askari wetu wamefariki na yeye amefariki” amesema IGP Sirro.

Ameeleza kuwa wanaendelea kufuatilia kufahamu mtu huyo ametokea wapi na baadaye watatoa taarifa kamili.

IGP Sirro amenukuliwa kupitia kipande cha video kilichorushwa kwenye mtandao wa kijamii wa Wasafi Fm.

PIA SOMA:
1. Mashuhuda wasimulia tukio la aliyekuwa akipiga risasi

UPDATE: Waliouawa ni Polisi Watatu na Mlinzi mmoja, wengine sita wajeruhiwa.
Jeshi la Polisi limesema idadi ya Watu waliouwawa na Mtu mwenye Bunduki aliekua akifyetua risasi ovyo karibu na Ubalozi wa Ufaransa Dar es salaam ni Watu wanne huku kati yao Watatu wakiwa ni Polisi na mmoja ni Mlinzi wa Kampuni binafsi ya ulinzi.

"Leo August 25 2021 tumekutwa na tukio baya kabisa, tukio la kihalifu ambalo limepoteza maisha ya Watu wanne na watatu kati yao ni Askari Polisi, limetokea katika makutano ya barabara ya Kenyatta na Kinondoni Askari wetu walikua kazini akatokea Mtu akawashambulia kwa Bastola na alipowashambulia na kuanguka alichukua Bunduki za Askari hao na kuanza kurusha risasi ovyo kuelekea Ubalozi wa Ufaransa"

"Ukiachia Watu wanne waliouwawa leo tuna Watu 6 ambao wamejeruhiwa kwenye tukio hili na wanaendelea na matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, taarifa zaidi tutaendelea kupeana kadri muda unavyokwenda, ni mapema sana kubaini kwanini alifanya vile lakini tumeshaanzisha Timu ya upelelezi na muda sio mrefu tutakamilisha"

"Kuhusu baadhi ya video kusema kwamba huyu Mtu ni Mkazi wa Upanga sisi hatuthibitishi mambo kupitia clips za video, tunathibitisha mambo kupitia upelelezi kwahiyo upelelezi ndio utakaoeleza, kuhusu swali la Waandishi kuhusu kuwepo kwa dalili zozote za ugaidi kwenye tukio la leo hatuwezi kusema chochote hii ni mapema lakini uchunguzi ndio utakaosema kama kuna ugaidi au hakuna ugaidi"

"Kwa sasa hatuwezi kusema amekutwa na kitu gani mfukoni, Polisi bado wapo eneo la tukio... ni mapema sana kusema amekutwa na nini kwasababu Wataalamu wapo kazini, kuhusu kama ni Raia kama sio Raia uchunguzi ndio utasema baada ya upelelezi kukamilika tunachojua sasa huyu ni Muhalifu"


View attachment 1907510
View attachment 1907511


View attachment 1907519


Hii ni developing news…

Kuna mtu mmoja, kapigwa risasi na kuanguka katikati ya barabara
View attachment 1907602
View attachment 1907621
Siyobalshababu??View attachment 1907645View attachment 1907646
Huyu anadaiwa kauawa.
Siyo alshababu?
 
Duh, hizi akili nyingine bana, kwa hiyo drama zinatengenezwa jamaa anatishia anaua polisi na yeye anauliwa!!

Najaribu kuwaza tu🤣🤣🤣

Pale palikuwa hamna drama, jamaa tu fyatu na akili zake, hakuelewa anataka nn, inawezekana hana akili timamu au kapandwa na mashetani yule,

Polisi walitakiwa wamkamate live wajue intention yake nnni haswa!!
Umewaza mbali, kudos sana,kumbe kungekuwa na utaratibu wa kumpiga na risasi ya usingizi,mda ana zinduka angetoa siri nyingi kama mfano Alshabab wamemtuma au vinginevyo.
Huwa nafuatilia sana zile police chase kwenye majiji ya Marekani,jinsi police wao wanavyofukuzia majambazi na kuwakamata wakiwa hai,gari zisizopungua tano zinafukuza gari moja ya jambazi,hewani kunakuwa na helcopter mbili moja inaenda kwa chini kidogo ikisaidia kufukuza nyingine inakuwa juu sana ikiwa inawawezesha polisi waliopanda kuona sehemu kubwa ya barabara za jiji husika,wakikaribia gari la mhalifu Wanajaribu kushoot matairi,lakini hatimaye huwa wanahakikisha wemkamata akiwa hai ilo atoe Siri za operation zake.
 
Itakie mema nchi yako,hakuna furaha katikati ya umwagaji damu.
Mkuu nasikitika sana kwa haya yanayotokea tena sana tu.Mimi ni Mkristo ninaye amini ktk kuishi kwa Amani na Upendo,lkn Dhuluma inafanya watu watafute haki kwa njia nyingine.Ndio maana Ktk Biblia kuna sehemu imeandikwa hivi "Haki huinua Taifa". Hivyo viongozi wetu wajitafakari.
 
Back
Top Bottom