Ushauri kwa Intelejensia ya Polisi:
1.Mnakumbuka mtandao wa watu wanaovusha "raia kutoka pembe ya afrika"(Halafu tunadaganywa kuwa ni waethiopia"wamekamatwa wakielekea Msumbiji au Afrika Kusini.
2.Wizara ya mambo ya ndani imeshawahi kuomba fedha ya kufunga mashine za "scan" ili raia wa kigeni wanaoingia nchini picha zao zichukuliwe na kuwa kwenye kumbukumbu za Idara ya Uhamiaji??(Leo kazi ingekuwa ndogo, maana tungesoma mfumo wa "data" za wageni walioingia, waliopo na wanatokea wapi na nani ni mwenyeji wao, watakaa nchini kwa muda gani na kwa shughuli ipi?!!).
3.Je?!zile camera za mitaani zilifungwa,zinafuatiliwa zifungwe maeneo muhimu.Maana naiona fedhaa nyingine ,kama ubalozi wa ufaransa na taifa lolote la nje likitoa taarifa ya mtu aliyefanya tukio hili halafu sisi tuishie kusema "uchunguzi" unaendelea.
Nawashauri vyombo vya dola:
1.Chukua picha, twende nchi jirani kwa ajili ya "scan" tujue ametokea wapi, tujipange kushughulika na mtandao wa mhalifu huyu.
2.Mjikumbushe/muwakumbushe wanasiasa/watawala umuhimu wa vyombo vyetu vya dola kuishi kitaaluma zaidi badala ya kuishi kisiasa,matokeo yake kutumika kisiasa na hivyo kupoteza muda wa kulinda maslahi ya taifa, na kukimbizana na raia wanaotafuta haki zao za kikatiba kutoka kwa watawala.