Kinondoni, Dar: Hamza Mohammed, Polisi Watatu na mlinzi mmoja wauawa katika Majibizano ya Risasi

Kinondoni, Dar: Hamza Mohammed, Polisi Watatu na mlinzi mmoja wauawa katika Majibizano ya Risasi

Tukio lililotokea leo jijini Dar wote limetuacha na maswali mengi. Wakati vyombo vya usalama vikiendelea kulitakafakari na kujiuliza mengi kuhusu tukio hili la kusikitisha, sisi wananchi tunalilaani sana na tunapongeza vyombo vya ulinzi na usalama kwa kuchukua hatua za haraka na za kishujaa kulidhibiti.

Pengine madhara yangekuwa makubwa zaidi. Tunawapa pole sana walioathirika na tukio hili kwa namna yoyote ile zikiwemo familia za maaskari wetu shujaa walioripotiwa kuwa wameuawa katika tukio hilo. Inasikitisha sana.. Matukio kama haya yanadhihirisha umuhimu wa serikali kuongeza nguvu katika kufuatilia na kuwatia kwenye mkono wa kisheria yeyote anayetuhumiwa kuhusika na masuala ya uhalifu na ugaidi bila kujali rangi, dini, kabila, cheo wala itikadi yake ya chama.

Yeyote anaweza kufanya uhalifu na yeyote anaweza kuwa gaidi. Kuna wengine wamekuwa wakipima suala la ugaidi na kiwango cha pesa. Wanataka wasikie kiasi cha mabilioni na matilioni yanatajwa. Hivi huyu jamaa wa leo, ametumia matilioni mangapi kufanya alichoweza kufanya? Nasikia hata bunduki aliyotumia amepora kwa askari (kama ni kweli).

Uhalifu na ugaidi uko zaidi kwenye fikra kuliko kiwango cha pesa. Kwa anayekamatwa vyombo vya sheria ni bora kuhakikisha kuwa sheria inatumika kwa usahihi na anayepatikana anapewa adhabu kali kwelikweli. Ni nani aliyejua kuwa huyo jamaa angeweza kufanya tukio hilo lililoshtua jiji na nchi nzima.?

Hakuna anayeweza kusema kwa uhakika wa nafsi yake kuwa fulani siyo mhalifu, au fulani siyo gaidi. Hakuna, si askofu, si mfuasi wa chama, si mwanafamilia, si yeyote. Hakuna. Muhimu ni kuacha vyombo vya usalama na upelelezi kufanya kazi yao na sheria kuchukua mkondo wake.
Yani umajipinda kuandika kote huko ila kilichokushinda na ambacho ulitamani uweke kwenye bango lako ni neno/jina moja tu MBOWE
 
Back
Top Bottom