Kuna mahala hapapo sawa detection ya hili tukio haikuwepo kweli?mpaka huo msafara unageuzwa na wananchi maana yake hakuna watu hapo mbele ambao walikua wanaconnection na msafara?means hakukua na wafagia barabara?
Huyu jamaa zimetumika risasi nyingi sana zaidi ya 50 na zilizomuangusha hazifiki 4 ...
Ok sawa ni gaidi kwann hakuzimishwa ili tukakae nae chini tujue alikua anataka nini na katoka wapi na wapo wangapi??
Nina jiuliza mengi kichwani....
Mkuu kwa ufahamu wangu mdogo kumzimisha mtu kama huyo ni process.
Pengine askari walikuwa wako horizontal na huyo mtu alafu hayo ni makazi ya watu,lazima askari wawe wqtulivu sana kwa sababu wakikosea ujue SMG risasi yake inaenda umbali wa zaidi hata ya KM 3 hivyo wakimkosa basi ndani ya umbali wa 3km ikimgusa mtu anaanguka.
Askari wakitumia vibaya risasi zao kupigapiga tu na risasi inaenda masafa marefu matokeo yake ni kuuwawa watu wasio na hatia.
Ingelikuwa rahisi sana kama kuna sniper yuko juu huyo jamaa angelipotea kabisa.
Lakini shida ni kuwa wote wapo chini,adui hana cha kupoteza kwa sababu yeye unaweza kumpiga risasi ya mguu ili kumzima nguvu lakini ukimpoga risasi ya mguu ile silaha yake pale mkononi una uhakika gani lama ataiwacha ?
Kitendo cha kumpiga maeneo ambayo hayauwi ili kutokupoteza ushahidi hii inaweza kumfanya apanick zaidi kwa sababu ya maumivu ma hapo angechanganyikiwa.
Na kuchanganyikiwa huko kungepelekea yeye afyatue risasi ovyo ovyo kumtafuta nani kampiga,jambo hili lingepelekea kufa qatu ambao hawana hatia alafu wangeambiwa polisi ndio ambao wameuwa kwa kukosa ulengaji.
Kumbuka jamaa alikuwa na bunduki mbili ambazo kila moja ilikuwa na full magazine ya risasi 30,hivyo angelikuwa na risasi 60.
Risasi moja tu inatosha kuuwa mtu mmoja,mannake risasi hizo 60 angelizifyatua ovyo angelipata kuuwa watu 60 ambao hawana hatia.
lakini askari anatakiwa aangalie akilenga akamkosa hatodhuru watu wengine wa pembeni ama walioko mbali ?
Mana kwa eneo lile ukienda kilomita mbili kila eneo lazima kuna raia.
Sasa kama risasi inaweza kuuwa hata umbali wa 3Km na lile eneo ndani ya 2km kuna raia hapo jiulize ingelikuwaje
Na inategemea askari yupo engo gani.
Kuna clip nimeiona askari akiwa anatambaa chini kumuwinda huyo jamaa nitaiweka hapa chini.
Matukio kama hayo raia anachanganyikiwa sisemi kwa askari ambae anatakiwa awalinde watu na kujilinda mwenyewe.0