Kinondoni, Dar: Polisi watawanya raia waliokuwa kwenye mikusanyiko mida ya usiku

magufuli katuachia UHURU kwanini wanataka kutubana bana.?

"baba unahonga hawara elfu kumi,
watoto wanakufa na njaa nyumbani"
 
Chamsingi watu wajiongeze juu ya hili si mpaka serikali itumie nguvu kukaa ndani
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kupiga viboko haisaidii..lock down ndiyo suluhu...ingawa sidhani Kama tutaweza imudu.

Poleni dar..huku Moro bado viboko havijatufikia
 
Jana usiku polisi walivamia mabaa ya kinondoni wakitawanya watu na kuwapiga viboko,ni vizuri wangetangaza officially watu wajue wafahamu.

Clouds Fm wakimhoji mkuu wa wilaya kinondoni amesema kwamba watu hawajielewi kuna corona halafu wanaleta mikusanyiko,na kasema yeye ndo kaagiza watandikwe na kama kushitakiwa ashitakiwe ila amewaepusha na corona.

Ila mwishoni kasema baa iwe na level seat na kukaa umbali wa zaidi ya mita moja baina ya watu,watafunga mabaa hadi pale agizo rasmi litakapotolewa

NB.Lakini kwa wakati kama huu watu pia hawajielewi,kuna maambukizi ya Corona bado wanaenda kwenye starehe na mziki wanalewa.

♡♤Life belongs to all who struggle for it♤♡♧
 
Nimewaunga mkono serikali ya ccm kwa mara ya kwanza kwa hili, mtu akiishalewa kweli hawezi kuwa na tahadhari ya huu ugonjwa wa korona

Na wapigwe tu.
Sent using Jamii Forums mobile app
 

Ah sasa si watangaze lockdown ieleweke moja?

Mambo ya kufurumisha watu kama utumwa haina maana
 
sio kila mtu anauwezo kama wako kunabaadhi ya watu hawawezi kupata chakula mpaka watoke majumbani mwao. Ninakumbuka sikumoja mwalimu nyerere alisema kuwa tumebakiwa na maadui watatu nao ni umaskini,ujinga na maradhi. Fikilia kabla ya kusema jambo
 
Wakalewe nyumbani tuvumilie kipite kipindi hiki kwanxa

Ni kweli, ila sio sahihi kumchapa mtu wakati hakuna Katazo. Ni vyema wakaweka Katazo kisha watu wakikiuka ndio adhabu zitolewe, tena sio kwa kupigwa na polisi huko mabar, bali kufunguliwa mashitaka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…